Mocumentary
JF-Expert Member
- Jul 31, 2017
- 769
- 1,959
Tafadhali rejea mada tajwa hapo juu.kumbukumbu namba ya tarehe 29/08/2020 kutoka kwa ndugu Lazaro Stephano Maige ambaye tarehe 25/08/2020 aliteuliwa kuwa mgombea nafasi ya Ubunge kwa Jimbo la Ulyankulu kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akinijulisha kwamba amejitoa kugombea nafasi hiyo.
Kufuatia kujitoa kwa Mgombea Ubunge wa jimbo la Ulyankulu ndugu Lazaro Stephano Maige kutokea Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kumwacha mgombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Ulyankulu Bi. Rehema Juma Migilla kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa mgombea pekee.
Kwa mujibu wa kifungu cha 44 cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura 343 inafafanua kuwa, endapo mgombea aliyeteuliwa ni mmoja atahesabika kuwa amechaguliwa na upigaji kura hautafanyika katika jimbo hilo kwa uchaguzi wa mbunge.
Kwa barua hii, kutokana na maelezo yaliyopo hapo juu, ninakutaarifu kuwa, umepita bila kupingwa, hivyo mara baada ya Uchaguzi kukamilika utapatiwa hati ya kuchaguliwa.