Taazia: Benjamin William Mkapa (1938 - 2020)

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,915
30,259
TAAZIA: BENJAMIN WILLIAM MKAPA NA KITWANA SELEMANI KONDO MARAFIKI WALIOPENDANA KWA DHATI

Kitwana Selemani Kondo wengi huenda watashangaa kusikia kuwa alikuwa rafiki kipenzi wa wa Benjamin William Mkapa urafiki wao ukianzia Government House (sasa Ikulu) mwaka wa 1963, Mkapa alipokwenda kufanya kazi katika ofisi ya Rais Julius Nyerere.

Mkapa anaingia Governnent House anamkuta Kitwana Kondo mwenyeji.

Kitwana Kondo kwa kauli yake kanihadithia kuwa yeye kaingia Government House miaka ya 1950 kuwasilisha kwa Gavana Edward Francis Twining taarifa za kikachero za Nyerere na TANU.

Kitwana Kondo wakati ule alikuwa Special Branch Idara ya Usalama ya Waingereza.

Kwenye jumba hili ambalo leo linaitwa Ikulu ndipo Mkapa alipofahamiana na Kitwana Kondo.

Ukimsikiliza Mzee Kitwana Kondo akikueleza urafiki wake na Mkapa na yale waliofanya pamoja hutopenda amalize kuhadithia na hizo ni siku za ujana wa Mkapa na ndiyo kwanza katoka kumuoa msichana mdogo Anna Mkapa.

Urafiki wao huu baina yake yeye na Mkapa na Mama Mkapa ulidumu hadi Mzee Kondo alipoiaga dunia.

Lakini labda kabla sijaendelea msomaji atakuwa anajiuliza mimi haya nimeyajuaje?

Mzee Kondo alipata kunambia kuwa katika ujana wake alipanga nyumba ya bibi yangu Sophia bint Farija, Mtaa wa Likoma mwisho.

Mzee Kondo ni baba yangu na akinipenda kama mwanae na akiniita mimi mtoto wake na akiwajulisha watu hivyo.

George Mkuchika alipokuja Tanga kama Mkuu wa Mkoa alinambia kuwa Mzee Kondo alimuagiza anitafute na aniangalie kama mdogo wake.

Nilipokutana na Mkuchika alinipa salamu kutoka kwa Mzee Kondo na akaniambia kuwa yeye kama nilivyokuwa mimi Mzee Kondo ni baba yake.

Ninayasema haya kama utangulizi ili nifahamiane na wewe msomaji wangu.

Wengi naamini bila wasiwasi watapigwa na butwaa kubwa isiyoweza kumithilishwa na nguvu yoyote katika siasa za Tanzania nikiwaambia kuwa Mzee Kondo peke yake nje ya Kamati ya Benjamin Mkapa, Jenerali Ulimwengu, Damian Ruhinda na wengineo, Kuchaguliwa rais wa Tanzania, alikuwa Kitwana Selemani Kondo.

Ukipenda unaweza ukamuingiza Mzee Kondo kama mjumbe katika Kamati ya Mkapa ya Uchaguzi wa Rais mwaka 1995.

Najua na naamini msomaji hili limekushangaza.

Nitakushangaza zaidi.

Kwa hayo niliyokueleza ya urafiki wa Mzee Kondo na Mkapa unaweza ukadhani labda Mkapa alimwegemea Kitwana Kondo katika safari yake ya kugombea urais kwa ajili ya urafiki wao wa miaka mingi au kwa ule uanamji wa Mzee Kondo.

Hapana la hasha haikuwa hivyo.

Mwalimu Nyerere mwenyewe ndiye akiyemtuma Mkapa kwa Kitwana Kondo na salamu kuwa ampe msaada Mkapa kushinda uchaguzi wa rais.

Mkapa wala hakumpigia simu Kitwana Kondo kutaka miadi ya kukutana amfikishie salamu za Baba wa Taifa.

Mkapa alimvamia Mzee Kondo nyumbani kwake Oyster Bay kumpa salamu za Mwalimu Nyerere.

Mzee Kondo katika kisa hiki anasema, "Pale pale baada ya mimi kupata salamu zile nikajua Mkapa ndiye atakaekuwa rais ajaye wa Tanzania sikuwa na shaka hata kidogo."

Mzee Kondo alikuwa mpenzi wa mashairi ya Muyaka bin Haji Al Ghassany na kuna ubeti akipenda kuusoma unaomalizikia na maneno haya, "Mbona unaghafilika na jambo lisilo na shaka?"

Mzee Kondo kwa kujua nguvu ya Nyerere hakuwa na shaka kuwa Benjamin Mkapa atashinda mbio zile za rais dhidi ya wagombea wote.

Mzee Kondo hakusikika popote wala kuonekana popote katika ushindi wa Rais Benjamin Mkapa.

Wala Mkapa hajamtaja Kitwana Kondo popote pale katika kitabu cha maisha yake, "My Life, My Purpose,"na kama asingenieleza mimi hili nisingelijua na wewe msomaji wangu pia usingelijua.

Mzee Kondo hili asingelisema ila alighadhibishwa na hii ikawa sababu ya yeye kulifungua sanduku lake la hazina na kutoa kito kama zawadi kwangu ili nisifadhaishwe pale nisomapo magazetini akitukanwa na yeye akanyamaza kimya.

Hakika kito hiki kilikuwa faraja kubwa kwangu nami nimeona nikitoe kukupa wewe ndugu yangu katika wakati huu wa kuomboleza msiba wa mpendwa wetu Benjamin William Mkapa Rais wa tatu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Sisi watoto wa Mzee Kondo tulimwomba sana baba yetu huyu aandike kumbukumbu zake lakini alitukatalia katakata na hivyo kuingia kaburini na hazina zake zote akituacha sisi wanae masikini.

Yapo mengi lakini haya yatoshe kama kumbukumbu ya kumkumbuka mpendwa wetu Benjamin William Mkapa.

Picha: Rais Benjamin William Mkapa akimtunuku Abbas Kleist Sykes medali ya utumishi bora na picha ya pili Mwandishi akifanya mahojiano ya televisheni na Kitwana Selemani Kondo katika miaka ya mwisho ya maisha yake.

ABBAS KLEIST SYKES NA BENJAMIN WILLIAM MKAPA (2).jpg
 
Asante kwa historia hiyo Mzee Mohamed, ila picha ya pili mwandishi akimuhoji Mzee Kondo hujaweka

RIP BW MKAPA
 
Nyerere alikuwa smart sana. Si kuwa alimtuma Ben kwa Kitwana Kondo pekee, wapo wengine. Ile ilikuwa ni namna ya kumuonyesha yeye ana umuhimu wa kipekee!! Ingawa pia kwa ukachero wake KK akawa amejua nini ungependa kusikia.
 
Nyerere alikuwa smart sana. Si kuwa alimtuma Ben kwa Kitwana Kondo pekee, wapo wengine. Ile ilikuwa ni namna ya kumuonyesha yeye ana umuhimu wa kipekee!! Ingawa pia kwa ukachero wake KK akawa amejua nini ungependa kusikia.
KK alikuwa mtoto wa mjini sana. Ila naye ana mambo yake mengi ambayo yalikuwa na walakini.
RIP Mkapa
 
Nyerere alikuwa smart sana. Si kuwa alimtuma Ben kwa Kitwana Kondo pekee, wapo wengine. Ile ilikuwa ni namna ya kumuonyesha yeye ana umuhimu wa kipekee!! Ingawa pia kwa ukachero wake KK akawa amejua nini ungependa kusikia.
Platozoom,
Hao wengine mie nawafahamu na baadhi wananijua.

Na walinijua kwa kutaka msaada katika kipindi kile.

Lakini hao walikuwa wachezea pembeni tu hakuna aliyekuwa na jukumu alilokuwanalo Kitwana Kondo.

Kwangu mimi Mzee Kitwana Kondo hakuwa hivyo unavyotamani wewe iwe na ndiyo maana wewe umekuja kuandika baada yangu.

Utapata shida kuaminika.
 
Kwa kuwa Mkapa alikuwa mkuu wa chuo cha Dodoma, ningependekeza siku ya Jumanne, mwili wake usafirishwe hadi UDOM ili jumuiya ya pale ipate nafasi ya kubid farewell to him.. Tukumbuke, hii ndiyo ilikuwa ajira yake ya mwisho hapa Duniani.
 
Platozoom,
Hao wengine mie nawafahamu na baadhi wananijua.

Na walinijua kwa kutaka msaada katika kipindi kile.

Lakini hao walikuwa wachezea pembeni tu hakuna aliyekuwa na jukumu alilokuwanalo Kitwana Kondo.

Kwangu mimi Mzee Kitwana Kondo hakuwa hivyo unavyotamani wewe iwe na ndiyo maana wewe umekuja kuandika baada yangu.

Utapata shida kuaminika.
Hahaaa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom