Tabia ya wanawake kuringa na kujisikia

Tabia ya wanawake kuringa na kujisikia

kuku_msela

Member
Joined
Jun 12, 2017
Posts
10
Reaction score
24
Hi tabia inakera sana, wanawake jaribuni kubadilika, mtu hata hakutaki wala hana wazo la kukutongoza lakini akikusemesha kidogo tu, utadhani amekutongoza miaka mitatu mfululizo, majuzi nimepoteza direction mahala flani, nikamuona dada mmoja nikamfuata kistarabu, nikamsalimu na kumuuliza, bora hata mtu akujibu sipafahamu, niliambua kubinuliwa midomo utadhani tupo hospitali za kung'oa meno.

Bora basi uwe unaringa sura unayo, unakuta wengine sura ngumu kama nyama ya mamba lakini hata ukikasalimu tu kosa, kajitu anauchuna kakijitahidi sana utajibiwa kwa mkato utadhani kuna ugomvi wa kudhurumiana pesa.

Mbadilike japo sio wote ila asilimia kubwa mmezidi, ata sms utakuta kamtu kana jibu k., au p,,, hivi mnavojikuta wazuri utadhani hamuendi chooni kukata magogo, afu kajitu kanakuringia wewe mwanaume ambae bila wewe kusema yes katasota miaka 30 hakajaolewa tu,
Dada zangu naamini jumbe umefika na mtaufanyia kazi.
 
Pole saana kwa masahibu yaliokukuta.

Watu wana stress sàna, wengine wamekopwa penzi, wengine wametumbuliwa na jpm, matatizo kibao.

Sometimes unasamehe bure
Mkuu umeongea point kweli umenifumbua fikra kumbe sio makosa yao lakini mbona wanaume sisi hatupo hivyo au sisi hatuna stress na hatutumbuliwi?
 
Mzee Baba pambana na hali yako.. Huenda ikawa ndo kikwazo cha kutoitikiwa hzo salamu
Kweli mkuu upo sahihi lakini hii wao imekua too much kiongozi kwani salama zinawamaliza damu au zinawapa ujauzito?
 
Pole kwa mkasa.

Kama unashida na kitu, unakuwa mpole tu hata angeleta maringo gani we unajifanya mjinga tu kwa mda. Hii itakusaidi sana kupata nini unachotaka.
 
Yote haya wa kulaumuwa ni sisi wanaume ambao tumekuwa tukiwadanganya waschana et ww mzuri huwez amn kuazia sku hiyoo anapata confidence asee wana akili ndogo kama piriton ila kwa huku vyuon dawa nu dem afke mwaka wa mwisho asee hata ukikohoa anaitikiaa yaan msichana tamba sana mda wako n miaka 27 unaitwaa bibi tayari
 
Mkuu umeongea point kweli umenifumbua fikra kumbe sio makosa yao lakini mbona wanaume sisi hatupo hivyo au sisi hatuna stress na hatutumbuliwi?
Hujakutana na watu waliona maswahibu.
 
Ilikua ghafla dada yangu, lakini ukiishi kwa itifaki hizo, utakua sio rafiki wa muda na utakosa vitu vingi

Jitahidi uwe unafuata wakaka wenzako ukiwa na shida kuepuka kubenjuriwa midomo na wadada
 
Pole sana mleta mada.

Kuna kipindi nilipatwa na mkasa wa staili hiyo ya umepotea unataka kuuliza njia.

Mbaya zaidi nilikuwa nadrive , kwa hiyo yule dada nilimuita zaidi ya mara 3 na eneo lenyewe halina watu wengi hivyo mtu akikupita hadi ukutane na mwingine ni ishu..

Mimi nikaamia kumpa kavu kuwa "Dada sikutongozi , naulizia njia tuu"

Kwa aibu akarudi kunielekeza
 
Mi Niliingia Exim Bank Nyerere Road Branch Nilipeleka Makabrasha Flani Kwa Meneja, Meneja Akaniongoza Kwa Mdada Mfanyakazi Wa Humo Eti Yule Dada Ananiambia Fungua Hiyo Barua Soma Inahusu Nini? Khaaa Nikamwambia Chukua Usome We Si Ndio Kazi Yako? Tulibishana Kwa Ujinga Nikamwambia Mi Nimeishia Darasa La Saba Sijui Kiinglishi Ila Huyo Bosi Wako Ananiheshimu Nikawa Naondoka Nikamwambia Dada Utafukuzwa Kazi Ukapike Matembele Kwenu Kwa Ujinga Wako! Samahani Nyiiiingi, Siku Hiyo Wamekuja Ofisini Kwetu Akaelekezwa Kwangu Kuniona Tu............Hahahahaaaa Alikuwa Mpole Kama Ana Vyeti Feki Vile . Wadada Acheni Dharau Mnachelewa Kuolewa Kwa Ujuaji Wenu
 
hahaha kuku msela kwenye real life cjawahi kukutana na maswaibu yako, ila kwenye sms chatting ndo wadada huwa wananiboaga sana..utakuta demu kaanza kuku-text yeye mwenyewe hlf anategemea wewe mwanaume ndo uendeleze story, kidemu kinaanza na text kama vile, "niambie" "mambo" "hi" halafu cha kuongea hana....uzuri mimi huwa siwafichi nawachana ukweli kuwa text zao zinaboa, wananinunia wee ila dawa ndo imewapata, mwingine anajibu sms yako ndefu kama hivi "mhmhmhmh" au "oh" au "k"

Sasa mademu wakitext hivo sielew ni uvivu wa ku-text, kajifosi kuku-text, kujifanya wako bize sana, mashauzi, kuringa, kujiona keki sabab ya kutongozwa sana, au cjui ndo trend ya sasa kuku_msela rubii
 
Mi Niliingia Exim Bank Nyerere Road Branch Nilipeleka Makabrasha Flani Kwa Meneja, Meneja Akaniongoza Kwa Mdada Mfanyakazi Wa Humo Eti Yule Dada Ananiambia Fungua Hiyo Barua Soma Inahusu Nini? Khaaa Nikamwambia Chukua Usome We Si Ndio Kazi Yako? Tulibishana Kwa Ujinga Nikamwambia Mi Nimeishia Darasa La Saba Sijui Kiinglishi Ila Huyo Bosi Wako Ananiheshimu Nikawa Naondoka Nikamwambia Dada Utafukuzwa Kazi Ukapike Matembele Kwenu Kwa Ujinga Wako! Samahani Nyiiiingi, Siku Hiyo Wamekuja Ofisini Kwetu Akaelekezwa Kwangu Kuniona Tu............Hahahahaaaa Alikuwa Mpole Kama Ana Vyeti Feki Vile . Wadada Acheni Dharau Mnachelewa Kuolewa Kwa Ujuaji Wenu

Ni kweli umeishia la saba, au ulijifanya umeishia la saba? hlf baadae huyo dada aligundua kuwa wewe una cheo gani? varavara
 
duh..binafsi sijawah kupatwa na swaibu kama Hilo,yan kumuuliza mtu njia tu ndo akubinjulie domo kweli?
 
Tatizo huwa mnazani wadada hatuna mawazo,unaongea na MTU anakuangalia ila mawazo yake yapo kibiti,alafu ilo shwala la kusema wadada wakiitwa tu wanahisi kutongozwa sio kwamba tunahisi ila ndo ukweli ukiitwa na wanaume kumi ujue Tisa watakutongoza au wote kabisa.
 
Akili zenu ndo zinavyowaambia hvyo....punguzeni akili za vyege
 
Inategemea na muonekano wako kwa wakati huo,
Mbona sisi wengine hatujawahi kufanyiwa hayo madharau?
 
Back
Top Bottom