Table manners - tusaidiane

1)Ukikohoa unaholea pembeni na unaweka mkono

2)Ukila ni vidole tu vinachafuka katikati na kijanja safiii

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
Kwa hiyo namba 2 ukila ugali inakuaje?
 

Hilo la mwisho limenishinda. Ukizidisha chumvi au ukileta kibichi nakupa live baada tu ya kijiko cha kwanza.
 
Koma!!!

Ila kwa sababu mtani usikome.

Table manners zetu zinaendana na mazingira yetu, kutupika kwa knife and fork ni kutuchosha tu.

Kuna watu wanatafuna kama mchwa, inakera sana.

I hate uma na kisu

Hata utamu wa chakula unapungua
 

Hahahahah kula ugali mlenda kwa uma na kisu
 
15. Kama utakuwa ukitumia uma na kisu kwa wakati mmoja uma hushikwa na mkono wa kushoto na kisu kiwe mkono wa kulia
16. Angalau mda wa dak 25-30 upite katika kutofautisha aina za vyakula ambavyo huliwa/kunywa vikiwa aidha vya moto au baridi.

Kula kwa mkono wa kulia siku zote kama si mtumia kushoto wa kuzaliwa.Usile wala kunywa ukiwa umesimama, labda kwa dharura.
 
Weka ishara ikiwa umemaliza kula.
Katikati ya sahani, weka umma wako kushoto kwako na kisu kulia, makali ya kisu yakielekea kwenye tongs za uma.
Hii ni ishara kwa mwenyeji wako au waiter kuwa umemaliza kula. Kitendo hiki kinatoa nafasi kuhudumiwa drinks.
 
1.usiji kunune kwa kutumia mkono unaolia chakula(ksma unakula kavu kwa mkono)
2.usisokomeze vidole mdomoni wala kulamba vidole wakati wa kula.
3.usimseme/ kumgombeza mtu wakati wa kula hata km amekuudhi vipi.
4.usisusie chakula hata uwe na hasira vipi.
5.usiunganishe chakula mdomoni meza kwanza ndipo uweke kingine mdomoni.
6.usiongee wala kucheka while chakula ipo mdomoni.
7. usibeue wa kucheua wakati wa kula......
 
Wakati wa msosi angalia speed ya wenzako ktk kula. Speed yako isiwe ndogo sana au kubwa sana. Usiweke mifupa au masalia ya chakula juu ya meza. Weka kwenye sahani. Usile 1/2 ya chakula ulichobeba ktk uma au kijiko. Pima kiasi kinachoweza kuingia kinywani mwako mara moja.
 
Kama ikitokea ukataka au kuomba chumvi,usiseme chumvi,sema naomba dawa ya mboga.
 


Kama tupo wawili tu aise hapo lazima nikuchane laivu
Ole wako ukawa mke wangu hahahaaaaa... utajuta
Nitakustiri tu kama wapo wageni
 
aseee mm nachukia sana mtu kula kama mbwa na kujilamba hadi vidole tena kama mwanaume asee ndo nakushusha thaman kabsa...mshua wang yeye kula huku unamwangalia usoni wakati uko mezani anakurushia kijiko.
Hapo kwenye kujilamba vidole kwa kweli nashindwa kuelezea, ukiangalia kwa jicho la tatu ni uchafu ambao hauelezeki

Tena wengine wanajiramba kila wakati ... mfano kila baada ya tonge kadhaa anajilamba ... halafu vidole vyote

Mimi hiyo nilishawahi kuiona mara nyingi sana tu nikiwa nimejikalia labda wengine wakiwa wanakula halafu wewe mgeni umekataa kujiunga nao

Inaelekea mshua wako alitoa mafunzo/maelekezo yenye maadili bora ila baadhi ya wahusika hawataki kuelewa ... ndio maana inafikia muda anashindwa kujizuia kwa hasira. Kwa kweli mtu ambae mgumu kufundishika tabia anatia sana hasira

Mshua wako kidume nampa mia
 

My wife was like u, ila nimeshambadili
Imagine unakula hivo utawezaje kuwakanya wanao
 
Kuna wakati mazingira hayaruhusu mkuu

Inabidi ukubali matokeo ule kwa nyenzo

Vinginevyo utapata kipindu pindu

Ni kweli
MaZingira yasiporuhusu natumia kwa shingo upande, ila ndo hata si-enjoy
 
Hapo kwenye kiganja kujaa msosi huwa panashangaza kabisa.

Ukila, usijipakaze chakula kwenye lips, na ikitokea, jifute mara moja. Hii inaweza kutia kinyaa kwa wanaokutazama.

1)Ukikohoa unaholea pembeni na unaweka mkono

2)Ukila ni vidole tu vinachafuka katikati na kijanja safiii

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…