Kwa mujibu wa utafiti wako sio?Habari za utafiti wa hivi karibuni toka shirika amaTaasisi ya kimataifa ya Intelijensia ya Kiuchumi/ Economist Intelligence Unit/EIU lenye makao yake makuu jijini London Uingereza, limetoa matokeo yake ya kitafiti kuhusu UCHAGUZI ujao wa 2020 wa Tanzania.
Taasisi hiyo ya kimataifa ambayo ndo think tank kuu ya mambo ya kimataifa katika Nyanja za KISIASA, KIUCHUMI n.k.imetoa utafiti wake.
Miongoni mwa kazi zake kuu ni kufanya Utafiti/Research na ANALYSIS/ UCHAMBUZI ili kupata MATOKEO/ PROJECTION za nchi mbali mbali kuhusu Siasa na Uchumi na hivyo kubashiri wakiwa wamelenga shabaha kabisa/ Accuracy katika ubashiri wao.
Kulingana na Tafiti na Chambuzi zake za hivi karibuni zinazohusu uchaguzi wa Tanzania wa mwaka ujao wa 2020,
Rais Magufuli anategemewa kuchaguliwa tena kwa kura nyingi sana kuliko uchaguzi uliopita wa mwaka 2015.
Tafiti zao zinaonyesha pia kuwa, chama cha CCM kitachukua viti vingi sana vya UBUNGE na hivyo kuvinyima vyama vya upinzani nafasi nyingi za UBUNGE.
Tafiti zinasema pamoja na kuwa vyama vya upinzani vimejaribu sana bado CCM itapata ushindi mkubwa sana na hivyo kuifanya Tanzania kubaki nchi iliyo na Stability/AMANI kwa miaka mingi ijayo.
Chanzo: IEU.