Tabia zinazovunja ndoa/uchumba

bagain

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2011
Posts
363
Reaction score
230
Salaam wana MMU,

Uchumba mwingi na hata ndoa zinavunjika kila siku na sababu kubwa ikiwa ni madai ya watu kutokuendana kitabia.

Basi wana MMU tutumie nafasi yetu kuorodhesha hizo tabia hatarishi kwa wanaume na wanawake zinazopelekea ndoa/uchumba kuvunjika.

Itasaidia wanawake wawe "wife materials" na wanaume wawe "husband materials", na kwa kufanya hivyo taasisi ya ndoa itarudisha heshima yake.

Kwa kuanza mimi naona tabia hizi huondoa mwanamke kuwa "wife material"

~binti/mwanamke kuwa na tabia za kununa nuna, kuzira na kususa.
~uvivu wa kufanya kazi za nyumbani usafi, upishi n.k

Karibuni tusaidie kizazi hiki
 
ubinafsi ni mbaya sana kwenye mahusiano.
mtu anakuwa anajiwazia yeye tu na wazazi/ndugu zake.
upande mwingine wanaendelea kuisoma namba
 
mithali 31:10-31 mwenye hekima kuliko wote duniani aliwapa somo hapo wakinadada.
mke mwema/wife material kuacha kufuata haya kuacost mahusiano hasa ndoa nyingi. haijalishi una dini, huna, ni sifa mtambuka
 
ubinafsi ni mbaya sana kwenye mahusiano.
mtu anakuwa anajiwazia yeye tu na wazazi/ndugu zake.
upande mwingine wanaendelea kuisoma namba

Je namna gani ya kuing'amua hii tabia kwa wachumba?

Kwa mtu aliyeolewa atahitaji sana msaada wa mwenza wake ili kumbadilisha polepole practically. Yaani ndugu wakija inabidi kumsaidia mke ili awajali wote kwa kiwango sawa. Kikubwa inabidi kuelezana tu kwa uwazi wanandoa kuhusu tabia mnazotakiwa kuzirekebisha.

Binafsi napenda sana kuelezwa udhaifu wangu moja kwa moja siyo kwa kuzungukazunguka lakini pia nami hupenda kumweleza mwenzangu direct kuhusu udhaifu wake.

Ni kweli udhaifu hautaondoka ghafla lakini ni hakika baada ya muda si mrefu unakuta hizo tabia zinazowakera zinaondoka
 
Kutokujali,mfano mwenzio kakwambia anaumwa au kapatwa na matatizo hata pole humpi wala kumfariji hakuna anakueleza nimepatwa na haya unaishia kumjibu okay,hii ipo sana kwa wanaume sasa hapo mwanamke akipata anaemjali wewe utakumbukwa vp ndo inaishia ku break up.
 
1.umalaya uzinzi uasherati wa aiba zote
2. Uchoyo, ubinafsi na umimi aina zote
3. Ubabe
4.dharau
5.majivuno majigambo
6. Kuwa mama's boy
7.ubondia aina zote
8. Uchawi ushirikina na makandokando yake
9. Lugha mbovu chafu isiyo na staha
10. Kutokuthaminiana na kutokujali na kutokusikilizana
11. Kutokujiamini
12. Ulevi wa aina zote


Nyingine kesho...nimechoka
 
Kuchoka pia...kwahiyo ndugu mleta uzi jirekebishe
 
Maisha yamebadilikasana kiukweli tunahitaji kutumia hekima sana unapoamuakuoa lkn sio swala lakukurupuka kuoa unapo fikia wewe mwenyewe maamuzi yakuoa/kuolewa mtangulize mw/mugu kumuomba akupe Mke mwema au mume mwema atakupa na ufanye maombi ya dhati mbeleya Mungu
 
-Ujuaji mwingi na ubabe wa wanawake wakutaka kushindana na Waume zao.

-Ukosefu wa Pesa nyingi kwa wanaume.

-Kuwa na Marafiki wabaya wanaoweza kuwachonganisha.
 

hizi kwa tulio kwenye ndoa tupambane na hizi tabia kuzitafutia ufumbuzi ili kubadilika kama zipo.

Kwa wanaotaka kuwa wife material na husband material wajiepushe nazo, na kama wanazo watafute namna ya kubadilika kabla ya kupata wachumba
 

Wanaume tulioko kwenye ndoa kihatarishi kingine hicho "kutokujali".

Wanaotaka kuwa good husbands jifunzeni hata kwa kujali dada, mama na wanafamilia wengine. jizoeze kuwatembelea wakiwa ktk kuumwa, nyakati za furaha wapongeze n.k
Itarahisisha hiyo tabia kuihamishia kwa mchumba/mke
 

Ulaji m'bovu,wanawake kuomba omba hela!
 
MAWASILIANO ndo sababu kuu ya kuwa na uhusiano imara au mbovu na kupelekea kuvunjika kwa huo uhusiana au kuimarika.
Mawasiliano ni mada ndefu na ina husisha vitu vingi, sio kupigiana simu na sms, kuongea tu, hapana! Hivi viwepo ila ni zaidi ya hivi!

Ni suala la kujiexpress yourself na kuwa huru kwa mwenzako na kupelekea kuonyesha rangi zako halisi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…