PreGE2025 Tabora: Watendaji wa vituo vya uboreshaji wa daftari la wapiga kura washiriki tamko la kujitoa uanachama wa vyama cha siasa

PreGE2025 Tabora: Watendaji wa vituo vya uboreshaji wa daftari la wapiga kura washiriki tamko la kujitoa uanachama wa vyama cha siasa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Wont be the same

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,564
Reaction score
2,483
Watendaji wa vituo wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, Mkoani Tabora katika uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wakitoa tamko la kujitoa uanachama wa chama cha siasa au kutokuwa mwanachama wa chama cha siasa na kiapo cha kutunza siri, mbele ya Afisa Mwandikishaji (hayupo pichani) kabla ya kuanza kwa mafunzo yao ya siku moja leo Aprili 29, 2025. Mafunzo hayo ni sehemu ya maandalizi ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya pili.

Uboreshaji wa Daftari awamu ya pili unafanyika sambamba na uwekaji wazi wa Daftari la Awali la Wapiga Kura kwenye mikoa ya Geita, Mara, Kagera, Shinyanga, Mwanza, Simiyu, Rukwa, Tabora, Katavi, Kigoma, Iringa, Ruvuma, Njombe, Mbeya na Songwe. Mazoezi hayo kwenye mikoa tajwa yatafanyika kwa siku saba kuanzia tarehe 01 Mei, 2025 hadi tarehe 07 Mei, 2025.
1745927139407.png
 
Back
Top Bottom