Tabia za wanaume zisizowapendeza wanawake! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tabia za wanaume zisizowapendeza wanawake!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Mar 21, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Mar 21, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Ngoja nizidadavue hapa chini kama ifuatavyo...............

  1. Aina ya kwanza ni ile ya mwanaume ambaye anatatabirika. Wanawake hawapendi wanaume wanaotabirika kwa sababu wanaelewa ni jinsi gani watalipokea jambo lolote linalotokea. Mwanamke anaweza kujua kabisa kwamba, leo atatolewa outing au hapana, ataletewa zawadi au la. Yaani hakuna kitu tunachokiita surprise. Wanawake wanataka kiasi fulani cha kutotabirika toka kwa wanaume. Ndio maana utakuta anaishi au kuolewa na mwanaume jeuri au mwenye roho mbaya . siyo kwamba anampenda kwa jeuri yake, bali kwa kutotabirika kwake.

  2.
  Aina ya pili ni ile ya mwanaume anayejisikia (mwenye maringo). Huyu kwa kawaida ni mbinafsi sana. Ni jeuri siyo kwa mpenzi wake tu, bali hata kwa mtu yeyote ambaye anamuona yuko chini yake. Kuwaringia watu wengine ni sawa na kumringia mpenzi wako moja kwa moja.

  3. Aina ya tatu ni ile ya wanaume jeuri. Mtu jeuri hana aibu! Wakati mwingine anaonesha waziwazi kwamba anamtamani mwanamke mwingine mbele ya mpenzi wake! Anafikia hatua ya kumsimulia mpenzi wake kuhusu marafiki zake wa kike wa zamani na hata u.p.u.u.z.i waliokuwa wakifanya! Kwa ujumla anawadharau wanawake.

  4. Aina ya nne ni ile ya mwanaume bahili. Hamnunulii mpenzi wake zawadi hata siku moja! Kila wakati watokapo outing yeye na mpenzi wake huagiza vyakula vya bei rahisi sana pamoja na kwamba, anazo hela. Anataka kumfanya huyo mpenzi wake atishike naye aagize vya bei rahisi. Na wakati wa kulipa anahesabia fedha mfukoni, anatoa fedha utadhani bajeti inabana sana au utadhani yeye na mpenzi wake wamekubaliana "kukaza mikanda." Mwanaume anaonesha ana mkono wa birika namna hiyo katika siku za kwanza tu za mapenzi! Je huko baadaye itakuwaje? Si atahesabu hata vipande vya nyama jikoni!

  5. Aina ya tano ni ile ya mwanaume mbishi. Hata majadiliano ya kawaida tu, yeye anataka kubishana! Anapomtoa outing mwanamke, anakuwa kama amempeleka kwenye mashindano ya mdahalo! Mwanamke hajisikii kuwa huru kutoa maoni au kusema hisia zake, maana atabishiwa.

  6.
  Aina ya sita ni ya mwanaume asiyekosea. Huyu bwana anapenda sana kuhumu wenzie. Inawezekana hanywi wala havuti sigara, anataka hata wenzie wamuige yeye, wasinywe wala wasivute sigara. Toka siku ya kwanza anayotoka na mwanamke anaanza kumhubiria anayoyataka yeye, siyo asiyoyataka mwanamke. Huyu hataki kabisa mwanamke akawa huru kama yeye, bali angependa yeye amuamulie awe nani na afanye kipi au asifanye kitu gani, ebo! Sasa hapo ni mtu na mpenzi wake au mtu na mtumwa wake!

  7. Aina ya saba ni ile ya mwanaume kuwachukia wanawake. Hafichi chuki yake kwa wanawake. Huyu huonesha dhihaka nyingi kwa mpenzi wake na kuwaponda wanawake kwa ujumla wao. Mazungumzo yake yote yatakuwa ni kuwadharau, kuwadhalilisha na kuwanyanyapaa wanawake. Hivi ni mwanamke wa namna gani ambaye atamkubalia mwanaume mpondaji namna hii? Labda mwanamke mwenye mkabala wa kufujwa peke yake au yule mwenye kutaka tu kuchuna buzi na kusepa zake.

  Nitaendelea kuwamwagia Tabia za wanaume zisizowapendeza wanawake siku zijazo....
   
 2. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #2
  Mar 21, 2012
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hiyo ya pili ndo style yangu, mbona naona ndo wanazidi kunipenda :cool2:
   
 3. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #3
  Mar 21, 2012
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Mkuu ahsante kwa ni pweint,ngoja niongezee.
  player: mwanamke hapendi lianaume shingo feni.
  Pafomensi: mwanamke hapendi michezo ya kitoto,anapenda shughuli
  Mpira:kila weekend unaangalia manchesta,tena bar,kwako kuna miiba?
  Wazazi: dume linajali ndugu zake tu,ndo nini?
  ............tuendelee wakuu....
   
 4. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #4
  Mar 21, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  duh . . . .
   
 5. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #5
  Mar 21, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Najua nimekubamba.................Tena kwa asilimia 75 unazo tabia hizo...............LOL
   
 6. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #6
  Mar 21, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  h, yani nadhani ntascore 5 au sita hivi, kumbe ndio maana sipendwiiiiii:A S 13:
   
 7. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #7
  Mar 21, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  hizi point zinaka ukweli ndani aisee...
   
 8. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #8
  Mar 21, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,034
  Likes Received: 23,814
  Trophy Points: 280
  Wanaume wenye vibamia: Wanawake wengi hawapendi wanaume wenye vibamia
  Wanaume wenye mitarimbo: Wanawake wengi wanaogopa mitarimbo mikubwa
  Wanaume wenye wowowo: Wowowo ni sunnah kwa wanawake
  Wanaume wenye sauti nyembaba: Khaa!
  Wanaume wasio na ndevu: heheheh dah!
  Wanaume wafupi: Duh!
  Wanaume wenye matege: Aisee:cool2:
  Wanaume wanaokoroma usiku: Phewww
  Wanaume wambea: Ni nomer

  Source: Mke wa ODM a.k.a bibi yenu.
   
 9. Yegomasika

  Yegomasika JF-Expert Member

  #9
  Mar 21, 2012
  Joined: Mar 21, 2009
  Messages: 7,125
  Likes Received: 23,734
  Trophy Points: 280
  Mtambuzi wewe hapo upo kundi lipi?.
   
 10. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #10
  Mar 21, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,035
  Trophy Points: 280

  babu....naomba ridhaa yako niongezee tafadhali.......
   
 11. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #11
  Mar 21, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,035
  Trophy Points: 280
  yupo namba 4......

   
 12. Yegomasika

  Yegomasika JF-Expert Member

  #12
  Mar 21, 2012
  Joined: Mar 21, 2009
  Messages: 7,125
  Likes Received: 23,734
  Trophy Points: 280
  Duu huyo kaa nae mbali..hafai kabisa. kama mpaka senene anafukunyulia mfukoni basi muogope!.
   
 13. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #13
  Mar 21, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,034
  Likes Received: 23,814
  Trophy Points: 280
  Ruksa.... ila ngoja nikuwahi.

  Wanaume wenye vitambi, isipokuwa ODM: Wanawake wengi wanapenda athletic figures (six pax lol)

  Source: Preta, JF Arachuga.
   
 14. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #14
  Mar 21, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,224
  Trophy Points: 280
  mwanaume wa aina hii hana madhara makubwa, na rahisi kumhandle loh!!!  mwanaume wa aina hii hafai yupo radhi nyumbani mke na watoto wale ugali kwa chumvi, yeye mradi kashiba waaalaaa.... na usiombe mke upate shida uhitaji assistance yake...utajutaaaa
  na usiombe awe jeuri na mkono mwepesi wa kupiga.....wallah ndoa utaiona chungu....mbaya zaidi wanaume wa aina hii hawashauriki hawa...


  ukishamjua mwanaume wa aina hii wala hakusumbui mkitoka out unaagiza vyakula vya bei, mwache yeye ale vyakula vyake vya bei rahisi...(tahadhari uwe na extra cash mfukoni hawachelewi kukuadhiri hawa..) na uwe mchakarikaji usitegemee kupata tatizo akakusaidia, ingawa yeye akihitaji pesa toka kwako atakughasi mpaka umpe....
  hahahaaaa kweli wanawake wana kazi....

  Mr perfect........
  wana kuwa na kipaji cha ziada, wanajua kucriticise hadi ujione huna maana


  Mtambuzi, inawezekana wanaume wa aina hii childhood yao ilikuwa na matatizo fulani, au malezi yao kuna vitu fulani wamekosa/wamepotoshwa au wamekuwa na baba mwenye tabia hizo...  asante kwa darasa...
  si tu nilikuwa najifunza lakini nimeenjoy sana maana...............(nitakwambia siku nyingine)
  ila umesahau wanawake hawapendi wanaume mala*a..... yaani unakuta hata housegirl huweki, wala ndugu wa kike hawaji....kisa unahofia mumeo asipojaribu kuwabaka atawatongoza...

  na wanawake hawapendi wanaume wenye ghubu....Mtambuzi ushawahi kukutana nao? yaani hawana dogo dogo kwao kubwa kubwa kwo kubwa, hawa hata kosa la miaka kumi iliyopita watalikumbushia....
   
 15. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #15
  Mar 21, 2012
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Umesahahu, wanaume wanaogeuka kuangalia angalia wanawake njiani hata kama yupo na mpenzi wake.
   
 16. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #16
  Mar 21, 2012
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mimi sikubaliani na point yako kabisa, vipi mwanaume mwenye maringo asimsaidie mke wake?

  Hebu nipe point wapi uliona mwanaume mwenye maringo mke wake akafa njaa.

  Vipi mtu awe ana maringo wakati kwake watu wanakufa njaa, labda wanaume wa bongo hao :cool2:
   
 17. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #17
  Mar 21, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Hii mimi imenibamba aisee..............
  4. Aina ya nne ni ile ya mwanaume bahili. Hamnunulii mpenzi wake zawadi hata siku moja! Kila wakati watokapo outing yeye na mpenzi wake huagiza vyakula vya bei rahisi sana pamoja na kwamba, anazo hela. Anataka kumfanya huyo mpenzi wake atishike naye aagize vya bei rahisi. Na wakati wa kulipa anahesabia fedha mfukoni, anatoa fedha utadhani bajeti inabana sana au utadhani yeye na mpenzi wake wamekubaliana "kukaza mikanda." Mwanaume anaonesha ana mkono wa birika namna hiyo katika siku za kwanza tu za mapenzi! Je huko baadaye itakuwaje? Si atahesabu hata vipande vya nyama jikoni!

   
 18. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #18
  Mar 21, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,035
  Trophy Points: 280
  hapo kwenye bluu naomba nigandamizie wino......kabla sijaendelea kwa ridhaa yako.....
   
 19. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #19
  Mar 21, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,035
  Trophy Points: 280
  hapo sasa.....badilika Mtambuzi........

   
 20. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #20
  Mar 21, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Aina zote zinavumilika ila no 2,3,4,5, na 6 aisee pasua kichwa sn!
   
Loading...