Taarifa ya kukosekana umeme

Hakuna kitu kinaniudhi kama umeme kuwa unakatwa kila mara,tuliambiwa mitambo ya gas inaunganishwa,baadae ukaendelea kukatwa,leo tena tunaambiwa sijui nini,je jana na juzi cause ya kukosa umeme ilikuwa nini?
 
Kuuliza si ujinga mkuu

kama kina cha maji nalo kumbe ni tatizo,kwanini hawakusema?,bali wakadanganya kuwa wanaunga gesi na baada ya hapo tatizo litaisha.

hii pattern inafanana na ya 2008 ambapo hali ilikuwa hivihivi,kumbe watu wanatafuta namna ya kuingiza richmond.

na sasa unajionea tena umeme unatumika kufikia malengo fulani ya watu,na mhusika ni yuleyule
 
eti mitambo inawashwa,wapi bana,,,,hiyo mitambo ya aina gani wanawasha mwezi mzima?,mbona hata mitambo ya nyuklia haichukui mda wote huop kuwaka?
 
ndo hapo mtu unajiuliza,kwanini mkurugenzi wa tanesco bado yuko kazini........inakaa kama kuna element ndani ya serikali zinafanya sabotage...

Wangepewa zile fedha za escrow zingewafufua sana. Lakini pamoja na cag kuthibitisha fedha ni za serekali wakubwa wakasema si za serekali.
 
tanesccm katika ubora wake! waongo sana hawa!
 
Tuliaminishwa Gas imeshafika Dar kwenye mitambo ya Symbion,
leo tunaambiwa tatizo linatokana na upungufu katika uzalishaji wa umeme hasa katika vituo vya maji.
Tanesco na Serikali inataka kutwambia nini hapa?

nani kakudanganya kuwa gas ilifika dar
 
nani kakudanganya kuwa gas ilifika dar

Hapa naona umeongea kitu nyeti sana ila angalia usije toa siri bure. Ila sie malofa tulishadanganywa gas inaingizwa kwenye mitambo kumbe issue ni maji yamekauka
 
Tuamie kwenye umeme wa radi. Mkuu wa Bodi ya Tanywesico apewe furusa kuonyesha utaalamu wake kati teknolojia ya umeme wa Radi. Tutaepuka haya majanga.
 


Umeme unafanywa siasa acha kutetea vitu ambavyo vipo obvious.
Tanesco wanajua kuwa mahitaji ya umeme yanaongezeka kila kukicha na hatua madhubuti zinatakiwa kuchukuliwa.
Kwanin miaka na miaka tatizo la umeme haliishi? Linazidi kuchukua kasi?
Kutokea hitilafu sawa, ila umeme kukatwa mara kwa mara ni uzembe wa serikali ya CCM.
 
Hiyo ni leo....
Lakini pia baada ya kushughulikiwa kwa hitilafu........umeme hakuna.......hata jana kabla ya hitilafu.....juzi.....juzi ile.......umeme haukuwepo pia............

inapofika siku ya anguko lako Mungu hukupiga upofu ili usiweze kuona ukang'amua na kuokoka.kila ukifanyacho utakiona ni sawa
 
Dawa ni kuindoa ccm madarakani
 
Tuamie kwenye umeme wa radi. Mkuu wa Bodi ya Tanywesico apewe furusa kuonyesha utaalamu wake kati teknolojia ya umeme wa Radi. Tutaepuka haya majanga.

Kwa hiyo mkuu unataka kuniambia serikal ingie mkataba na wananchi wa shinyanga
 
nimewatukana hadi nimechoka... shirika la hitirafu tanzania, dawa yenu 25th oct
 

Bora leo kajaribu kusema kaukweli kuwa kuwa umeme hamna hadi mvua itakapo nyesha siyo ile blah blah eti gesi inawashwa kidogo kidogo wakati gesi walishapewa wachina.
 
Yaani hii nchi inatakiwa kiongozi dikteta ili akomeshe hali hii.

Ile ges iliyotoka mtwara imeenda wap?

Matumain ambayo serikal imekua ikitutangazia kila siku kuwa umeme utakua historia yapo wap

Yaan kila sehem ni rushwa na uchafu usiofaa

Sijui watanzania tuseme lugha gan hali hii ibadilike

Tanesco tumeingia nao mkataba watuhudumie ipasavyo lakin wameshindwa kufanya hivo

Tunahitaji kufanya kitu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…