Taarifa za habari Tv za kibongo

Taarifa za habari Tv za kibongo

magnifico

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2013
Posts
13,277
Reaction score
31,857
Nimeikuta Bongo5.com

Habari nyingi kwenye TV za kibongo hazina mvuto. Unaweza kufurahia kuangalia habari labda kama siku hiyo kuna ajali kubwa imetokea, bungeni kumeumana ama siku Barack Obama akirudi tena Bongo. Kusipokuwa na matukio ya kuvutia yaliyopo tayari, taarifa za habari kwenye TV zetu zinaboa si kidogo.
Watakujazia habari za mikutano, semina, warsha na mikutano na waandishi wa habari ambazo hazivutii hata chembe. Zinaweza kuwa na vigezo vya kuitwa ‘news’ lakini hizi si habari unazoweza kuziona kwenye TV za watu wanaojielewa. Hizi ni habari za kupoteza muda tu na wala hazina ‘impact’ yoyote kwa wananchi.
Nafahamu mazingira ya kufanya kazi kwenye TV za Tanzania na ninalo jibu la uhakika la kwanini habari za semina, warsha au press conference ndizo zinazotawala line-up ya habari kwenye vituo vyetu. Sababu kubwa ni kwamba waandishi wengi wa habari wanalipwa ujira mdogo mno na hivyo ili kujikimu kimaisha inabidi wafanye zaidi story za warsha na mikutano ambazo huwapa posho za hapa na pale.
Hiyo ina maana kuwa waandishi wengi wa habari hawana muda wa kuandika habari za kuvutia zinazohitaji ubunifu zaidi, muda wa kutosha na ‘mnuso wa habari’ (nose for news). Wamiliki wa vyombo vya habari wanahitaji kuwekeza zaidi katika kuwalipa vizuri waandishi wanaokusanya habari zao, kuwa na usafiri wa kuaminika na kuwa na wahariri wabunifu wenye uwezo wa kujua habari zenye mvuto, zenye impact na zilizoandikwa kwa kina.
Taarifa za habari pia zinatakiwa kuhusisha wataalam ama wachambuzi wa masuala mbalimbali kutilia mkazo ripoti husika. Mashirika makubwa ya habari ya kimataifa hupenda kutumiza ‘contributors’ mbalimbali ambao huhusika katika uchambuzi wa masuala ya siasa, biashara na uchumi, masuala ya jamii pamoja na michezo na burudani.
Kwa kutumia watu hawa, habari hupanuliwa zaidi na kuzungumzwa katika mtazamo mpana.
Kwa mfano, weekend hii Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, amedai kuwa bara la Afrika halimtendei haki Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kama mtu muhimu kwenye harakati za ukombozi wa Afrika kutoka kwa wakoloni. Hii ni habari ambayo inaweza kuripotiwa kwenye taarifa za habari katika TV za Tanzania kwa kuichambua zaidi kwa kuhusisha wazee na viongozi wa zamani watakaotoa maoni yao kutokana na kauli hii, viongozi wa juu wa Tanzania na hata wasomi wa vyuo vikuu kuipa wigo zaidi.
Kwa ufupi, matatizo makubwa kwenye taarifa za habari kwenye vituo vyetu vya runinga ni pamoja na:
Habari nyingi hazivutii
Wasomaji wengi wa habari hawana mvuto na hawavalishwi vizuri
Muonekano na uwasilishaji wa habari ni wa kawaida
Hakuna habari za kina na zenye uchambuzi
Habari si za kutafuta, nyingi ni za matukio ya kuandaliwa
Hakuna matumizi ya wataalam katika fani mbalimbali
Uandishi wa script hautumii maneno yenye kuvuta usikivu wa watu au matumizi ya lugha ya macho
Matumizi ya ripota wanaotumia simu za mkononi
Wasomaji wa habari hawategenezwi kuwa ‘TV personalities’ kama ilivyo Kenya ambako wamezaliwa watu maarufu na wenye ushawishi wakiwemo Julie Gichuru, Kanze Dena na Lulu Hassan au Swaleh Mdoe wa Citizen TV au Larry Madowo wa NTV na wengine
Habari zinakuwa serious mno na kusahau upande wa ‘humor’
Uandishi wa habari unachukuliwa kama taaluma kupitiliza na kusahau kuwa uandishi pia ni sanaa inayohitaji ubunifu kama uandishi wa vitabu au utunzi wa mashairi yenye mvuto
Waandishi wa habari na maripota wa TV ambao wako chini ya wahariri, wanatakiwa kuanza kufikiria nje ya box na kutafuta habari za maana na kuondokana na uandishi uliozoeleka wa‘Madiwani wa kata ya ‘Mti Mkavu’ wametakiwa kuwa waadilifu katika kazi yao’ ‘Ama mbunge wa Kilimabubu ameweka jiwe la msingi kwenye shule ya Mnazi Mchungu’.
Watazame aina ya habari wenzetu huziandika ambazo huwa na mvuto, zimechambuliwa vizuri, zimetumia vyanzo vya kutosha na uandishi wa script wenye maneno matamu.
 
Kula likes nyingi kaka. nitarudi kutoa mchango.
 
ni kweli habari nyingi za vituo vya Tv hazivutii sijui hawajifunzi sehemu nyingine wanafanyaje
 
hapo umeongea mtoa mada, wanatilia shaka sana taaluma yao
 
Nimeikuta Bongo5.com

Habari nyingi kwenye TV za kibongo hazina mvuto. Unaweza kufurahia kuangalia habari labda kama siku hiyo kuna ajali kubwa imetokea, bungeni kumeumana ama siku Barack Obama akirudi tena Bongo. Kusipokuwa na matukio ya kuvutia yaliyopo tayari, taarifa za habari kwenye TV zetu zinaboa si kidogo.
Watakujazia habari za mikutano, semina, warsha na mikutano na waandishi wa habari ambazo hazivutii hata chembe. Zinaweza kuwa na vigezo vya kuitwa ‘news' lakini hizi si habari unazoweza kuziona kwenye TV za watu wanaojielewa. Hizi ni habari za kupoteza muda tu na wala hazina ‘impact' yoyote kwa wananchi.
Nafahamu mazingira ya kufanya kazi kwenye TV za Tanzania na ninalo jibu la uhakika la kwanini habari za semina, warsha au press conference ndizo zinazotawala line-up ya habari kwenye vituo vyetu. Sababu kubwa ni kwamba waandishi wengi wa habari wanalipwa ujira mdogo mno na hivyo ili kujikimu kimaisha inabidi wafanye zaidi story za warsha na mikutano ambazo huwapa posho za hapa na pale.
Hiyo ina maana kuwa waandishi wengi wa habari hawana muda wa kuandika habari za kuvutia zinazohitaji ubunifu zaidi, muda wa kutosha na ‘mnuso wa habari' (nose for news). Wamiliki wa vyombo vya habari wanahitaji kuwekeza zaidi katika kuwalipa vizuri waandishi wanaokusanya habari zao, kuwa na usafiri wa kuaminika na kuwa na wahariri wabunifu wenye uwezo wa kujua habari zenye mvuto, zenye impact na zilizoandikwa kwa kina.
Taarifa za habari pia zinatakiwa kuhusisha wataalam ama wachambuzi wa masuala mbalimbali kutilia mkazo ripoti husika. Mashirika makubwa ya habari ya kimataifa hupenda kutumiza ‘contributors' mbalimbali ambao huhusika katika uchambuzi wa masuala ya siasa, biashara na uchumi, masuala ya jamii pamoja na michezo na burudani.
Kwa kutumia watu hawa, habari hupanuliwa zaidi na kuzungumzwa katika mtazamo mpana.
Kwa mfano, weekend hii Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, amedai kuwa bara la Afrika halimtendei haki Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kama mtu muhimu kwenye harakati za ukombozi wa Afrika kutoka kwa wakoloni. Hii ni habari ambayo inaweza kuripotiwa kwenye taarifa za habari katika TV za Tanzania kwa kuichambua zaidi kwa kuhusisha wazee na viongozi wa zamani watakaotoa maoni yao kutokana na kauli hii, viongozi wa juu wa Tanzania na hata wasomi wa vyuo vikuu kuipa wigo zaidi.
Kwa ufupi, matatizo makubwa kwenye taarifa za habari kwenye vituo vyetu vya runinga ni pamoja na:
Habari nyingi hazivutii
Wasomaji wengi wa habari hawana mvuto na hawavalishwi vizuri
Muonekano na uwasilishaji wa habari ni wa kawaida
Hakuna habari za kina na zenye uchambuzi
Habari si za kutafuta, nyingi ni za matukio ya kuandaliwa
Hakuna matumizi ya wataalam katika fani mbalimbali
Uandishi wa script hautumii maneno yenye kuvuta usikivu wa watu au matumizi ya lugha ya macho
Matumizi ya ripota wanaotumia simu za mkononi
Wasomaji wa habari hawategenezwi kuwa ‘TV personalities' kama ilivyo Kenya ambako wamezaliwa watu maarufu na wenye ushawishi wakiwemo Julie Gichuru, Kanze Dena na Lulu Hassan au Swaleh Mdoe wa Citizen TV au Larry Madowo wa NTV na wengine
Habari zinakuwa serious mno na kusahau upande wa ‘humor'
Uandishi wa habari unachukuliwa kama taaluma kupitiliza na kusahau kuwa uandishi pia ni sanaa inayohitaji ubunifu kama uandishi wa vitabu au utunzi wa mashairi yenye mvuto
Waandishi wa habari na maripota wa TV ambao wako chini ya wahariri, wanatakiwa kuanza kufikiria nje ya box na kutafuta habari za maana na kuondokana na uandishi uliozoeleka wa‘Madiwani wa kata ya ‘Mti Mkavu' wametakiwa kuwa waadilifu katika kazi yao' ‘Ama mbunge wa Kilimabubu ameweka jiwe la msingi kwenye shule ya Mnazi Mchungu'.
Watazame aina ya habari wenzetu huziandika ambazo huwa na mvuto, zimechambuliwa vizuri, zimetumia vyanzo vya kutosha na uandishi wa script wenye maneno matamu.

Ukweli mtupu!
 
Hakuna habari za uchunguzi. Ukiangalia citizenTV kamwe huwezi kuangalia hii li TVT letu.
 
Hiyo ni kweli kabisa mkuu. Habari za Tanzania hazivutii kabisa harafu hakuna habari ata za uchunguzi.

Jerry muro alijaribu matokeo yake kabla ata ya hukumu tbc walimfukuza kazi .

Baadaye alishinda kesi. Vyombo vya habari haviwaungi mkono waandishi hao ndio maana wameishia kureport semina na mikutano tu sababu wamiliki wa vyombo vya habari uwatelekeza punde wapatapo matatizo
 
Jana kuna mtu alikuwa ananieleza habari za ajali ya Morogoro......nikwambia sijaona kwa vile siangalii TV......akashangaa sana nikmwambia nina miezi sita nadhani sijaangalia taarifa za habari za hapa home. Nilimueleza sioni hasara ya kutoangalia taarifa ya habari...............habari kama muhumu nitaipata hapa JF au other online sources. Kiufupi taarifa za habari za Bongo ni MAJANGA
 
Ni kweli tupu,mimi huwa navutiwa sana taarifa ya habari za citizen tv kutoka kenya,hawa jamaa kusema ukweli huchambua habari kwa kina na mara nyingi huleta wataalam mbali mbali ili kuchambua mada husika.
 
mi ndio mana siku hizi kwa habari zozote zinahusu bongo nimehamishia majeshi kwa jf,vi-blog na youtube.na kwa habari zinahusu east africa kwa ujumla,napenda kutazama bbc swahili ya kina salim kikeke na mzee charles hillary.mitivii ya bongo kichefu chefu.
 
kuwa muelewa. kwanini una-quote maneno yote hayo halafu una-comment maneno 2 tu? tunaotumia simu unatumalizia chaji bure!

Naweza nikawa muelewa lakini nikaonesha kutojali kama nilivofanya hapo juu..hii nayo imekaaje? Jifunze uvumilivu..si kila kitu unasema tu! mambo mengine unakufa na tie shingoni!
 
kuwa muelewa. kwanini una-quote maneno yote hayo halafu una-comment maneno 2 tu? tunaotumia simu unatumalizia chaji bure!

Akiandika maneno mengi ataonekana msaliti, hujui kuwa na huyu ni mhusika no 1 wa hii mada? Unganisha dot.
 
tatizo haliko kwenye TV tu--hata utangazaji wa redio siku hizi umeingiliwa sana na makanjanja. asilimia 90% ya airtime kwenye radio hutawaliwa na miziki ya kibangibangi, kutuma salama, story za blabla, mapenzi, ngono, umbeya na upuuzi mwingine kama huo.
 
Back
Top Bottom