Taasisi ya Urais iheshimiwe

Hivi unaanzaje hata kufikiria kumtukana Rais?

Tukubaliane kutokukubaliana na kutafuta njia muafaka kuaddress tofauti bila kuutusi Urais na kumtusi Rais
Wee Freema acha kutoa Aibu..yeye huwa anasemaje
 
Vijana wa lumumba jengeni hoja acheni vioja vya kutisha watu
 
Wewe ni nani? Mmmm acha kujipendekeza nafasi zimejaa za ma dc
 
Ben Saanane amegundua namna pekee ya kuthaminiwa ndani ya Chadema ni kuwashambulia viongozi wa chama tawala na serikali. Alikosa nafasi ya kugombea ubunge jimbo la Rombo kwa sababu hakuwa akifanya hivyo. Sasa anajiandaa kukubalika. Ni mtu hatari sana kwa sasa, ni mfedheheshaji mkubwa sana wa viongozi wa serikali.
 
Cadema hata uwe malaika watakutukana tu,ndio sera yao,ndio walivyolelewa,ila magufuli akijiunga Chadema hata leo atapambwa kama sio yeye,hao ndio Chadema
 
Rais amemtukana nani?
 
Ok umesikika subiria nafasi yako ya uteuzi
 
Hivi unaanzaje hata kufikiria kumtukana Rais?

Tukubaliane kutokukubaliana na kutafuta njia muafaka kuaddress tofauti bila kuutusi Urais na kumtusi Rais
Pia rais achunge kauli zake za dharau,kiburi na kudharirisha watu.hakuna mtu atakaye mtusi.JENGA HESHIMA UHESHIMIWE.rais tunataka atuunganishe bila ubaguzi na sio kututenganisha kisa tofauti zetu za kisiasa.kwa vile kuna vyama vingi lazima atambue tofauti za kimtizamo juu yake.aheshimu wote na wananchi watampa heshima kama kiongozi wao.
 

1. Isipojiheshimu yenyewe unategemea iheshimiwe vipi na watu wengine?

2. Na nadhani wewe na wenzako ndiyo mna matatizo kwa kushindwa kutofautisha KUKOSOA na KUTUSI. Kwenu kukosoa mnakupa tafsiri ya kutukana na huu ndiyo ugonjwa mbaya unaoisumbua serikali ya awamu hii na mashabiki wake kama wewe!!
 
Ukweli tz kuna kushuka sana kwa maadili. Sheri ichukue mkondo wake kwa wanaomdharau rais.
 
Nadhani hapa Tulipofika watanzania tunahitaji zaidi Viongozi wanaotuunganisha badala ya kuwa na viongozi wanaotugawa kwa kauli zao. Pande zote hivi sasa zina matatizo ya matamshi toka kwa viongozi hasa wa ngazi za juu. sasa sijui nani amfunge 'paka' kengele. Ushabiki unaofanywa na wale wanaojiita UVCCM na BAVICHA dhidi ya kauli ovu zinazotolewa na viongozi wao dhidi ya wengine ni kielelezo tosha kuwa jamii imepotoka hivyo tunahitaji wa kuturudisha kwenye Mstari. Wale ambao wenye uwezo wa kuwaambia viongozi wetu hapa unakosea mzee hawapo maana nguzo yetu imeliwa na mchwa nayo ilikuwa Baba wa taifa pekee. Tumlilie nani?
 

Labda Mh. Rais Amekuwa Mpole Sana!!
 
Unataka kuwafanya watu wengine hawajui maana ya kukosoa na kutukana? Unakosoa kwa kutumia maneno ya kejeli na matusi?
 
Huyu sio jk nawaambia mtapata matatizo sana kwa akili hizi za mkumbo.
Tafsiri ipi uliyonayo juu ya kujiheshimu, kuna siku yoyote raisi katukana mtu kwa tusi la mdomo au ishara ya dole la kati???
 
Wewe siyo mwana CCM.
 
Huyu sio jk nawaambia mtapata matatizo sana kwa akili hizi za mkumbo.

Tafsiri ipi uliyonayo juu ya kujiheshimu, kuna siku yoyote raisi katukana mtu kwa tusi la mdomo au ishara ya dole la kati???
Lol!
 


Onesha contents za matusi za huyo Ben saanane , maana mwisho wa siku huwa mnakurupuka kwenda mahakamani mkiwa hakuna ushahidi

Mbona wanaomchukia wako wengi sana babu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…