Taasisi ipi nzuri kwa huduma za Kifedha hapa Tanzania?

philipo njovu

Senior Member
Dec 30, 2016
173
107
Mambo ni vipi majamaa. Kitambo kidogo ila tu wazima. Wenzangu wa 2016 mpo active kweli? Hahaha

Nawasalimu kwa jina la Muungano wa Tanzania.. niajeee..

Ebhana eh, katika pitapita zangu hapa na pale katika machapisho ya Google.. nikaona topic kuhusu matumizi ya huduma za Kifedha (Bank/Benki) na swala zima la kupata faida kadri utakavyoweka pesa yako kutokana na mzunguko wa riba. Ni kwa upande kwa NBC. Sasa nikaona ni wakati mzuri ikiwa kama kijana Mzawa wa Tanzania. Ninae miliki kitambulisho cha NIDA na kadi ya mpiga kura.. nijisogeze nikapate KADI ya Benki.

Lakini kilichofanya nije hapa ni kuhusu kuhitaji ufafanuzi wa zaidi, kama kuna huduma nzuri na isiyokuwa na longolongo kutoka kwa kampuni nyingine za kibenki ili niweze kuchanganua ipi itafaa na ipi itakuwa ngumu kuweza kustahimili kipato changu haswa siku nikiwa sina

Natumaini wapo wanaotumia huduma hizo.

Nipeni elimu wakuu.
 
Back
Top Bottom