Tabia hii inakera sana.

Mkeshaji

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2011
Posts
4,258
Reaction score
1,418
Utakuta mtu yupo kwenye usafiri wa umma. Ameshikilia simu anatuma meseji. Jamaa mwingine yuko pembeni, bize anakodolea kila neno analoandika mwenzie. Hivi mtu anapata faida gani kufuatilia kusoma kitu kisichomuhusu?

Zipo kero nyingi zinazotaka kufanana na hii katika maeneo ya public. Hii ni mojawapo.

Tafadhali tuwe wastaarabu.

Wikiendi njema.
 
Afadhali hii ukimstukia unaficha. Nakereka na wanaoongea kwa sauti ya juu tena mambo private kama umbea katika public transport.
 
Na wewe unayeandika sms huku watu wako kwenya kadamnasi unategemea nini? Wewe unayeandika ujumbe ndiye unayekera kwa maana hukulazimishwa kuandika ujumbe kwenye kadamnasi!
 


Ukimwona yuko busy kusoma sms yako mweleze tu, hata akiwa mkali ujumbe utakuwa umefika na ukweli utakuweka huru kuliko kubaki unaumia moyoni na yeye anabaki na amani ya moyo wake.
 
kero zipo nyingi sana ila sio iyoo uliyosema: kero ni hizi
kula vitu vyenye harufu kwenye daladala...
kuongea kwenye daladala wakati hujapiga mswaki...
kuongea na simu kwa sauti ya juu....

kila mtu ana ustaarabu wake... Mungu akusaidie ununue gari lako usipate izo kero... lasivyo zoea tuu
 

Mmmh..!!
 
Na wewe unayeandika sms huku watu wako kwenya kadamnasi unategemea nini? Wewe unayeandika ujumbe ndiye unayekera kwa maana hukulazimishwa kuandika ujumbe kwenye kadamnasi!

Si anamuonyeshea kuwa ana simu ya bei mbaya............................!:rockon:
 
sasa mtu kasimama kwenye foleni masaa mawili jua kali joto harufu za vikwapa huna la kufanya gazeti huwezi kusoma sasa kwanini usisome msg ya mtu anayetuma? ili kupoteza muda? (kwa wale wa dar)
 
kuna mdada mmoja alishawahi kumpa mtu simu asome alichoandika alimwambia hivi huyo mkaka nanukuu '' naona unapata shida sana kuchungulia sms sasa chukua simu usome kabisa''
 
Kuna mdada mmoja alikuwa amepangana na babu ndani ya daladala, akawa anaandika msg, alipogundua babu anaisoma akaifuta na kuanza kuandika upya, aliandika hivi; haya MANYOKA hayatulii humu ndani ya begi, yamenishinda, nataka kuyaachia humu kwenye daladala. Unajua nini kilifuata?
 
Na wewe unayeandika sms huku watu wako kwenya kadamnasi unategemea nini? Wewe unayeandika ujumbe ndiye unayekera kwa maana hukulazimishwa kuandika ujumbe kwenye kadamnasi!
Dogo unadhani kutumia simu ni sawa na kuvuta sigara eeh! Nyambaaaf!
 
kuna mdada mmoja alishawahi kumpa mtu simu asome alichoandika alimwambia hivi huyo mkaka nanukuu '' naona unapata shida sana kuchungulia sms sasa chukua simu usome kabisa''
Sijui unapata faida gani kuchungulia meseji ya mtu mwingine....tena humjui.
 
mbaya nyingine... In public transport gari imejaa mko foleni tena mchana jua kali...MAJITU YANAJAMBA KWENYE GARI
 

chenga! Duh!
 
Na wewe unayeandika sms huku watu wako kwenya kadamnasi unategemea nini? Wewe unayeandika ujumbe ndiye unayekera kwa maana hukulazimishwa kuandika ujumbe kwenye kadamnasi!

basi haina maana tuwe na simu za mkononi
 
kero ni kero kweli inakera
majibu utapata macho hayana pazia
kwangu pia ni kero nami yanikera
kwake isiyemkera, yeye yake ndo tabia
leo tunakukanya, tabia chafu na mbaya uache
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…