Tabia ya mama mkwe mtarajiwa inaniogopesha kutangaza nia kwa mwanae

sangwine

Senior Member
Jun 16, 2013
144
45
Nimekuwa katika hali ya kumfanyia uchunguzi binti mmoja ambaye kwa mwonekano wa nje kanivutia sana.

Kwa ufupi binti kakamilika katika kila idara, pili ni mtoto ambaye anapenda sana kuji keep buzy .

Lakini jambo linaloniogopesha niisomapo tabia ya mama mzazi.

Kwa yeye alimzaa binti huyo akiwa bado mdogo sana akiwa na umri wa miaka 16.

Na pia ana watoto wa wili ambao kila mmoja anababa ake, na tatu ni mlevi sana, ni pia anatabia ya kupiga mizinga kila mkutanapo.

Kitu ambacho kina nitisha ni hizo tabia kwan nimefundishwa kwamba katika kutafuta mpenzi wa malengo ni muhimu kuangalia tabia hata ya familia ya binti.. je katika hili ntafanyaje..?
 
Akili kichwani...ukishaweka ndani, basi Maboga yote yataota kwako,coz ua si lipo ndani bhana.
 
hujapenda wewe jichunguze tena inawezekana umemtan tu

when u love someone huoni chochote zaid ya yeye..we mpk unamchunguZa mkweo!!

km unawasi muache dada wa watu huyo ni mamake na hakuna kitakachobadili uhalisia.
 
Nakushauri umchunguze huyo binti kwa umakini kuhusu tabia zake,and please take ur time usiharakishee....Kama tabia za binti zinakuridhisha kisha mamaake asiwe kikwazo cha wewe kushindwa kumuoa bintiake...Kama huyo mama ndo yupo careless hivo lazima kuna kitu ambacho kinaweza kukutatiza kuhusu malezi ya huyo binti au maisha aloyapitia...chunguza plzzz
 
Usikariri kbs la muhimu mchunguze huyo uliye nae tabia huwa hazijifichi kbs, ndani ya muda mfupi tu unaweza kumtambua mtu sio mara zote" like mother like daughter" huwa inafanya kazi. Chunguza sn wengine ni wasichana waliozaliwa kwenye familia yenye adabu na heshima tena malezi ya maana mtt kalelewa lkn mwsho wa siku anakua tofauti na familia anayotoka, km ni wa kike anaweza kuwa na tabia ambazo hata mama yake hana and vice versa is true.

Kwahiyo msome mtu tabia aliyo nayo km yeye na usimsome mtu tabia aliyonayo kupitia mwingine hii sio sahihi.
 
kweli,mkifatilia tabia za wazazi wetu hamtatuoa.

Haahaa! Maisha yataendelea tu, si mnavumiliana tu, kwani unadhani wote huthubutu kuonesha tabia zao? Ni bora hata huyo mama mkwe unajua kuwa ni m2 wa wa gambe na mizingo so jaribu kupanga stratergy za kwenda nae sawa tu, kama we mjanja atatulia tu then mtaenda sawa.! Usikaache hako katoto mbona kametulia kulingana na maelezo yako.!
Au unataka watu waongeze mke mwingine (mitala) shauri yako utajuta.!
 
kwa mtazamo wangu naona huyo bint anaweza akawa ana tabia nzuri kwani kungekuwa na kasoro ungeshaanza kuziona, ila tu kinachoweza kuja kuwa shida kwenye maisha yenu ya ndoa ni huyo mama mkwe kwani kwa hzo tabia ulizozielezea anaweza kuja kuwa zigo la usumbufu sana kwenye maisha yenu kiasi unaweza kujuta kwanini ulioa binti yake.
 
Nimekuwa katika hali ya kumfanyia uchunguzi binti mmoja ambaye kwa mwonekano wa nje kanivutia sana.

Kwa ufupi binti kakamilika katika kila idara, pili ni mtoto ambaye anapenda sana kuji keep buzy .

Lakini jambo linaloniogopesha niisomapo tabia ya mama mzazi.

Kwa yeye alimzaa binti huyo akiwa bado mdogo sana akiwa na umri wa miaka 16.

Na pia ana watoto wa wili ambao kila mmoja anababa ake, na tatu ni mlevi sana, ni pia anatabia ya kupiga mizinga kila mkutanapo.

Kitu ambacho kina nitisha ni hizo tabia kwan nimefundishwa kwamba katika kutafuta mpenzi wa malengo ni muhimu kuangalia tabia hata ya familia ya binti.. je katika hili ntafanyaje..?

mtoto akizaliwa na chizi sio kwamba nae atakuwa chiz kwa hiyo nae akichunguza akajua baba yako kazaa watoto nje akutilie shaka wewe
 
Nakushauri umchunguze huyo binti kwa umakini kuhusu tabia zake,and please take ur time usiharakishee....Kama tabia za binti zinakuridhisha kisha mamaake asiwe kikwazo cha wewe kushindwa kumuoa bintiake...Kama huyo mama ndo yupo careless hivo lazima kuna kitu ambacho kinaweza kukutatiza kuhusu malezi ya huyo binti au maisha aloyapitia...chunguza plzzz

Are you really gorgeous?
 
Mchunguze huyo binti kama ukiridhishwa na tabia zake basi atakufaa lkn pia ni vizuri kujua yeye anazionaje tabia za mamake je hapendezwi nazo , kwa sababu kuna watoto wengine hukerwa na tabia za wazazi wao lkn hawana cha kufanya. Ule utaratibu wa kuangalia tabia za wazazi si kila wakati uko sahihi waweza kuta wazazi wana tabia njema lkn binti akawa si mwema and vice versa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom