Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,673
- 149,858
Hili ndio swali ninalojiuliza maana makampuni haya bila shaka yatakuwa yanalipa kodi katika serikali zao na ili yalipe kodi stahiki ni lazima yaonyeshe mahesabu yao na mahesabu haya ni lazima yatategemea data za makanikia wanazopokea kutoka nchi mbalimbali duniani.
Isitoshe,ACASIA wanaweza kutudanganya sisi huku kuhusu viwango vya madini vilivyomo katika mchanga wa dhahabu lakini kamwe hawawezi kudanganya makampuni yanayochengua huu mchanga hivyo ni wazi makampuni haya ya kuchengua mchanga yatakuwa na data au picha sahihi kuhusu kiwango cha madini katika huu mchanga.
Na kama makampuni haya yatakuwa yanashirikiana na ACASIA kuficha ukweli,ina maana serikali za nchi yaliyoko makampuni haya na zenyewe zitakuwa zinashirika udanganyifu huu huku zenyewe zikipata kodi halali au na hizi serikali nazo zinaibiwa kodi yake?
Kwakuwa kamati ya uchunguzi ilikuwa imepewa uwezo wa kuongeza habibu za rejea kama kamati ingeona kuna umuhumi wa kufanya hivyo,ni kwanini kamati hii haikuona umuhimu wa kusafiri mpaka katika viwanda vinavyotumika kuchengua mchanga huu ili kujaribu kuoanisha taarifa yao na taarifa zilizoko katika viwanda hivi?
Tukumbuke kamati ya kuchunguza sakata la Richmond ilisafiri mpaka Marekani kwenda kutafuta ukweli saa sijui kwanini hii kamati haikutoka nje ya nchi kutafuta taarifa zaidi.
Msingi wa maswali haya ni kutokana na ukweli kuwa kutokana na tofauti kubwa ya viwango vya madini vilivyotajwa na kamati kulinganisha na viwango vinavyotajwa na ACASIA /TMAA,ni lazima tofauti hii ingekuwa reflected japo kwa kiasi fulani katika taarifa za makampuni/viwanda vya kuchengua huu mchanga.
Ni wazi pia makampuni haya yanapokea mchanga kutoka nchj nyingine duniani hivyo ungefanyika ulinganifu ni wazi clue ya wizi, kama upo, ingeonekana tu.
Chukulia mfano wa kukoboa mahindi au mpunga ambapo kwa uzoefu mtu unajua kabisa nikikoboa magunia kadhaa ya mpunga au mahindi basi sitakosa magunia kadhaa ya mchele/mahindi ya kukoboa.
Na kwa vyovyote vile ni wazi baada ya uchenguji kufanyika,lazima kutakuwa na records kuwa tarehe fulani mchanga kiasi fulani kutoka kampuni fulani ulichenguliwa na yakapatikana madini kadhaa na kila kiwango cha madini kilichopatikana kikiwa kimerekodiwa.
Najua mchanga wa dhahabu na magunia ya mahindi au mpunga ni vitu tofauti lakini bado naamini clue ingepatikana tu hasa kama wangelinganisha taarifa za kiwango cha makontena ya mchanga kutoka nchi zingine na estimste za madini yaliyomo katika makontena hayo kabla na baada ya uchenguaji.