Taarifa za kukanusha tuhuma za audio inayosambazwa ikumhusu Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe

Status
Not open for further replies.
TAARIFA

Ninazo audios zaidi ya tano tofauti tofauti ambazo zilirekodiwa wakati wa zoezi la kutunga propaganda ya kumchafua mwenyekiti wa CHADEMA Mhe. Mbowe, kwa kuigiza sauti yake ionekane kwamba amezungumza na msanii Wema. Tayari wanaohisiwa kufanya zoezi hili ovu wanafanyiwa uchunguzi wa kina na watawekwa hadharani ushahidi utakapokamilika.

Audios hizo, ilikuwa inatafutwa moja ambayo imepatiwa vizuri sauti zake, na moja ambayo waliobuni upuzi huo walipoiona inafaa, haraka haraka wakaisambaza kwenye mitandao ya kijamii hususan WhatsApp, na kuifanya kuwa habari.

Hivi sasa watanzania wameungana na wanachama na wapenzi wa CHADEMA nchi nzima kuomboleza msiba mzito wa mmoja wa waasisi wa CHADEMA Hayati Dkt Philemon Ndesamburo, watawala wamechukizwa na namna CHADEMA inavyoendelea kuungwa mkono na mamilioni ya watanzania, hivyo wanatafuta kila njia ya kuichafua CHADEMA na viongozi wake.

Historia ya muda mfupi uliopita imeonesha namna Mhe. Mbowe alivyopigwa vita na serikali hii ya CCM, ikiwa ni pamoja na kughushiwa madai ya kodi, kubughudhiwa kwenye shughuli zake za kilimo, kuhusishwa na uzushi wa madawa ya kulevya, kufungiwa hotels zake na kunyang'anywa majengo yake, n.k.

Hivi sasa, watawala (CCM) wanachokifanya, ni kukabiliana kwa kila namna na kwa gharama yoyote ile, kukabiliana na utekelezaji wa maazimio ya baraza kuu la chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA, yaliyoafikiwa kwa sauti moja na wajumbe wa baraza hilo mjini Dodoma, na kuungwa mkono na mamilioni ya watanzania.

Wanachama wa CHADEMA, wapenzi na wadau wa demokrasia nchini na wananchi wote, kwanza nawaomba na kuwasihi mzipuuze audios hizo zinazoendelea kusambazwa, kwani zina nia ovu kujaribu kuingilia kati shughuli nzima ya maandalizi ya kumuaga na kumpa heshima zote mzee wetu Ndesamburo, na kumchafua kiongozi wa upinzani nchini, ambaye amekuwa na heshima ndani na nje ya nchi.

Nimelazimika kutoa taarifa hii kama hatua ya kutoa ufafanuzi kwa wadau mbalimbali walioniuliza kuhusu upuzi huo, hivyo, nawashauri kuupuuza na kuendelea na masuala mengine ya muhimu, likiwepo kuendelea na maandalizi ya kumuaga na kumpumzisha mzee wetu Ndesamburo, na kujiandaa kikamilifu kutekeleza maazimio ya baraza kuu la CHADEMA, ikiwepo kupinga Udikteta Uchwara unaoendelea kuchipua nchini.

===================
Tuhuma za uwongo
Freeman Mbowe na Wema Sepetu ndani ya penzi zito
 
Ingawa wanasema kuwa alichokizungumza rais ama kukitaka rais wa Tanzania hakipingwi na mtanzania yeyote yule lakini kwa hili la mama Anna Mughwira kuteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro asipolipinga kwa kutumia busara zake basi atakuwa amekosa uelewa.

Mama Anna Mughwira ni mwenyekiti wa chama cha upinzani tena anaielewa vyema sana katiba ya CCM ya mwaka 1977. Anajua kuwa kwenye hiyo katiba kuna kipengele kinachosema wazi kuwa mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya ni ni wanachama wa chama hicho cha CCM. Pia wanatakiwa kushiriki shughuli za kisiasa za CCM na jukumu lao kubwa ni kusimamia na kuhakikisha ilani ya CCM inatekelezwa. Sasa nasubiri kuona huyu mama ataamua nini?

Akumbuke kuwa yeye ni mwenyekiti wa taifa wa chama cha upinzani ambacho kinakosoa sera za CCM. Akumbuke pia kuwa hakubaliani na Mwenge wa Uhuru, je ukifika Kilimanjaro ataupokea, kuuhubiri na hatimaye kuukimbiza?

Labda Zitto atuambie kuwa sasa ACT imejibinafsisha rasmi kwa CCM na ni moja tu ya matawi yake kisiasa.

Pengine sitashangaa kuona harakaharaka mama Anna akajiuzulu uenyekiti wa ACT Wazalendo na kujitoa ndani ya chama hicho na haraka haraka akahamia CCM ili kuutendea haki ulaji mpya aliopewa. Ndiyo aina ya wapinzani wengi tulionao.

Pia nitashangaa sana kuona kama wana CCM watapongeza hili na kupiga nderemo kama kawaida yao huku wakijua wazi kuwa mwenyekiti wao ameikanyaga waziwazi katiba yao na mbaya zaidi kumpa nafasi mtu ambaye amekuwa akiipinga CCM huku akiwaacha wana CCM lukuki waliokifia chama kwa muda mrefu. Wana CCM wengi ni wanafiki sana na watu wa ndiyo mzee. Ukitafuta ambao siyo wanafiki kwelikweli sidhani kama utampata zaidi ya walau Hussein Bashe. Ukiwa na kiongozi ambaye haheshimu hata katiba ya chama chake tu basi huyo ni kiongozi asiye na weledi. Kusigina katiba ya nchi kunaanzia kuchezea ya chama, kwakuwa tu huwezi kupingwa siyo busara kuamua tu kila unachoona kuwa kinakufaa wewe. Miiko ni lazima izingatiwe kwa kila jambo.

Haya mama Mghwira, nenda katekeleze na kuitetea ilani ya CCM ambayo wewe uliipinga kwenye uchaguzi mkuu. Pia uwe tayari kupangiwa majukumu ya kikazi na mwenyekiti mwenzako wa chama cha siasa.Pia wale wapinzani wanaoipinga ilani ya chama unachotumikia sasa uviamuru vyombo vya dola vipambane nao.
Mimi ninachojiuliza ni kuwa sasa mwenyekiti wa CCM ambaye ni boss wako amekataza mikutano na shughuli za kisiasa na wewe ambaye ni mwenyekiti mwingine wa chama cha upinzani unalipinga hili kwa kuwa linadumaza waziwazi mwamko wa kisiasa na kupelekea ugumu wa kujulikana kwa vyama vipya kama hicho cha ACT Wazalendo ambacho wewe ndiye kamanda wao mkuu. Haya mama nenda katekeleze ilani ya CCM ambayo wewe uliipinga na ukaamua kuja na ilani nyingine uliyoona kuwa inafaa kuliko hiyo ya CCM. Kazi njema kwenye kuijenga CCM mkoa wa Kilimanjaro na kuisimamia vyema ilani hiyo ili kuleta matumaini ya wananchi kwa CCM na kuwafanya wasione umuhimu wa vyama vingine ikiwemo ACT Wazalendo maana ukifanya vyema wataona kuwa "CCM yatosha"

Au na nyie ACT Wazalendo mtuambie ukweli kuwa na nyie ni "reserved bench" la serikali ya rais Magufuli,kwamba akitaka anafanya tu sub na kumchomoa anayemtaka huko ACT ili aitumikie serikali. Chama cha siasa kukubali watu wake muhimu kutumiwa tumiwa tu kwa kadiri ya uwezo wa mtumiaji huku chama hicho kikijidai kuwa kinafanya kila njia ili siku moja kitwae dola ni ujinga!

Tusubiri tuone hili ingizo jipya sokoni.
 
Attachments

  • VID-20170405-WA0002.mp4
    6.4 MB · Views: 30
Huyo mtu anayefanya hivyo kwa demage aliyoisababisha sidhani kama wakucheleweshwa asiwekwe hadharani
 
TAARIFA

Ninazo audios zaidi ya tano tofauti tofauti ambazo zilirekodiwa wakati wa zoezi la kutunga propaganda ya kumchafua mwenyekiti wa CHADEMA Mhe. Mbowe, kwa kuigiza sauti yake ionekane kwamba amezungumza na msanii Wema. Tayari wanaohisiwa kufanya zoezi hili ovu wanafanyiwa uchunguzi wa kina na watawekwa hadharani ushahidi utakapokamilika.

Audios hizo, ilikuwa inatafutwa moja ambayo imepatiwa vizuri sauti zake, na moja ambayo waliobuni upuzi huo walipoiona inafaa, haraka haraka wakaisambaza kwenye mitandao ya kijamii hususan WhatsApp, na kuifanya kuwa habari.

Hivi sasa watanzania wameungana na wanachama na wapenzi wa CHADEMA nchi nzima kuomboleza msiba mzito wa mmoja wa waasisi wa CHADEMA Hayati Dkt Philemon Ndesamburo, watawala wamechukizwa na namna CHADEMA inavyoendelea kuungwa mkono na mamilioni ya watanzania, hivyo wanatafuta kila njia ya kuichafua CHADEMA na viongozi wake.

Historia ya muda mfupi uliopita imeonesha namna Mhe. Mbowe alivyopigwa vita na serikali hii ya CCM, ikiwa ni pamoja na kughushiwa madai ya kodi, kubughudhiwa kwenye shughuli zake za kilimo, kuhusishwa na uzushi wa madawa ya kulevya, kufungiwa hotels zake na kunyang'anywa majengo yake, n.k.

Hivi sasa, watawala (CCM) wanachokifanya, ni kukabiliana kwa kila namna na kwa gharama yoyote ile, kukabiliana na utekelezaji wa maazimio ya baraza kuu la chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA, yaliyoafikiwa kwa sauti moja na wajumbe wa baraza hilo mjini Dodoma, na kuungwa mkono na mamilioni ya watanzania.

Wanachama wa CHADEMA, wapenzi na wadau wa demokrasia nchini na wananchi wote, kwanza nawaomba na kuwasihi mzipuuze audios hizo zinazoendelea kusambazwa, kwani zina nia ovu kujaribu kuingilia kati shughuli nzima ya maandalizi ya kumuaga na kumpa heshima zote mzee wetu Ndesamburo, na kumchafua kiongozi wa upinzani nchini, ambaye amekuwa na heshima ndani na nje ya nchi.

Nimelazimika kutoa taarifa hii kama hatua ya kutoa ufafanuzi kwa wadau mbalimbali walioniuliza kuhusu upuzi huo, hivyo, nawashauri kuupuuza na kuendelea na masuala mengine ya muhimu, likiwepo kuendelea na maandalizi ya kumuaga na kumpumzisha mzee wetu Ndesamburo, na kujiandaa kikamilifu kutekeleza maazimio ya baraza kuu la CHADEMA, ikiwepo kupinga Udikteta Uchwara unaoendelea kuchipua nchini.

===================
Tuhuma za uwongo
Freeman Mbowe na Wema Sepetu ndani ya penzi zito
Anayekanusha ni nani?
Kwa nini Mbowe asiitishe Press kukanusha tuhuma hii?
 
Zitume hizo tano tuamin, otherwise tutaendelea kuamin iliyopo. Ila kiukweli Mwanaume kwa mwanamke ni kama mfupa kwa fisi. Au nzi kwenye kidonda yupo radhi afie hapo hapo.

Mtu wa aina na kaliba ya mbowe alipaswa achukue tahadhali katika kila ovu analofanya sio kwa kujianika ivi.

Inapaswa achukue hatua.
 
Zote hizi ni sihasa mapenzi siasa, kazi siasa, democrasia siasa, maendeleo siasa anyway taarifa nyingine wala hazihitajiki kusomwa Kwa maana tunazidi kusambaza hizo information
 
"Sioni haja ya kumchafua mtu kwa jambo asilolitenda, wanao fanya hivyo inabidi wachunguzwe akili zao inwezekana hazifanyi kazi na wanafwata upepo"
 
hata yale mauwaji ya Arusha ilisemwa kuna mkanda na ushahidi wa kutosha

vipi mpaka leo?

hata hivyo sio jambo la ajabu kwa mwanaume kuwa na michepuko kwani kuwa mwenyekiti wa chama

unapoteza urijali wako? Mbowe tafuna vyombo kadri uwezavyo.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom