Tabia hatari katika mahusiano ya kimapenzi; Jirekebisheni.

Tabia hatari katika mahusiano ya kimapenzi; Jirekebisheni.

Nicas Mtei

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2010
Posts
11,556
Reaction score
7,113
black-couple-arguing-pf3-378x309.jpg



Tunazungumzia mapenzi katika sura ya kipekee kwa kuwa yanahitaji thamani ya hali ya juu. Yanaheshimiwa kupita kiasi kwa sababu yenyewe ni sanaa kiranja ambayo kila mtu lazima atayapitia..... Katika mapenzi hayo hayo kuna mambo ambayo kwa namna moja ama nyingne ni hatari mno katika mahusiano.... Endapo mtashindwa kuyazuia mambo hayo basi yatakuwa sumu hatari katika mahusiano yenu kitu ambacho kitapelekea kutoaminiana au kuachana.

Kila mmoja anapoingia katika uhusiano wa kimapenzi, moja kwa moja ndoto zake huwa ni kumfanya mwenzi wake kuwa wa kudumu. Atajiwekea malengo hata yasiyotekelezeka ilimradi airidhishe nafsi yake.


Wengi waliopo kwenye mahusiano huwa wanakuwa na ndoto nyingi za kufika mbali zaidi, lakini ndoto hizo hugeuka za alinacha kama si kitendawili kwa kuwa hatuwezi kujirekebisha tabia zetu ambazo ni hatarishi katika mahusiani. Matunda ya hali hiyo ni kuwa na kizazi chenye kujiwekea matarajio ya blah blah kila siku.....

Pointi ya msingi hapa kama kweli tunataka kuwa na mapenzi ya kudumu ni kujua udhaifu wetu angali bado mapema. Kutambua mambo ambayo ni sumu, zinayoweza kuuua uhusiano wetu ili tuzichukue kama changamoto, kisha tuzikabili na kushinda.

Kwa leo ningependa tujikite katika kujadili jambo moja kubwa ambalo linaweza kuwa sumu kali katika mahusiani yenu... Wengi huwa wanadhani kuwa ni jambo dogo sana na ni jambo ambalo sio rahisi kuvunja uhusiano... ukweli ni kwamba hayo ni mawazo potofu sana... Jambo hilo hufanywa na wote katika mahusiano... Mwanamke hufanya pia mwanaume hufanya...... Jambo lenyewe ni :

UONGO

Tafsiri yake ni tabia ya kutosema ukweli, yaani ujanja mwingi na kudanganya ili kujiweka katika mazingira salama. Pamoja na ukweli kwamba wengi huutumia katika kujipa ushindi wa mezani, lakini hii ni sumu nyingine kali kwenye uhusiano wa kimapenzi.



Maana nzuri katika tafsiri fupi ni kuwa uongo ni dharau kwakuwa angemheshimu, asingemdanganya. Mtu anayemuongopea mpenzi wake, huyo si muoga kwenye uhusiano, hivyo anakuwa amepitwa na nguzo muhimu ya kulifanya penzi lake lidumu kwa miaka mingi.


Ukichunguza kwa makini, asilimia kubwa ya watu waliodumu na wenzi wao ni wale wanaoishi kwa hofu katika uhusiano. Anauheshimu, kwahiyo anaogopa kuuvunja. Anaweka mikakati ya kujiweka salama mbele ya laazizi wake. Lakini hayo si ndiyo mapenzi?


Aidha, ukichunguza tena kwa makini, utabaini kuwa uongo, maana yake ni kujiona unajua vitu vingi kuliko wengine. Wewe ni fundi wa kugeuza maneno na unaweza kumfanya mtu aamini moja jumlisha moja ni tatu. Lakini mapenzi hayataki hivyo!



Wengi huuchukulia uongo kama chachandu ya mapenzi, huku asilimia kubwa wakiufanya kuwa sehemu ya maisha yao. Je, hujawahi kumuona mtu asiyejua kusema ukweli? Na kila akibadilisha pointi, anapandisha uongo juu ya uongo?



Jibu; watu wa aina hiyo ni wengi, wamejaa kila sehemu, lakini ni busara kujiuliza swali lingine, unadhani wanapata faida? Jawabu lake ni kuwa inawezekana kupata faida, lakini mbona wengi wao waliishia kuumbuka? Akili kumkichwa!



Unatoka nje, ukirudi unadanganya, unasema uongo ili kumnasa ndege wako, lakini lazima ukumbuke kuwa za mwizi ni arobaini.

Uongo ni Sumu... Jirekebishe haraka sasa.
 
Ni kweli mkuu umenena vema sana...

Ila kwa mapenzi yetu haya ya kibongo ambayo watu hutaka kusikia kile wanachopenda kusikia huwei kuwa mkweli ukadumu...Believe me ukiwa msema kweli sana unaonekana kama mshamba fulani hivi....

Ila all in all dawa ni kujifinza useme nini wakati gani baaasi...hata kama ni uongo au ukweli....
 
Ni kweli mkuu umenena vema sana...

Ila kwa mapenzi yetu haya ya kibongo ambayo watu hutaka kusikia kile wanachopenda kusikia huwei kuwa mkweli ukadumu...Believe me ukiwa msema kweli sana unaonekana kama mshamba fulani hivi....

Ila all in all dawa ni kujifinza useme nini wakati gani baaasi...hata kama ni uongo au ukweli....


Pamoja na yote hayo.... haiwezi kuondoa ukweli kwamba uongo ni sumu ya mapenzi
 
sihusiki hapa maana sidanganyagi mimi ,btw huyo hapo kwenye avatar yako ni wewe mwenyewe eti

Kama wewe hudanganyi basi inawezekana kuwa huwa unadanganywa....
 
Ni sumu ya mapenzi kwa watu walio serious ila kwa wenzangu na mimi tuliokutana kimjini mjini...huchelewi kuachwa aiseeee.....
kWELI... Pia kadri ya muda mtakaokuwa pamoja ndo inaweza kukupa ujasiri wa kujua ni nanma gani uhusiano wenu uwepo
 
uongo kweli mbaya ndo maana mtu akijiangusha eneo la penati anapewa kadi ya njano uongo kwa mkeo ni zaidi ya kujianguasha eneo la penati ni kujiangusha ndani ya gori kabisa.
 
Back
Top Bottom