Tabia za mashabiki wa Simba na Yanga ndo tabia za mashabiki wa CCM na Chadema

Kamgomoli

JF-Expert Member
May 3, 2018
1,865
3,802
Ni wiki la kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa. Zoezi limedoda watu ni km wamesusia,mwitikio ni mdogo sn hali inayopelekea viongozi kuanza kutafta wa kumuangushia zigo. Nashangaa kwann viongozi wetu wamechanganyikiwa kwa hiki kinachoendelea wkt ni wao wenyewe ndo wametengeneza haya mazingira. Kuna siku namba moja aliwahi tamka hadharani kuwa Watanzania si wajinga.Ni kweli si wajinga wanaelewa nn maana ya uchaguzi. Duniani kote uchaguzi ni ushindani baina ya pande mbili. Ni km ilivyo kwa Simba na Yanga. Simba wakifanya vibaya mashabiki hawaendi viwanjani vilevile kwa Yanga. Ili kuweza kuwavutia mashabiki wa timu zote mbili kwenda viwanjani ni lazma timu zote ziwe bora, na marefa wawe fare.( Watende haki) kinyume chake tegemea mgomo wa mashabiki. Ndo kinachotokea ktk swala la kujiandikisha.Bila fareness kwa vyama vyote migomo km hii itaendelea na hiki tunachokishudia leo ni cha mtoto hali inaweza kuwa mbaya zaidi kwa chaguzi zijazo na hivyo kupoteza kabsa maana ya uchaguzi. Mengi ya yale mnayofanya mkizani WTZ ni wajinga au hawayaoni haya ndio majibu yake. Wtz wenzangu twendeni tukajiandikishe ivo ivo tu km mashabiki wa Yanga ya Zahera.
 
hapa losers ni wapinzani kwa sababu watu wao wengi ndio hawaendi kujiandikisha wakiamini kwamba hata wakijiandikishaje mshindi ashapangwa tayari
 
Sasa unaenda kujiandikisha nini, wakati chama tawala kishajitabiria ushindi iwe isiwe...

Waacheni washindane wenyewe...


Cc: mahondaw
 
Back
Top Bottom