Mkulima na Mfugaji
JF-Expert Member
- Jul 26, 2013
- 1,056
- 1,867
Mimi ni kijana ambaye niko kwenye ndoa naelekea mwaka wa pili sasa. Kama kawaida kwenye ndoa kuna milima na mabonde ya kupitia, na pia kwenye ndoa kuna Raha na karaha. Ila kwa Mke wangu kila anaponikwaza adhabu ambayo inamtesa nikimpa ni kususia chakula,na kumtenga kitandani yaani adhabu hizi huwa zinampa sana Tabu adhabu hii.
Alishawahi kuniambia kwamba hata kama unakasirika ila kula chakula changu halafu endelea kununa, kuna siku aliniudhi usiku nikamtenga kitanda nilichukua mkeka nikatandika sebuleni, kuja kusituka usiku wa manane namuona pembeni yangu kalala ikabidi nimuamshe tukalale kitandani.
Sasa leo ameniuzi tokea asubuhi sijala na yeye pia tokea asubuhi mpaka jioni ya leo hajakula kitu na ananyonyesha. Je tabia hii ya mke wangu inaashiria nini?