Taasisi na Jumuiya zapewa siku 15 kuhuisha taarifa zao kwa Msajili

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,279
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imesema itazifutia leseni Jumuiya na Taasisi ambazo zitashindwa kuwasilisha vyeti, katiba na kanuni za uendeshaji katika ofisi za msajili ndani ya siku 15 kuanzia Novemba 15.

Hayo yamebainishwa Novemba 15, 2021 Msajili wa Jumuiya, Emmenuel Kihampa wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kuanza kwa shughuli ya kuhuisha taarifa zao ambayo imeanza Novemba 15 katika Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kwa kuanzia Mkoa wa Mbeya

Amesema kuwa lengo la zoezi hilo nchini kutambua idadi ya Jumuiya zisizo za kidini na kidini huku akieleza mikoa ya Mbeya na Songwe ni vinara wa kuwa Jumuiya nyingi ambazo hazijasajiliw

''Jumuiya zote zinatakiwa kuhuisha taarifa zao kwa ofisi za msajili lengo ni kuzitambua na ziwe chini ya Serikali ili kuepusha migogoro itokanayo na matumizi mabaya ya fedha kwa viongozi wachache kwa maslahi yao binafsi badala ya kuwanufaisha wanachama ''amesema


Mwananchi
 
Back
Top Bottom