Tabia tatu tunazopaswa kumuiga paka

Mwl Philemon

Member
Nov 29, 2018
61
67
Paka ama nyau kama wengi tunavyo mtamba ni mnyama wa aina yake na ana sifa za kipekee sana hasa ukija kwenye suala la utafutaji au uchakalikaji kwa lugha zetu za mitaa.

Mnyama huyu ambaye yupo katika makundi mawili yaani paka wa nyumbani na paka wa porini anaweza kutufunza mambo kadha wa kadha katika kuishi kwetu kama wanadamu na kupitia hayo tukaweza kuwa na mafanikio makubwa katika nyanja mbalimbali za kimaisha hasa kwenye uchumi na kijamii.

Leo nataka tuzungumzie mambo matano makubwa kutoka kwa paka ambayo ukifanikiwa kuiga na kujijengea tabia na sifa za namna hiyo basi bila shaka utakuwa mtu wa tofauti na mwenye nguvu kubwa sana za kimusukumokatika utekelezaji wa mambo yako na unaweza kuwavutia wengine pia kuwa kama wewe, mambo hayo ni kama yafuatayo

1: Mpole ila Jasiri na katiri sana anapohitaji kukumirisha jambo lake.
Ndiyo, si rahisi kumshuhudia paka akiwa anagombana au kupigana na mara chache yanapomkuta mazingira ya fujo hujitahidi kuyaepukuka aidha kwa kumtisha mbaya wake au kukimbia mbali na adui yake. Lakini linapokuja suala linalo mlazimisha apambane huwa si muoga kabisa na mara nyingi huweza kuyashinda mapambano yake. Ukiachana na panya ambaye paka hutumia kama chakula chake, pia nyoka humtambua kiumbe paka wanapokutana. Inasemekana hata binadamu ukimfungia paka akakosa pa kupita ili kukuepuka unapomfanyia vurumai basi anaweza kuushambulia na kukusababishia majera makubwa.

Kama Binadamu ukijifunza tabia hii ya paka kwanza utabaki na maadui wachache sana na halisi sana. Kutokana na upole wako wengi watavutiwa na wewe na watakuwa tayari kukisikia maana kutokana na upole wako bila shaka utakuwa na uchaguzi sahihi wa nini cha kuzungumza na kwa wakati gani.

2:Hategemei kundi na hana makundi

MMnyama huyu huweza kutekeleza majukumu yake ya kila siku kwa kujitegemea mwenyewe. Huwezi kumukuta paka anawinda na rafiki yake, jirani yake, ndugu yake au kitu chochote.

Hapa haimaanishi tujifunze ubinafsi hapana, bali tusizuiliwe kutekeleza majukumu yetu eti kwa kuwa tu fulani hajatuunga mkono. Tunapaswa kuendelea na taratibu tulizo jiwekea bila kujali tuna wa kutuunga mkono au la ili mradi ni halali na haziathiri watu wengine na zina manufaa.

3: Huwa makini sana

Kama umewahi kubahatika kumuona paka wakati akifanya mawindo yake utakubaliana na mimi ni mnyama ambaye huweka uangalifu mkubwa sana kwenye kusudio lake. Na kutokana na kuwa makini huweza kufanikisha malengo yake kwa kiwango kikubwa.
Hapa tunapaswa kujifunza ufuatiliaji wa mambo tunayokusudia uwe wa kiwango cha juu. Kama huwezi kufuatilia usianzishe maana kuanguka hakutakuwa mbali na wewe.

3:Huwa mkimya.

Paka anapopanga kwenye kuwinda huondoka kimya mpaka sehemu ya mawindo na mpaka anapokamilisha mawindo. Hujulikana kuwa alikuwa mawindoni anapoonekana na windo lake.
Hapa tujifunze kutoweka wazi kila tunalofikiria mengine ni hatima zetu.
images (1).jpeg
 
Paka ana maisha ya siri sana kila kitu kwake anakifanya kwa kisiri,hata kunyanduana huwez waona unashitukia tu mtu ana mimba.
Hata kwenye inshu za kuchuma dawa yake yakujitibu anapopata madhara labda ya kula sumu au kagombana na nyoka,dawa huenda kuchuma kwa kificho
 
Kwa ninyi msiowapenda Nyau, Hapo awali nilikuwa na mitazamo yenu. Baadae mtizamo ulibadilika. Hadi sasa nyau ni mnyama nimpendae yamkini kuliko wanyama wote duniani. Huwaga ninaishi nao kwa amani sana. Wanaletaga "peace of mind"

JESUS IS SAVIOR
 
Paka ama nyau kama wengi tunavyo mtamba ni mnyama wa aina yake na ana sifa za kipekee sana hasa ukija kwenye suala la utafutaji au uchakalikaji kwa lugha zetu za mitaa.

Mnyama huyu ambaye yupo katika makundi mawili yaani paka wa nyumbani na paka wa porini anaweza kutufunza mambo kadha wa kadha katika kuishi kwetu kama wanadamu na kupitia hayo tukaweza kuwa na mafanikio makubwa katika nyanja mbalimbali za kimaisha hasa kwenye uchumi na kijamii.

Leo nataka tuzungumzie mambo matano makubwa kutoka kwa paka ambayo ukifanikiwa kuiga na kujijengea tabia na sifa za namna hiyo basi bila shaka utakuwa mtu wa tofauti na mwenye nguvu kubwa sana za kimusukumokatika utekelezaji wa mambo yako na unaweza kuwavutia wengine pia kuwa kama wewe, mambo hayo ni kama yafuatayo

1: Mpole ila Jasiri na katiri sana anapohitaji kukumirisha jambo lake.
Ndiyo, si rahisi kumshuhudia paka akiwa anagombana au kupigana na mara chache yanapomkuta mazingira ya fujo hujitahidi kuyaepukuka aidha kwa kumtisha mbaya wake au kukimbia mbali na adui yake. Lakini linapokuja suala linalo mlazimisha apambane huwa si muoga kabisa na mara nyingi huweza kuyashinda mapambano yake. Ukiachana na panya ambaye paka hutumia kama chakula chake, pia nyoka humtambua kiumbe paka wanapokutana. Inasemekana hata binadamu ukimfungia paka akakosa pa kupita ili kukuepuka unapomfanyia vurumai basi anaweza kuushambulia na kukusababishia majera makubwa.

Kama Binadamu ukijifunza tabia hii ya paka kwanza utabaki na maadui wachache sana na halisi sana. Kutokana na upole wako wengi watavutiwa na wewe na watakuwa tayari kukisikia maana kutokana na upole wako bila shaka utakuwa na uchaguzi sahihi wa nini cha kuzungumza na kwa wakati gani.

2:Hategemei kundi na hana makundi

MMnyama huyu huweza kutekeleza majukumu yake ya kila siku kwa kujitegemea mwenyewe. Huwezi kumukuta paka anawinda na rafiki yake, jirani yake, ndugu yake au kitu chochote.

Hapa haimaanishi tujifunze ubinafsi hapana, bali tusizuiliwe kutekeleza majukumu yetu eti kwa kuwa tu fulani hajatuunga mkono. Tunapaswa kuendelea na taratibu tulizo jiwekea bila kujali tuna wa kutuunga mkono au la ili mradi ni halali na haziathiri watu wengine na zina manufaa.

3: Huwa makini sana

Kama umewahi kubahatika kumuona paka wakati akifanya mawindo yake utakubaliana na mimi ni mnyama ambaye huweka uangalifu mkubwa sana kwenye kusudio lake. Na kutokana na kuwa makini huweza kufanikisha malengo yake kwa kiwango kikubwa.
Hapa tunapaswa kujifunza ufuatiliaji wa mambo tunayokusudia uwe wa kiwango cha juu. Kama huwezi kufuatilia usianzishe maana kuanguka hakutakuwa mbali na wewe.

3:Huwa mkimya.

Paka anapopanga kwenye kuwinda huondoka kimya mpaka sehemu ya mawindo na mpaka anapokamilisha mawindo. Hujulikana kuwa alikuwa mawindoni anapoonekana na windo lake.
Hapa tujifunze kutoweka wazi kila tunalofikiria mengine ni hatima zetu.
Daah tozo zinachanganya sana.
Hii habari ni ya chatu au paka?
Mkuu wewe ni mganga umechanganya madawa?
 
Back
Top Bottom