Tabia ya kuomba miongozo ovyo bungeni yawatokea puani CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tabia ya kuomba miongozo ovyo bungeni yawatokea puani CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nikupateje, Jun 29, 2012.

 1. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #1
  Jun 29, 2012
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Pamoja na kwamba nimeitaja CCM lakini sina ushabiki na chama chochote. Ninachokieleza ni ukweli ambao baada ya kunisoma hadi mwisho mtakubaliana nami na mtanielewa.

  Bunge hili la Anne Makinda lilianza baada ya uchaguzi wa 2010 na kwa mara ya kwanza upinzani mkali umetokea bunge hili.

  Nusu ya kwanza ya mwaka 2011 hoja kali toka upinzani zilikuwa zikitolewa. Njia kuu waliyotumia CCM ni kuomba muongozo kila unapopatikana kama njia ya kuzima hoja za wabunge wa CHADEMA.

  Kweli njia hii ya kuomba mwongozo ilifaulu sana na CHADEMA mwanzoni walijikuta wanatumbukia mtegoni. Mtu alikuwa anasimamishwa hoja yake kwa kuombwa mwongozo kwa neno ambalo mtaani ni la kawaida kabisa.

  Narudia, CCM waliwanasa sana CHADEMA na mbinu hii ya mwongozo, maana ukibanwa hata kwa kineno kidogo basi tayari mfululizo wa hoja yako unapinda, confidence inakuondoka na hata unayomalizia wananchi tayari wanapata picha ya mashaka kuhusu ukweli wa unachoongea.

  Walichoshindwa kutambua CCM na Spika ni kwamba hata CHADEMA nao wanajua kuomba mwongozo ovyoovyo. Spika mwenyewe alikuja kugundu ahili siku ile alipotamka kwamba bunge limekuwa kama Soko la Kariakoo. Alisema alikerwa alipokuwa na udhuru hakuwa bungeni lakini akaangalia bunge kupitia TV yake.

  Mnakumbuka alisema aliudhika hadi akazima TV. Kwa nini alizima TV? NI kwa sababu aliona kila mmoja anainuka kama vile yamekuwa mashindano ya kuomba mwongozo.

  Ni kweli kabisa alistahili audhike. Lakini alisahau kwamba kuruhusu miongozo kwa vitu ambavyo si vya msingi sana ndiko kulileteleza yote yale. Kwani kama ni mbinu ya kuzima hoja kwa kuomba ovyo miongozo kila mmoja anaweza.

  Kwa kiasi kukatulia lakini tabia ikawa imemea mizizi kwa wote. Kumbuka mwongozo uliosababisha Lemma, Tundu Lissu na Msigwa kutolew nje mwaka jana.

  Sasa, kikai cha jana May 28, 2012, baadhi ya wabunge wa CCM na CUF wameanza kejeli kwamba hawakutumwa na wananchi kuja kuomba miongozo bungeni. Mmoja kasema mwisho bunge hili la Anne Makinda litaitwa Bunge la MIONGOZO.

  Anne Makinda alifurahishwa sana na hoja hizi na akapandilia kwa kusema hata hivyo waombaji wakuu wa miongozo wanajulikana.

  Ni kweli kwamba miongozo imekuwa mingi. Lakini yote haya yametokana na nini?

  Kwanza kabisa muongozo ni sehemu ya Kanuni za Bunge ambazo za sasa zimepitishwa mwaka 2007 huku CHADEMA ikiwa haina wabunge zaidi ya 11. Majority wamekuwa ni CCM miaka yote. Hivyo ni kanuni zilizopitishwa na CCM.

  lakini hilo si tatizo sana. Tatzi ni hili nililoeleza humu kwamba wao wenyewe CCM ndiyo walianza sana kasi ya kutumia miongozo ku-harras hoja za wabunge wa CHADEMA.

  Sasa, CHADEMA wamejibu mapigo tunaanza kulalamika na kuita majina kwamba bunge limekuwa la miongozo. Enzi za Samwel Sitta hakukuwa na miongozo mingi kiasi kile. Matokeo ya kulichukulia mzaha jambo hili mapema ndiyo haya tunayoyaona sasa.

  Hivyo, hakuna sababu ya kukejeliana kwamba bunge limekuwa la miongozo na waomba miongozo wanajulikana. Taabu ni kwamba hansard zinaonyesha wazi kuwa walionza tabia ya kuomba miongozo ni kina nani.

  Wakati naandika haya, nimepitia paper chache za hansard ili nitume harakaharaka. Lakini kama wingi wa watu hasa bungeni wakibisha itabidi tu-list miongozo yote iliyoombwa tangu Anne makinda alipoingia Bungeni.

  Ni kazi ndefu lakini inawezekana maana hansard ni public and easily accessible document.

  Enzi
   
 2. Chuck j

  Chuck j JF-Expert Member

  #2
  Jun 29, 2012
  Joined: Jun 17, 2011
  Messages: 1,984
  Likes Received: 416
  Trophy Points: 180
  Utanipata tuu,,,,,,,
  Kwahoja yako, kweli unakitu,,ccm wwamezoea, tena sana,,watakoma mwaka huu,,,
   
 3. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #3
  Jun 29, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  Hata hoja na Lukuvi kumowndoa mnyika ulikuw aupuuzi.Mzee mzima badala ya kusikiliza hoja alikuwa busy kutafuta pahala pa kumdaka Mnyika.Huwa napata taabu sana na wabunge wa CCM. -wanakubali hoja kwa alimia 100 mpaka 200 halafu wananza elezea shida zao ambao ngekuwa ni point basi ungezitoa hadi zibaki -100% hadi 2000%. -Wanazomea kama watoto. -wanalazimisha majibu. -hawajui tofauti ya miradi ya UN,WORLD BANK, IMF,ADB ambayo serikali yoyote ingepewa hiyo mikopo au hat misaada. -Wanashambulia CDM kwa mambo ya uzushi na yapo wazi kuwa wamefundishwa kwani yana pattern moja. -Hawaheshinu vijana wa CDM ,huku wansahau nao wana vijana, na vijana wa CDM wapo safi kuliko mbunge yeyote wa CCM. Napata huzuni, kwa chama kilichonivalisha scurf, na magwanda ya kijani wakaniita Chipukizi, wakaniita kamanda...najivunia kuwa sikuwahi ipenda nyumba yao.Ni kama walinibaka kifikra, na kuchukua uhuru wangu nikashiriki ushirika mbaya. SIJUI KWANINI HAWTAKI INGIA KABURINI KWA AMANI KM MBINGU NDIO WAITAKAYO?
   
 4. k

  kijiichake JF-Expert Member

  #4
  Jun 29, 2012
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 285
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Yaani hawa wabunge wa ccm wamezeeka vibaya, kuna msemo usemwao kwamba palipo na wazee hapaharibiki neno nami napingana nao kwa aslimia mia moja kwamba kama wazee ni hawa wa ccm like lusinde, komba, and kijana mchumi mwikulu mchemba? Basi hakuna haja ya kuwa na bunge ama mwakilishi wa jimbo, siku hizi silitazami bunge coz bunge letu linakaa like nyumba ya kuuziwa pombe kali kama gongo na chang'aa, yaani bar ya chubuku. Nadhani wabunge hawa wa ccm wanakunywa kwanza viroba kama kumi hivi ndo waingie bungeni, aibu kwao.
   
 5. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #5
  Jun 29, 2012
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Maandiko yanasema ukizeheka utapelekwa usipotaka...
   
 6. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #6
  Jun 29, 2012
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Dah short article lakini full madini...
   
Loading...