Tabia 10 zinazokufanya uonekane si Msomi au mtu aliyeelimika

Hussein Massanza

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
918
1,994
Taaluma au kuwa msomi ni vitu ambavyo wengi tunapenda na ikiwezekana tutaendelea kusoma sana na kupata vyeti vya kutusababishia kupata vyeo na mara nyingine kupandishwa vyeo. Ukweli wa mambo hakuna mtu mkamilifu, lakini si kauli ya kutafuta sababu ya kuwa na tabia mbaya au zisizo na tija katika taaluma yako. Kuna tabia kumi ambazo unapaswa kuziepuka wakati wote hasa kwenye taaluma yako bila kuwa na visingizio;

1. Tabia ya Uvivu
Sawa, hiki ni kitu cha juu kwenye mtiririko wa tabia za kuziepuka. Uvivu unasababisha mtu kutokumaliza kazi kwa wakati, kushindwa kuongea na wateja au kushindwa kukamilisha mambo, hivyo unakuwa mtu wa kukaa tu na maneno mengi huku ukiwa hauna kitu cha kufanya au una vitu vya kufanya ila unapuuza na kushindwa kufanya kutokana visingizio visivyo na sababu.

2. Uchelewaji
Lazima nikiri watu wengi hufanya vitu kutokana na watu tunaowaheshimu na kupuuzia linapokuja suala la kazi au biashara. Heshima kubwa ni kuheshimu muda, kama umesema utakuwepo saa fulani mahali fulani uwe hapo. Kama utashindwa toa taarifa mapema zaidi ili uonekane ni mtu unayejali na hujapanga kuchelewa.

3. Macho Juu Juu au Tamaa
Sisi sote ni binadamu na ni jamii ya wanyama. Huwa tunapenda kushtuka pale ambapo jinsia tofauti inapopita mbele yetu au kuvutiwa na mtu mwingine. Lakini binadamu huyo huyo anatakiwa kuwa na kiasi na uwezo wa kujitawala kihisia na matendo. Ukishindwa kufanya hivyo unaweza ukawa na umri mkubwa lakini ni mtu ambaye hajakomaa kitu na ubinadamu.

4. Kuwa na Ahadi Hewa/ Matumaini Hewa
Hii ni hali ya kuwa na matumaini ambayo hayapo au hayawezekani. Kama huna uhakika jaribu kuangalia kitabu cha 1913 baada ya dhoruba fulani kuna watu wengine bado watakwambia mambo yako sawa kabisa wala hakuna shida. Usijaribu kupuuza ushauri wa kitaalamu wakati wowote katika taaluma yako.

5. Kutokuwajibika
Ni sawa tu na kuwa mchelewaji, unapomwambia mtu utakuwa sehemu fulani saa fulani na wala usifanye hivyo huko ni kutokuwajibika ipasavyo. Hii inaendana na jambo lolote linalohusu majukumu yako ya kila siku na unafika sehemu unashindwa kufanya na wala huoni ni tatizo wewe si mwajibikaji.

6. Kutokuwa na Mpangilio katika Utendaji
Inawezekana ukifika ofisini kitu cha kwanza ni kuangalia habari kwenye mitandao ukimaliza ni kunywa chai ndo kazi ianze. Wakati huo huo kuna watu ambao unatakiwa kuwahudumia au kujibu barua pepe haraka iwezekanavyo. Hivyo kama unashindwa kupangilia kitu gani ni cha muhimu kuliko kingine una matatizo makubwa.

7. Kushindwa Kujieleza
Ukiwa na uwezo wa kushindwa kujieleza inashangaza uliendaje shule, na umewezaje kupita? Watu wanategemea uwe na uwezo wa kuelezea jambo, hivyo kurahisisha utendaji na wafanyakazi wenzako au wafanyabiashara wenzako.

8. Usiri Mwingi
Ukweli wengi tunapenda kuwa wasiri katika maisha yetu binafsi, lakini kazi zetu haziusiani na usiri huo. Kama unaficha kitu cha msingi kwa wafanyakazi wenzako au wateja hauonyeshi tabia nzuri kama kiongozi, unawafanya wajiulize watakuamini vipi?

9. Kutoa ahadi kubwa isiyotekelezeka
Kila muuzaji mzuri anajua moyo wa kuuza bidhaa na vile vile kuhakikisha bidhaa inamfikia mteja kwa wakati. Kila mjasiriamali huwa anahakikisha anatoa ahadi kubwa, lakini suala ni uwezo wa kumpatia mteja bidhaa hiyo.

10. Kudanganya au Uongo
Rais George W. Bush alisema "unidanganye mara moja, aibu kwako. Ukinidanganya mara mbili, aibu kwangu."

Hisani: Bongo5
 
Which group of people are talking about? employed individuals, business man or investors ? kama vp nipotezee
 
which group of people are talking about? employed individuals, business man or investors ? kama vp nipotezee

Kwani heading inasemaje mkuu?,Hapo ni wote ili mradi wewe ni Msomi,haijalishi umeajiriwa serikalini,Kampuni,au Umejiajiri.
 
Ni kweli kiongozi hizo ni baadhi ya sifa za wasomi ila kwa msomi wa kitanzania ni kinyume chake.
 
Mbona ni kama unaongelea mambo ya "mtu mstaarabu" hata wasiosoma wengi tu mbona wako hivyo
 
Sifa pekee inayobeba sifa zote ulizotaja hapo ambayo kama huna huwezi kuwa na hizo hapo juu ni, kutokuwa mnafiki na mwoga kusema ukweli.Na hii imewashinda viongozi wengi wa POLICCM
 
Ukiangalia sana hata kingereza chenyewe ni majanga harafu ukumbuke kuwa msomi si kujua lugha hata kigogo ni lugha lakini hukijui.
 
Ongea kiswahili acha kujiaibisha
Hajajiaaibisha na wala msimkatishe tamaa kujifunza. Ukiona hivyo ujue tu hiyo sio lugha yake ya asili na hapo anajifunza, mtieni moyo!

Lakini, mbona wengi humu wanaandika kiswahili kibovu huwa hamuwadhalilishi?
 
kuotkujua kujieleza sio tatizo la usomi, wewe kuna watu wan phobia kibao.usiandike vitu kwa kukurupuka fanya research
kwanza.
 
Taaluma au kuwa msomi ni vitu ambavyo wengi tunapenda na ikiwezekana tutaendelea kusoma sana na kupata vyeti vya kutusababishia kupata vyeo na mara nyingine kupandishwa vyeo. Ukweli wa mambo hakuna mtu mkamilifu, lakini si kauli ya kutafuta sababu ya kuwa na tabia mbaya au zisizo na tija katika taaluma yako. Kuna tabia kumi ambazo unapaswa kuziepuka wakati wote hasa kwenye taaluma yako bila kuwa na visingizio;

1. Tabia ya Uvivu
Sawa, hiki ni kitu cha juu kwenye mtiririko wa tabia za kuziepuka. Uvivu unasababisha mtu kutokumaliza kazi kwa wakati, kushindwa kuongea na wateja au kushindwa kukamilisha mambo, hivyo unakuwa mtu wa kukaa tu na maneno mengi huku ukiwa hauna kitu cha kufanya au una vitu vya kufanya ila unapuuza na kushindwa kufanya kutokana visingizio visivyo na sababu.

2. Uchelewaji
Lazima nikiri watu wengi hufanya vitu kutokana na watu tunaowaheshimu na kupuuzia linapokuja suala la kazi au biashara. Heshima kubwa ni kuheshimu muda, kama umesema utakuwepo saa fulani mahali fulani uwe hapo. Kama utashindwa toa taarifa mapema zaidi ili uonekane ni mtu unayejali na hujapanga kuchelewa.

3. Macho Juu Juu au Tamaa
Sisi sote ni binadamu na ni jamii ya wanyama. Huwa tunapenda kushtuka pale ambapo jinsia tofauti inapopita mbele yetu au kuvutiwa na mtu mwingine. Lakini binadamu huyo huyo anatakiwa kuwa na kiasi na uwezo wa kujitawala kihisia na matendo. Ukishindwa kufanya hivyo unaweza ukawa na umri mkubwa lakini ni mtu ambaye hajakomaa kitu na ubinadamu.

4. Kuwa na Ahadi Hewa/ Matumaini Hewa
Hii ni hali ya kuwa na matumaini ambayo hayapo au hayawezekani. Kama huna uhakika jaribu kuangalia kitabu cha 1913 baada ya dhoruba fulani kuna watu wengine bado watakwambia mambo yako sawa kabisa wala hakuna shida. Usijaribu kupuuza ushauri wa kitaalamu wakati wowote katika taaluma yako.

5. Kutokuwajibika
Ni sawa tu na kuwa mchelewaji, unapomwambia mtu utakuwa sehemu fulani saa fulani na wala usifanye hivyo huko ni kutokuwajibika ipasavyo. Hii inaendana na jambo lolote linalohusu majukumu yako ya kila siku na unafika sehemu unashindwa kufanya na wala huoni ni tatizo wewe si mwajibikaji.

6. Kutokuwa na Mpangilio katika Utendaji
Inawezekana ukifika ofisini kitu cha kwanza ni kuangalia habari kwenye mitandao ukimaliza ni kunywa chai ndo kazi ianze. Wakati huo huo kuna watu ambao unatakiwa kuwahudumia au kujibu barua pepe haraka iwezekanavyo. Hivyo kama unashindwa kupangilia kitu gani ni cha muhimu kuliko kingine una matatizo makubwa.

7. Kushindwa Kujieleza
Ukiwa na uwezo wa kushindwa kujieleza inashangaza uliendaje shule, na umewezaje kupita? Watu wanategemea uwe na uwezo wa kuelezea jambo, hivyo kurahisisha utendaji na wafanyakazi wenzako au wafanyabiashara wenzako.

8. Usiri Mwingi
Ukweli wengi tunapenda kuwa wasiri katika maisha yetu binafsi, lakini kazi zetu haziusiani na usiri huo. Kama unaficha kitu cha msingi kwa wafanyakazi wenzako au wateja hauonyeshi tabia nzuri kama kiongozi, unawafanya wajiulize watakuamini vipi?

9. Kutoa ahadi kubwa isiyotekelezeka
Kila muuzaji mzuri anajua moyo wa kuuza bidhaa na vile vile kuhakikisha bidhaa inamfikia mteja kwa wakati. Kila mjasiriamali huwa anahakikisha anatoa ahadi kubwa, lakini suala ni uwezo wa kumpatia mteja bidhaa hiyo.

10. Kudanganya au Uongo
Rais George W. Bush alisema “unidanganye mara moja, aibu kwako. Ukinidanganya mara mbili, aibu kwangu.”

Hisani: Bongo5

Wewe ni mmoja kati ya wanaoitendea haki jf.

Safi sana.
 
Back
Top Bottom