TABIBU TV Imeanza vizuri

TABIBU TV Imeanza vizuri

LaVictoria

Member
Joined
Jul 23, 2016
Posts
11
Reaction score
79
Kwa watumiaji wa king'amuzi cha Startimes waliopo mkoa wa Dar es Salaam watakuwa wameiona channel mpya ya TABIBU TV ambayo ipo kwenye majaribio, jamaa wanaonyesha muvi kali na series za ukweli, bado haijajulikana mmiliki wa Tabibu Tv ni nani, wengine wanadai inamilikiwa na Dr Mwaka, lakini vyovyote itakavyokuwa jamaa wamefanikiwa sana kuliteka soko la TV za bongo, idadi ya watazamaji imekuwa kubwa sana na imekuwa gumzo kila kona.
Endeleeni namna hiyo hata mtakapoanza kurusha vipindi vyenu
 
Kwa jina la channel usitegemee wakianza kurusha matangazo yao rasmi watarusha tena hizo movie. Jiandae kwa Tiba Mbadala. Hayo ni majaribio tu mkuu.
 
kama ni dr mwaka kweli, basi huyu mjomba ni kiboko yao
 
Isije ikawa kama channel moja hivi yenye rangi ya kijani baada ya kutolipia kingamuzi chaneel zoote zimefutwa na kubaki hiyo moja tuu. Changamoto

1. Muda wote ni muziki

2. Muda wa asubuhi wapo bize na filim na muziki badala ya hata kuchambua yliojiri kwenye magazeti

3. Filim zaio nyingi ni PGA yaani zinahitaji usimamizi wa wazazi mbaya zaidi vipindi hivyo vinawekwa wakati wa mchana sasa muda huo nadhani wazazi wapo makazin.
 
Mbona umeambiwa wapo kwenye majaribio.
 
Kama ni ya mwaka..tujiandae kutangaziwa habari za kunywa madumu ya dawa
 
Kuna mpaka gazeti la Tabibu japo sijawahi nunua
 
Back
Top Bottom