Taboa yamuomba Dk. Mwakyembe kuzipiga `stop` Noah

kbm

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
5,222
1,670
Mgogoro kati ya wamiliki wa mabasikatika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha na wakuu wa mikoa hiyo umepamba moto, baada ya Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (Taboa), kumuomba Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, kuingilia kati.
Katika maombi hayo, Taboa inataka Dk. Mwakyembe awapige marufuku wakuu wa mikoa hiyo kutokana na kuanza kuwaruhusu wamiliki wa magari aina ya Noah kusafirisha abiria umbali mrefu kwa sababu sheria haziruhusu.
Katibu Mkuu wa Taboa, Enea Mrutu, akizungumza jana katika kipindi chaKumepambazuka kinachorushwa na Redio One Stereo, alisema baadhi ya wakuu wa mikoa ya Kanda ya Kaskazini wamekuwa wakiwakingia kifua wamiliki wa Noah kwa kuwaruhusu kusafirisha abiria umbali mrefu wakati sheria haziruhusu hivyo.
Mrutu alisema wamiliki wa mabasi hawaogopi ushindani wa kibiashara na wamiliki wa Noah, lakini wanachotaka ni kufuatwa kwa sheria kwa sababu baadhi yao hawana leseni za usafirishaji.
Alisema wanapowafuata viongozi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini Nchini (Sumatra) wanashindwa kuwachukulia hatua wamiliki wa Noah kwa kuogopa kufukuzwa kazi na baadhi ya wanasiasa.
Mrutu alisema ikifika Ijumaa ya wikihii kama Noah zitaendelea kusafirisha abiria umbali mrefu, watachukua hatua ya kusimamisha usafiri wa mabasi mikoani ili wawaachie wafanye kazi hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo, akijibu alisema Taboa haina mamlaka kuzungumzia masuala ya Noah kwa sababu Taboana wenye Noah wote wapo chini ya Sumatra.
Mulongo alisema suala la Noah mjadala ulishamalizika baada ya Waziri Mwakyembe kuruhusu zifanye kazi na Bunge likapitisha.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama, alihoji ilikopata Taboa mamlaka ya kuhoji suala la kwamba, wamiliki wa Noah hawanaleseni.
SOURCE: NIPASHE
 
Back
Top Bottom