Taarifa za kukanusha tuhuma za audio inayosambazwa ikumhusu Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe

Status
Not open for further replies.

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
38,325
2,000
TAARIFA

Ninazo audios zaidi ya tano tofauti tofauti ambazo zilirekodiwa wakati wa zoezi la kutunga propaganda ya kumchafua mwenyekiti wa CHADEMA Mhe. Mbowe, kwa kuigiza sauti yake ionekane kwamba amezungumza na msanii Wema. Tayari wanaohisiwa kufanya zoezi hili ovu wanafanyiwa uchunguzi wa kina na watawekwa hadharani ushahidi utakapokamilika.

Audios hizo, ilikuwa inatafutwa moja ambayo imepatiwa vizuri sauti zake, na moja ambayo waliobuni upuzi huo walipoiona inafaa, haraka haraka wakaisambaza kwenye mitandao ya kijamii hususan WhatsApp, na kuifanya kuwa habari.

Hivi sasa watanzania wameungana na wanachama na wapenzi wa CHADEMA nchi nzima kuomboleza msiba mzito wa mmoja wa waasisi wa CHADEMA Hayati Dkt Philemon Ndesamburo, watawala wamechukizwa na namna CHADEMA inavyoendelea kuungwa mkono na mamilioni ya watanzania, hivyo wanatafuta kila njia ya kuichafua CHADEMA na viongozi wake.

Historia ya muda mfupi uliopita imeonesha namna Mhe. Mbowe alivyopigwa vita na serikali hii ya CCM, ikiwa ni pamoja na kughushiwa madai ya kodi, kubughudhiwa kwenye shughuli zake za kilimo, kuhusishwa na uzushi wa madawa ya kulevya, kufungiwa hotels zake na kunyang'anywa majengo yake, n.k.

Hivi sasa, watawala (CCM) wanachokifanya, ni kukabiliana kwa kila namna na kwa gharama yoyote ile, kukabiliana na utekelezaji wa maazimio ya baraza kuu la chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA, yaliyoafikiwa kwa sauti moja na wajumbe wa baraza hilo mjini Dodoma, na kuungwa mkono na mamilioni ya watanzania.

Wanachama wa CHADEMA, wapenzi na wadau wa demokrasia nchini na wananchi wote, kwanza nawaomba na kuwasihi mzipuuze audios hizo zinazoendelea kusambazwa, kwani zina nia ovu kujaribu kuingilia kati shughuli nzima ya maandalizi ya kumuaga na kumpa heshima zote mzee wetu Ndesamburo, na kumchafua kiongozi wa upinzani nchini, ambaye amekuwa na heshima ndani na nje ya nchi.

Nimelazimika kutoa taarifa hii kama hatua ya kutoa ufafanuzi kwa wadau mbalimbali walioniuliza kuhusu upuzi huo, hivyo, nawashauri kuupuuza na kuendelea na masuala mengine ya muhimu, likiwepo kuendelea na maandalizi ya kumuaga na kumpumzisha mzee wetu Ndesamburo, na kujiandaa kikamilifu kutekeleza maazimio ya baraza kuu la CHADEMA, ikiwepo kupinga Udikteta Uchwara unaoendelea kuchipua nchini.

==
Tuhuma za uwongo
Freeman Mbowe na Wema Sepetu ndani ya penzi zito

------------------------------------
Kama tumeamua kuruhusu mambo binafsi yanayovuja yawe hewani basi ni vizuri ila tu tuwe wavumilivu na tusiangalia cheo cha mti ili hata upande wa pili ukiguswa tusione upendeleo wa kuondoa haraka kilichopostiwa.

Mimi sina shida na hili jambo kuanikwa ila nachukia unafiki wa kuangalia cheo cha mtu.

Ni vizuri tukawajua wanasiasa wetu ila tutende haki bila kujali wadhifa wala madaraka ya mtu.

Haya mambo yanawezekana kwa nchi za wenzetu tu waliokomaa kisiasa lakini sio huku kwetu.Sisi tunapenda kuanzisha mambo ambayo sisi wenyewe hatuwezi kuyavumilia.

Kwenye haya mambo sijui nani msafi kiasi cha kuweza kuanika ya mwenzake na yeye akabaki salama kwamba hajihusishi nayo.
 
Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
21,266
2,000
Kama tumeamua kuruhusu mambo binafsi yanayovuja yawe hewani basi ni vizuri ila tu tuwe wavumilivu na tusiangalia cheo cha mti ili hata upande wa pili ukiguswa tusione upendeleo wa kuondoa haraka kilichopostiwa.

Mimi sina shida na hili jambo kuanikwa ila nachukia unafiki wa kuangalia cheo cha mtu.

Ni vizuri tukawajua wanasiasa wetu ila tutende haki bila kujali wadhifa wala madaraka ya mtu.

Mkiwa waungwana hata huu uzi hamtautoa na kama ni kuutoa au kuhamishwa jukwaa basi muanze na hiyo clip maana nayo hili jukwaa sio sehemu yake otherwise tutahisi kuna jambo nyuma ya pazia.

Mbowe siyo Kiongozi wa nchi hivyo hoja yako haina mshiko, na kama ulitaka kumfananisha Mbowe na Raisi wa nchi unaweza kufanya hivyo halafu tofauti utaiona kwa kitakachokupata, umemsahau chadema mwenzenu Ze Utamu? Yuko wapi leo hii, tena hakuwa anaishi Tanzania lkn nguvu ya Dola ilimfikia, sikio halizidi kichwa tunasema Waswahili!
 
ISIS

JF-Expert Member
Apr 20, 2016
91,521

Preach!
 
kopites

JF-Expert Member
Jan 28, 2015
5,716

Yaaani mnahangaika mpk kuigiza sauti?acheni hizo bana.
 
Msengapavi

JF-Expert Member
Oct 23, 2008
8,250
2,000
Mbowe siyo Kiongozi wa nchi hivyo hoja yako haina mshiko, na kama ulitaka kumfananisha Mbowe na Raisi wa nchi unaweza kufanya hivyo halafu tofauti utaiona kwa kitakachokupata, umemsahau chadema mwenzenu Ze Utamu? Yuko wapi leo hii, tena hakuwa anaishi Tanzania lkn nguvu ya Dola ilimfikia, sikio halizidi kichwa tunasema Waswahili!
 
Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
38,325
2,000
Mbowe Ni KUB Ndio Maana Amepewa Hadi Gari Kwa Hiyo Anatakiwa Aishi Kama Kiongozi Wa Ngazi Ya Juu
Sawa mimi sikatai ila haya mambo tuwaachie wenzetu katika nchi zilizoendelea ambako hakuna doublestandard ya kuangalia wadhifa wa mtu.
 
Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
38,325
2,000
Mbowe siyo Kiongozi wa nchi hivyo hoja yako haina mshiko, na kama ulitaka kumfananisha Mbowe na Raisi wa nchi unaweza kufanya hivyo halafu tofauti utaiona kwa kitakachokupata, umemsahau chadema mwenzenu Ze Utamu? Yuko wapi leo hii, tena hakuwa anaishi Tanzania lkn nguvu ya Dola ilimfikia, sikio halizidi kichwa tunasema Waswahili!
Haya kaangalien sasai jinsi yule dada maarufu alivyojibu ndio muone hatari ya haya mambo mnayoyaanzisha.
 
Status
Not open for further replies.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom