Tabia ya kuweka vitoto vidogo kuuza duka

Tabia ya kuweka vitoto vidogo kuuza duka

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Posts
40,799
Reaction score
46,917
Kuna katabia nimeka notice hasa huku sinza kwa mwaibula na maeneo ya jirani.., wenye maduka hutafuta vitoto vidogo vya miaka 12 hadi 14 ili vifanye kazi ya kuuza duka. obviously vitoto hivi vinadhulumiwa haki yao ya msingi ya kufurahia utoto na kupata elimu kwani huu muda ukipita haurudi tena. vile vile wanafanya kazi bila ujira wowote au ujira kidogo sana.Kuna wakati nilienda dukani saa saba usiku nikakakuta katoto kamoja kako dukani bado kanauza.., kalikuwa kanasinzia ila kalikuwa kanajikaza tuu.., nilimwonea huruma sana..,nilipomuuliza kwa nini hujafunga duka akaniambia hua hafungi duka.., yaan hakuna usingizi wa kueleweka.., ni kusinzia tu pale panapokua hakuna wateja. Serikali mpo..?!
 
Au jirani yako dukani amuache mtoto wake wa miaka 9 na wewe Unataka condo
 
Au jirani yako dukani amuache mtoto wake wa miaka 9 na wewe Unataka condo

Mkuu.., hawa watoto huchukuliwa toka vijijini kwa ahadi za uongo.., hakuna mtu anaeweza kumtesa mtoto wake mwenyewe kwa kiasi hiki..
 
Tanzania tuna sheria ambazo ni Employment and Labor Relations Act No. 6 2004 and Child Act of 2009 lakini bado zimeacha upenyo mkubwa kwa watu kama wenye maduka kuajiri watoto kwa sababu imekataza kuajiri watoto wa miaka chini ya 14 katika kazi hatarishi lakini zimeruhusu kuajiri katika kazi zinazoitwa kisheria (light work) wakati ambao hawatakiwi kuwepo shuleni, hata hivyo sheria imeshindwa kuzisema 'light work' ndiyo kazi zipi nchini.

Serikali imeshindwa kuchambua light work in zipi kulingana na mazingira kwa sababu hata huku kwetu Bariadi kijijini ambako kuchunga mifugo mara nyingi inafanywa na watoto wenye umri wa kuanzia miaka mitano sijui kisheria utaita ni light work au hard work kwa sababu ni kazi inayoonekana niya kawaida kabisa na inafanywa karibia na kila mtoto kwa furaha.
 
Badala ya kuboresha hizi sheria watu wanakazania serikali 3.., hovyo kabisa..
 
Lakini kuna baadhi ya watoto hiyo kazi ya kuuza duka ni kama tunu. Unakuta kamaliza std 7, nyumbani ni umaskini wa kutupwa hata mlo mmoja kwa siku ni taabu. Suala ni kuzingatia masaa ya kazi na viwango vya mishahara (hii ni kazi ya labor dept)
 
Badala ya kuboresha hizi sheria watu wanakazania serikali 3.., hovyo kabisa..
Nipishane na wewe kidogo kama maana ya hoja yako ni kukazania Katiba Mpya lakini vile vile nitakubaliana na wewe kama hoja yako una maana ya wabunge kurumbana na kukazania Sura ya Kwanza na Sita ya Rasimu ya Katiba.

Tunahitaji sana Katiba Mpya au mabadiliko ya Katiba ili pia iwe ni mwongozo rahisi kwa sheria kama hizi za kuwalinda watoto kutungwa bila kupingana na Katiba.
 
Tuko pamoja.., afu unaonekana makini sana.., we lawyer nini..
 
Tabia hii ni dar nzima,mtt kaz yake ni kula na kusoma ni watt wao siku hiz wafanyakaz waaminifu nishida kupatikana
 
Kuna kamoja kajirani niliendaga kununu salama nikaenda kwa mchepuko, kurudi home hali ya hewa imeshachafuka kumbe kalienda kusema.
 
Bora huko mujini...Nendeni vijjijini kama Sinya au Mundarara huko Longido muone watoto wanavyochunga mbusi....Lol
 
Hii sheria iende kilimanjaro isee vibwasheee kibao ndio utavikuta vinauza maduka hapa mjini
 
Hao watoto mnadhani wananyaswa wengi wao wakifisha miaka 18 nao wanamiliki maduka yao labda kama hajatoka kilimanjaro akifisha miaka 30 anakuajiri wewe uliyekua unakalia dawati kwa mshahara anaotaka yeye.
 
Ni umasikini ndio unafanya watu kuajiri watoto wadogo kama hawa coz ujira wake unakua mdogo then hana malipo ya mwisho wa mwezi yy anahitaji kula tu na hapa mjini hana family ndio ukaona wanakesha hadi saa 7usiku
 
Back
Top Bottom