Tabia njema

CleverKING

JF-Expert Member
Apr 24, 2014
8,502
25,469
Tabia Njema...

Wakati huu tunaoishi mengi zaidi ya kuharibu tabia njema yamedhihiri kuliko wakati mwingine wowote ule wa historia ya mwanadamu, Kwa sababu ya kukua kwa njia za habari na mawasiliano na kuporomoka kwa maadili,

Utaona mambo machafu na ya aibu yakitendeka popote ulimwenguni, basi sehemu zote yatadhihirishwa na kupigiwa debe kwa ubora wake, na wala sio kwa ubaya wake, au kuchusha kwake,

Imekuwa rahisi kwa walimwengu kuzikubali tabia zote chafu na kuzitenda kwa zile sifa njema kemkem zinazopewa tabia hizo chafu na kulazimishiwa katika akili,
Leo ukiangalia sehemu nyingi utaona kuporomoka kwa maadili, matokeo yake kila yale yenye kuleta utulivu, amani yamepotea badala yake utasikia, au utaona maasi yaliyozagaa, maingiliano ya kijamii kuharibika mapenzi, amani,heshima, utulivu miongoni mwa wanajamii kukosekana watoto kukosa amani kwa wazazi wao, wazazi kukosa amani kwa watoto wao,

Ndoa ambayo ni sababu ya kupata utulivu imekuwa ni sehemu za khiana na kulaniana, wanyama na mimea havikusalimika, unyanyasaji wa kila aina, wizi, mauaji, ufisadi wa kila jinsi na khofu vimeenea,

Cha kusikitisha miongoni mwa jamii nyingi kwa kule kuzama kwao katika upotofu zimekosa muelekeo, matokeo yake yale ya tabia njema ya kuirekebisha jamii yanapigwa vita, na miongoni ya yale ya upotovu na kuleta madhara yanapambiwa na kuonekana kuwa ni mtindo.

Mfano wa machache mwa mengi ya kuchusha ni:-

Wanaume kujifananisha na wanawake na
Wanawake kujifananisha na wanaume kwa mavazi, mitindo kama vile kwa wanaume kuvaa hereni, mikufu, hali kadhalika kuvaa mavazi yasio kuwa na maadili, kuongezeka kwa ulevi, rushwa, ukatili.
Kutumiwa wanawake kama chombo cha kutangazia biashara.
Ndoa za jinsi moja katika jamii na mengineyo,

Namuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu atuepushe na atuongoze na vizazi vyetu katika kufanya yenye kheri.
 
Back
Top Bottom