tamu 3
Member
- Dec 11, 2024
- 88
- 216
Tabia ya watu KUOMBA HELA inakuja kwa kasi sana.
Sio kwenye undugu, sio kwenye Urafiki, kwenye Mapenzi ndio usiseme Sasa.
Utasikia, Oi! Kama una ten haina kazi nifanyie utaratibu, kuna mishe nasikilizia !
Eti ten haina kazi. Kwa maisha gani mwamba uwe na ten haina kazi? Acha utani!
Mwingine sasa utasikia Mzee huku maduka yamefungwa, em nitumie buku tano chap nijiunge bando, kesho mapema narekebisha
Bora hata huyu uongo wake siyo mkali sana kama huyu anayesema oi huku leo ATM zote hazifanyi kazi nirekebishie ten chap narudisha mapema!😄😄
Ukimnyima anakutishia kwamba kumbuka kuna kesho, we poa tu!
Zamani hii tabia ya kuombaomba tulijua ni ya dada zetu tu lakini siku hizi mpaka wanaume wamo
Maana siku hizi hata vijana wa kiume wanaomba zawadi, usipo waletea wananuna. Nyiee! Hii sijaipenda kabisa.
Kijana wa kiume hata kumtumia mwanaume mwenzako sms ya nipigie inashitua sana. Tena anaandika pg🫢🫢. Hapana bhana!
Siku hizi dada zetu wanalalamika sana kwamba vijana wa kiume mnawaomba sana hela. Hii kiafrika haikubaliki!
Tabia hii ya kuomba watu hela imetuharibia ule utamaduni wa kusalimiana na kujuliana hali tuliokuwa nao huko nyuma.
Siku hizi ni hatari kumjulia hali mtu. Kuna mtu ukimsalimia hapo hapo anakuomba hela.
Sasa ole wako umwambie ntakucheki, inageuka kuwa deni, zitapigwa simu mpaka ukome. Ndani ya siku moja utakuta missed calls mpaka 200. Atakuomba utadhani pesa zako ni zake.
Hata ule utamaduni wa kuaga ndugu, jamaa na masela wakati unasafiri ili wakutakie baraka tele umeondoka. Watu sasa wanaogopa kuaga wataombwa kurudi na vitu.
Kama unaenda Kigoma utaagizwa dagaa, mawese, migebuka na vitenge vya Congo as if kule unakwenda kuviokota mtoni. Maana mtoni ndiko kuna vya bure inasema methali ya waha
Kama unakwenda Mbeya jiandae kuagizwa mchele na maharage ya Soya maji mara moja.
Unakwenda Mwanza watakutuma Sangara na senti tano hawakupi. Sasa usiwaletee. Utanuniwa ukome.
Nimeona niyaseme haya kabla hujalala. Kama umenielewa naomba ukamwambie na jamaa yako naye aache hii tabia, anatukera sana.
Mwambie jamaa yako kuna watu siku hizi wakimuona mbele wanamkwepa ili asiwaombe hela.
🤡🤡