RafikiElimu
Member
- Mar 1, 2013
- 11
- 7
Dear wadau wa JF na watanzania wote kwa ujumla, uongozi wa Taasisi Isiyokuwa ya kiserikali ya RafikiElimu Foundation unapenda kutoa taarifa ya ufafanuzi kuhusu taarifa kadhaa zilizo tolewa dhidi ya taasisi yetu. Siku ya leo, tumesoma taarifa iliyo tolewa na mtumiaji wa mtandao wa Jamii Forums , anayetumia jina la S.N BARRY aliweka uzi wenye kichwa " RafikiElimu matapeli, poleni wote mliotapeliwa ", uzi huu unasomeka hivi :
" Taasisi kupitia blog yake www.rafikielimu.blogspot.com ilitangaza nafasi za masomo kwa kozi ya NGO MANAGEMENT, watu wamechukua fomu na kulipa ada ya maombi 12000 na ada ya mafunzo 135000 kupitia crdb, wao walisema ofisi zao zipo changanyikeni opp. na chuo cha takwimu lakini watu walipoenda walikuta ofisi ilifungwa siku nyingi na masomo ilibidi waanze ja 14/01/2013 na pesa wameshalipa kupitia benki, poleni mliotapeliwa akiwemo mdogo wangu david a.k.a daudi. "
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ielimu-matapeli-poleni-wote-mliotapeliwa.html
Mtoa uzi huyu aliendelea kwa ku comment chini ya uzi wake akisema
" na fremu pale nje ya ofisi yao limeandikwa linapangishwa means jamaa walishafukuzwagaa! "
Sisi kama uongozi wa Taasisi ya RafikiElimu Foundation, tunasema tumefedheheshwa sana na taarifa hizi kwa sababu ni za uzushi na hazina ukweli wowote.
Ni kweli sisi kama taasisi tunatoa mafunzo ya kozi iitwayo " NGO MANAGEMENT & OPERATION". Tumeanza kutoa kozi mwezi January 2013 na mpaka sasa zaidi ya watu 100 wamekwisha soma kozi hii. Kati ya watu 100 waliosoma kozi hii, watu 50 ambao walikuwa enrolled kwenye intake ya kwanza ya mwezi January wapo wanachukua mafunzo kwa njia ya vitendo " Field Training " katika taasisi mbalimbali zisizo kuwa za kiserikali ambazo zinashirikiana na taasisi yetu.
Watu wote walio fanya application, kwenye intake ya mwezi January na kuwa admitted, walisoma kozi hii na hakuna hata mtu mmoja ambaye alitoa hela na hakuweza kusoma. Katika watu wote 50 wa intake ya kwanza, hakuna mtu anaye itwa jina la David kama ambavyo mtoa uzi huyu amedai.
Hoja ya mtoa uzi huyu kwamba : " na fremu pale nje ya ofisi yao limeandikwa linapangishwa means jamaa walishafukuzwagaa! " nayo pia ni dhaifu na haina mashiko. Wakati tunaanza, ofisi yetu ilikuwa kwenye frame, na tulikuwa tumeandika RafikiElimu Foundation, lakini baada ya ofisi kupanuka, tulihamia kwenye ofisi kubwa ambaye ipo ndani ya geti la pembeni kutoka kwenye fremu, kwa hiyo kama kweli mtoa uzi huyu ana uhakika na anacho kizungumza, na kama kweli alikuja hadi kwenye hiyo fremu iliyopangishwa asingeweza kutukosa, kwa sababu tumeweka bango pale linalo elekeza kwamba tumehamia ndani, na kama hiyo haitoshi pembeni ya fremu hiyo kuna ofisi zetu za stationery , kama kweli mtoa uzi huyu ni msomi baada ya kufika na kuona fremu imeandikwa imepangishwa angeuliza basi hata kwenye hiyo stationery au kwenye ofisi yoyote iliyo karibu na fremu hiyo.
ANGALIZO LETU : Tunapaswa kuwa makini sana kabla ya kutoa taarifa zozote mbaya zinazo husu taasisi, kampuni ama watu binafsi. Kabla hujaenda mtandaoni na kuweka taarifa zinazo chafua taasisi fulani, kampuni fulani, ama mtu fulani, unapaswa kuwa na uhakika sana na unacho kieleza kwa sababu taarifa zako zinaweza kuchafua jina la taasisi ama kampuni husika.
Pili; ni taarifa kuhusu kuwepo kwa mtu ama watu walio jaribu kuiba pesa za watu mtandaoni kwa kutumia jina la taasisi yetu. Watu hao walijitangaza kwamba wanatoa nafasi za kazi na watu walio fanya application,waliambiwa wawatumie shilingi elfu tano kwenda namba 0763906931( AMBAYO MBAYA ZAIDI, WAMEISAJILI KWA JINA LA RAFIKIELIMU ). Baada ya kutumiwa pesa hizo humuelekeza mtuma pesa kuja kuripoti katika ofisi z etu kwa ajili ya kupatiwa kazi. Bahati mbaya ama nzuri, hadi sasa tumepata kesi ya mtu mmoja tu kitu ambacho kinaamnisha watu walistukia mchezo mchafu unao fanywa na hawa jamaa. Mpaka sasa tumekwisha ripoti taarifa hii polisi, na tunawasaka wahusika kwa udi na uvumba, na tutawatia mbaroni ndani ya muda mfupi sana kuanzia leo hii. Tumekwisha toa taarifa ya tahadhari kwenye blogu yetu na kwenye blogu nyinginezo. Unaweza kuisoma taarifa hiyo kupitia blogu yetu : RafikiElimu FOUNDATION: TAHADHARI KUHUSU WATU WANAO FANYA UTAPELI MTANDAONI KWA JINA LA TAASISI YA RAFIKI ELIMU.
Mwisho, tunapenda kuwafahamisha ya kwamba, taasisi yetu ipo, ofisi zetu zipo katika eneo la Changanyikeni karibu na Chuo Cha Takwimu. Siku za kazi ni Jumatatu jadi Ijumaa, saa tatu kamili asubuhi hadi saa 9 kamili jioni. Unaweza kuwasiliana nasi kwa simu : 0782405936.
Tunawatakia kila la kehri katika ujenzi wa taifa letu.
Uongozi,
RafikiElimu Foundation.