Tabia za kiboya za wasanii wa Bongo

Tabia za kiboya za wasanii wa Bongo

GRAMAA

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2014
Posts
1,322
Reaction score
4,211
Bongo hapa tunawasanii wengi sana wanaofanya vizuri nje na ndani ya Bongo. Pamoja na mazuri yao wasanii hao wengi wao huwa na Gambia za ajabu ajabu sana.

Mfano kila msanii na yake.

1. NIKKI WAPILI
Huyu hujionaga yeye ndiye msanii msomi pekee dunia nzima hakuna. Kwenye kila media akienda kufanya interview basi interview nzima itatawala kuelezea usomi wake tu na kujidai kwingi. Ila cha kushangaza nyimbo zake ni za kawaida sana hazina usomi wowote.

2. NAY WA MITEGO
Huyu ni mzee wa akili kisoda nguvu kontena. Yeye huamini katika miguvu na majigambo meeengi. Yeye huamini ili uwe msanii bora ni lazima uwe mbabe na utukane wangine. Hata nyimbo zake nyingi huwa anaimba kwa hisira na jazba utazani anabifu na mike. Huyu anaponzwa na usela mwingi sana.

3. DIAMOND PLATINUMZ
Huyu ni mzee wa kuongeza sifuri sifuri mbele.
Akinunua gari la milioni sitini akawii kukuambia amenunua milioni mia sita. Huyu pia anauwezo mkubwa sana wa kujipendekeza kwa wasanii wakubwa wa nje na pia hucheza sana na udhaifu wa mabinti ili abaki kwenye chati. Asilimia kubwa ya umaarufu wake umetengenezwa na wanawake aliwahi kuwa nao kwenye mahusiano. Bila ya kina Wema Sepetu, Zali the boss, Mabetto na wengine Diamond angekuwa kama Meja Kunta tu.

4. ALLY KIBA
Huyu ni mzee wa kutilia huruma ili aweze kumaintain status. Huyu huigiza kuwa yeye ni mpole na ni msanii mstaarabu kuliko wasanii wore duniani kumbe hakuna lolote ni sound tu. Ali Kiba hutumia sana mbinu ya kutilia huruma ili aonekane kama mtu anayeonewa ili amantain mbinu hii imemsaidia sana kumantain jina lake hasa pale anaposhindanishwa na Diamond Alikiba huamua kuigiza hustaarabu.

5. Q CHIEF
Huyu ni mzee wa lawama. Huyu jamaa kama umefuatilia interview zake yeye kutwa nzima huona anaonewa tu na media. Hukawii kumsikia akisema media hazimpendi ndiyo maana hazipigi nyimbo zake. Hutumia saa nzima kulaumu tu. Huyu jamaa gemu analazimisha tu kwani ameshindwa kwenda na wakati kabisa mwisho wa siku anamtafuta mchawi wa muziki wake.

Wapo wengi sana wengine ongeza na wewe. Mimi naishia hapa kwa leo.
 
Fanya Maisha, hao uliowataja wote hapo wanatengeneza Pesa. There is no right way of doing things in war and making money, we kalia hapohapo.

Kwanza ukajifunze kuandika vizuri. mpore - Mpole, hustaarabu - Ustaarabu.
 
Fanya Maisha dogo.. acha ushoga, hao uliowataja wote hapo wanatengeneza Pesa.. there is no right way of doing things in war and making money, we kalia hapohapo
Kwanza ukajifunze kuandika vizuri.. mpore - Mpole, hustaarabu - Ustaarabu.
Nyinyi ndiyo mnaitwa wajanja wa kibongo.
Ngoja nikupe like kwa koment nzuri kiongozi.
 
Watu masikini hujipoza stress za maisha kwa kuongelea madhaifu ya watu utadhani wao ni parfect.

Najua umefarijika bt nakushauri ushughulike zaidi na maisha yako angalau usiukose mkate wakila siku.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom