Tabia 8 Zinazochelewesha Mafanikio

Tabia 8 Zinazochelewesha Mafanikio

stabilityman

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2024
Posts
604
Reaction score
1,237
*✨ Tabia 8 Zinazochelewesha Mafanikio —

🔷 1. Aliyemaliza chuo na hajawahi kujifunza ujuzi wowote wa ziada
Kama hana kazi, atateseka sana. Soko la ajira limejaa ushindani. Elimu ya chuo haitoshi bila ujuzi wa vitendo unaolipa bila ajira kama digital marketing, graphic design, coding, video editing, sales, nk. Ujuzi huu ndio unaomtofautisha mtu sokoni. Bila hivyo, mtu hubaki kusubiri ajira ambazo ni chache.

🔷 2. Anayelaumu hakuna wateja, lakini hafanyi juhudi za masoko
Wateja hawawezi kujua tu kuwa una bidhaa au huduma.
Kama unataka kuuza, watu wajue upo.
Fanya masoko kila siku–tumia mitandao ya kijamii, tuma broadcast WhatsApp, nenda maonyesho, tafuta referrals.
Biashara ni vita ya akili, si ya kusubiri bahati.

🔷 3. Anayedharau mitandao ya kijamii lakini anatarajia kuuza
Dunia imehamia mtandaoni. Kama hujajifunza kutumia Instagram, WhatsApp Business, Facebook au TikTok kwa biashara yako, unachelewesha maendeleo yako.
Hapo ndipo wateja wako walipo.
Uzuri wa mitandao ya kijamii, haina upendeleo. Ni wewe tu.

🔷 4. Anayesema haoni cha kufanya
Tanzania ina fursa nyingi mno.
Tatizo si kwamba hakuna cha kufanya, bali ni hofu, kiburi na kutaka kuanza ukiwa umekamilika.
Anza kidogo na kilicho mkononi.
Fursa hazitangazwi mabango–zipo kwenye changamoto za watu.

🔷 5. Anayetegemea ndugu au marafiki kila wakati
Hakuna atakayekuvumilia milele.
Kutegemea watu kila wakati hukufanya usifikirie kuhusu kujitegemea.
Anza na kidogo ulicho nacho–sio lazima uwe na mtaji mkubwa.
Jijenge, hata kama ni kwa taabu.

🔷 6. Anayependa kusema ‘Kesho rasmi naanza’
Uvivu wa kutokuanza leo ndio muuaji wa ndoto.
Unapanga kila siku lakini huchukui hatua.
Hakuna kesho iliyo bora kuliko leo.
Mafanikio hayangojei ubora–huja kwa kuanza na kuboresha polepole.

🔷 7. Anayekaa na watu wanaolalamika tu maisha bila kuchukua hatua
Mazingira yana nguvu ya kukuathiri.
Ukikaa na walalamikaji, utaanza kuona kila kitu ni kigumu.
Kaa na watu wanaoongea fursa, mikakati, mafanikio, na hatua.
Ukibadilisha social circle yako, unaweza ukabadilisha maisha yako.
Hata page za ku_follow – si unaona ulivyofollow hii kuna vitu unaona vinawezekana?

🔷 8. Wanaotaka matokeo makubwa kwa juhudi ndogo
Mafanikio hayaji kwa njia za mkato.
Kama huna nidhamu ya kujituma, kujifunza kila siku na kubeba majukumu, utasema "maisha ni magumu".
Subira, ubunifu na commitment–hizo ndo gharama za mafanikio ya kweli.

---
Eng JAMES 0743257669
 
Back
Top Bottom