Tabora: Wanafunzi wote waliopata mimba kuendelea na masomo

kISAIRO

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
1,796
654
Ndugu wana JF,

Mkuu wa Mkoa wa Tabora ametoa maamuzi yafuatayo;

Wanafunzi wote walioacha shule kutokana na kupata ujauzito,utoro,kuozeshwa na wazazi wameamriwa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri kurudi shule mara moja,nakusema kuwa waliowaoa ama kuwapa ujauzito watajulikana mbele ya safari sheria zitakapo anza kuchukua mkondo wake.

Chanzo: ITV

Mytake: Hii ni hatua nzuri kwani kumfukuza shule mwanafunzi aliyepewa mimba sio suluhisho la tatizo ila ni vizuri tukarekebisha sheria na sera zetu tuweke haya mambo kisheria.
 
Mwanriii.jpg

Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri amesema kuwa wanafunzi wote walioacha shule kutokana na kupata ujauzito, utoro au kuozeshwa na wazazi wanatakiwa kurudi shule mara moja.

Amesema kuwa wote waliowaoa ama kuwapa ujauzito watajulikana mbele ya safari sheria zitakapoanza kuchukua mkondo wake.
 
Huyu mzee mimi huwa namuaminia sana, hata kukosa ubunge kilichomponza ni uccm wake tu sio zaidi ya hapo
 
Hii imekaa vema sana, huwa inatia huruma kuona binti anapewa mimba anafukuzwa shule, aliyempa mimba anamtelekeza, nyumbani binti anafukuzwa, ndugu hawamtaki tena (Kwa sisi wazazi tunajua ilivyo shughuli kumhudumia mwanamke mwenye mimba na mtoto). Hili waliweke kisheria kabisa, mwanafunzi akipata mimba asimamishwe shule hadi ajifungue kisha arudi kuendelea na masomo.
 
Ndugu wana JF,

Mkuu wa Mkoa wa Tabora ametoa maamuzi yafuatayo;

Wanafunzi wote walioacha shule kutokana na kupata ujauzito,utoro,kuozeshwa na wazazi wameamriwa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri kurudi shule mara moja,nakusema kuwa waliowaoa ama kuwapa ujauzito watajulikana mbele ya safari sheria zitakapo anza kuchukua mkondo wake.

Chanzo: ITV

Mytake: Hii ni hatua nzuri kwani kumfukuza shule mwanafunzi aliyepewa mimba sio suluhisho la tatizo ila ni vizuri tukarekebisha sheria na sera zetu tuweke haya mambo kisheria.
Safi kabisa Mh. Mwanri! Haki ya elimu ni ya kila mwananvhi wa Tanzania!
 
Lakini kwa upande mwingine hakutankuwa na hofu yeyote kwa wanafunzi kuwa wazinzi maana hana cha kuhofia nadhan litazamwe kwa mapana zaidi na vip kwa wale wasio na mimba watamuonaje huyo mwenzao? Na watakifunza nini au ndio tuna halalisha uzinzi mashulenimashuleni? Je huyo mjamzito atakuwa na confidence kukaa darasani na tumbo lake? Nadhana labda yafanywe marekebisho ya kurudia darasa, baada kumsimamisha masomo ili kujenga nidhamu ili kupunguza uzinzi mashuleni.
 
  • Thanks
Reactions: J C
Uzinzi umehakalalishwa aisee. Sheria itungwe kwa wanafunzi wa kiume pia kupokea adhabu sawa na wa kike .
 
Back
Top Bottom