Tabia gani hupendi kuingia nayo 2019?

Tabia gani hupendi kuingia nayo 2019?

raiswenu

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2018
Posts
1,036
Reaction score
1,803
Kila mtu kwa nafasi yake anamapungufu yake, ni busara kila mtu kujitathimini na kujua ni mapungufu yapi yanamrudisha nyuma katika nyaja tofautitofauti za kujiletea maendeleo, kwa kufanya hivyo unapata nafasi ya kusonga mbele katika kufikia malengo yako.

Nakumbuka nilikuwa nina tabia kadhaa ambazo kwa mwaka huu nimejitahidi kupambana nazo na kuhakikisha kuwa ninaziacha, mojawapo ni tabia ya kuahirisha mambo bila sababu ya msingi, naweza kuwa ninampango wa kufanya kazi flani kwa muda fulani

Ukifika huo muda najiona mood iko down so kinachofuata hapo ni kuahirisha, nakumbuka mwaka huu ndio mara yangu ya kwanza kusoma kitabu ambacho siyo novel (serious knowledge book) na nikakimaliza chote ndani ya muda mfupi kinaitwa “100 ways to motivate yourself” kimeandikwa na Steve Chandler

Kwa sababu nilizoea kusoma hivi vitabu vyenye sukari nyingi(reading for pleasure) kupitia kitabu hiki kuna mbinu kadhaa zimenisaidia sana. Nitaelezea chache.

Kufanya kidogokidogo- kupitia kitabu hiki nimejifunza hii mbinu ya kufanya kidogokidogo na imenisaidia sana, kwa mfano nataka labda kufanya mazoezi kulingana na ratiba yangu, but niko so down kiasi kwamba hata sijisikii kufanya hivyo(uvivu).

Anza kwa kufanya zoezi ambalo ni kidogo kabisa ambalo litakumotivate kuwa kwenye full mood ya kufanya mazoezi, kwa mfano unaweza kuanza kwa kutembea tu, ukasema labda ngoja nitembee nusu km, ukiimaliza unakuwa motivated kuongeza nusu ingine na mwiso utakuwa umekamilisha ratiba yako, hii njia unaweza kuitumia kwenye kazi yoyote.

Kuongeza muda wa kuahirisha- tenga muda kadhaa mfano jiwekee dk labda kumi,”ngoja nifanye hii kazi kwa dk 10 then niachane nayo” zikiisha hizo dk kumi, ongeza zingine hata tano kwa kufanya hivyo utajikuta umekuwa motivated na umemaliza kazi yako.

Sitaweza kuelezea kila kitu, ila nimeona ni busara kukiweka hapa hicho kitabu ili kwa mtu anayehitaji mabadiliko binafsi aweze kukisoma pia(sharing is caring).

Self motivation ni mhimu sana katika kufanya mambo kwa wakati ili kufikia malengo yako, kuiweka umakini kwenye jambo lolote litakuwa. naamini kwa mwaka huu kila mtu amejiwekea malengo yake, malengo bila matendo au tabia sahihi ni vigumu kufanikiwa.

Je kwa mwaka huu ni tabia gani umepambana nazo? Na umetumia mbinu gani kupambana nazo? Tabia gani bado zinakusumbua ambazo hutaki kuendelea nazo mwaka 2019? Tupia hapo chini tuweze kusaidiana na kupeana ushauri ilikufikia malengo yetu.

NAWASILISHAView attachment 100_Ways_To_Motivate_Yourself_Change_Your_Life_Forever.pdf
 
Kila mtu kwa nafasi yake anamapungufu yake, ni busara kila mtu kujitathimini na kujua ni mapungufu yapi yanamrudisha nyuma katika nyaja tofautitofauti za kujiletea maendeleo, kwa kufanya hivyo unapata nafasi ya kusonga mbele katika kufikia malengo yako.
Nakumbuka nilikuwa nina tabia kadhaa ambazo kwa mwaka huu nimejitahidi kupambana nazo na kuhakikisha kuwa ninaziacha, mojawapo ni tabia ya kuahirisha mambo bila sababu ya msingi , naweza kuwa ninampango wa kufanya kazi flani kwa muda flani, ukifika huo muda najiona mood iko down so kinachofuata hapo ni kuahirisha, nakumbuka mwaka huu ndio mara yangu ya kwanza kusoma kitabu ambacho siyo novel (serious knowledge book)na nikakimaliza chote ndani ya muda mfupi kinaitwa “100 ways to motivate yourself” kimeandikwa na steve chandler, kwa sababu nilizoea kusoma hivi vitabu vyenye sukari nyingi(reading for pleasure) kupitia kitabu hiki kuna mbinu kadhaa zimenisaidia sana. Nitaelezea chache.
Kufanya kidogokidogo- kupitia kitabu hiki nimejifunza hii mbinu ya kufanya kidogokidogo na imenisaidia sana, kwa mfano nataka labda kufanya mazoezi kulingana na ratiba yangu, but niko so down kiasi kwamba hata sijisikii kufanya hivyo(uvivu). Anza kwa kufanya zoezi ambalo ni kidogo kabisa ambalo litakumotivate kuwa kwenye full mood ya kufanya mazoezi, kwa mfano unaweza kuanza kwa kutembea tu, ukasema labda ngoja nitembee nusu km, ukiimaliza unakuwa motivated kuongeza nusu ingine na mwiso utakuwa umekamilisha ratiba yako, hii njia unaweza kuitumia kwenye kazi yoyote.
Kuongeza muda wa kuahirisha- tenga muda kadhaa mfano jiwekee dk labda kumi,”ngoja nifanye hii kazi kwa dk 10 then niachane nayo” zikiisha hizo dk kumi, ongeza zingine hata tano kwa kufanya hivyo utajikuta umekuwa motivated na umemaliza kazi yako.
Sitaweza kuelezea kila kitu, ila nimeona ni busara kukiweka hapa hicho kitabu ili kwa mtu anayehitaji mabadiliko binafsi aweze kukisoma pia(sharing is caring).
Self motivation ni mhimu sana katika kufanya mambo kwa wakati ili kufikia malengo yako, kuiweka umakini kwenye jambo lolote litakuwa. naamini kwa mwaka huu kila mtu amejiwekea malengo yake, malengo bila matendo au tabia sahihi ni vigumu kufanikiwa.
Je kwa mwaka huu ni tabia gani umepambana nazo? Na umetumia mbinu gani kupambana nazo? Tabia gani bado zinakusumbua ambazo hutaki kuendelea nazo mwaka 2019? Tupia hapo chini tuweze kusaidiana na kupeana ushauri ilikufikia malengo yetu.NAWASILISHAView attachment 977445
Wew nahis unakipawa ndani yako, na shetani anakukwamisha mambo mengi sana, na uko msoto sana but uwezo wako ni mkubwa sana,

Mungu anataka ufanye kama alivo panga.

And all the same to me.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom