Taarifa ya kuanza kwa kikao cha Bunge kesho | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taarifa ya kuanza kwa kikao cha Bunge kesho

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwanajamii, Apr 9, 2012.

 1. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #1
  Apr 9, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  [h=3]Taarifa Ya Kikao Kijacho Cha Bunge[/h]
  [​IMG]
  KIAPO CHA UTII KWA WABUNGE WAPYA:
  Kwa mujibu wa masharti ya Kanuni ya 24(1) ya Kanuni za Bunge, toleo la 2007 kutakuwa na Kiapo cha Utii kwa Wabunge wapya wawili. Wabunge hao ni Mheshimiwa Cecilia Danieli Paresso (Viti Maalum CHADEMA) aliyeteuliwa kujaza nafasi iliyoachwa wazi Kufuatia kifo cha marehemu Regia Estalatus Mtema aliyefariki kwa ajali ya gari, na Mheshimiwa Joshua Nassari (CHADEMA) aliyechaguliwa katika Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki uliofanyika tarehe 1 Aprili, 2012 kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo marehemu Jeremiah Solomon Sumari (CCM).


  SHUGHULI ZA SERIKALI:
  kwa Mujibu wa Kanuni ya 17 (1) (d) Toleo la 2007, Serikali ilikwishaziwasilisha kwa Katibu wa Bunge na shughuli za Serikali Bungeni katika Mkutano Ujao na kuorodheshwa kwenye Kitabu cha Shughuli za Bunge kama ifuatavyo:-


  MISWADA YA SHERIA YA SERIKALI:
  Miswada ya Sheria ya Serikali Minne(4) ambayo ilishasomwa kwa mara ya kwanza katika Mikutano ya Bunge iliyopita itawasilishwa Bungeni katika Mkutano ujao wa Bunge.. Miswada inayotarajiwa kusomwa kwa Mara ya Pili na kuendelea na hatua zake zote ni hii ifuatayo:-
  (Kusomwa kwa Mara ya Pili na Hatua Zake Zote Kwa Mujibu wa Kanuni ya 86 ya Kanuni za Bunge):
  Muswada wa Sheria ya Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania wa Mwaka 2011 [The Tanzania Livestock Research Institute Act, 2011];


  Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa Mwaka 2012 [The Social Security Laws (Amendments) Act, 2012 (No.2) Act, 2011];
  Muswada wa Sheria ya Marekebisho wa Sheria Mbalimbali wa Mwaka 2011 [The Written Laws (Miscellaneous Amendments) (No. 2) Act, 2011];
  Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali za Biashara wa Mwaka 2011. [The Business Laws (Miscellaneous Amendments) Bill, 2011].


  HOJA ZA SERIKALI:
  Bunge kukaa kama Kamati ya Mipango:
  Kwa Mujibu wa Kanuni ya 94, Bunge litakaa kama Kamati ya Mipango ili kutekeleza matakwa ya Ibara ya 63(3)(c) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, kujadili na kuishauri Serikali juu ya mapendekezo ya Mpango wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali katika Mwaka wa Fedha 2012/2013.


  Taarifa ya Serikali ya utekelezaji wa Maazimio ya Bunge:
  Katika Mkutano wa Tano wa Bunge Serikali ilipokea Mapendekezo yaliyotolewa na Kamati Teule ya Bunge iliyoundwa kuchunguza uhalali wa utaratibu wa Wizara ya Nishati na Madini kuchangisha fedha kwa ajili ya kupitisha Bajeti Bungeni. Hivyo basi katika Mkutano huu Serikali itatoa Bungeni Taarifa ya utekelezaji wa Maazimio hayo.


  SHUGHULI NYINGINE:
  MASWALI:
  Maswali kwa Waziri Mkuu:
  Kwa mujibu wa masharti ya Kanuni ya 38, Waziri Mkuu anatarajiwa kuulizwa na Wabunge maswali 16 ya msingi.
  (ii) Maswali ya Kawaida:
  Kwa mujibu wa Masharti ya Kanuni ya 39, Jumla ya Maswali 125 ya kawaida yanatarajiwa kuulizwa na Wabunge na kujibiwa na Serikali katika mkutano ujao wa Saba.


  TAARIFA ZA KAMATI ZA BUNGE:
  Kwa mujibu wa Kanuni ya 114 (15), Kamati za Bunge zitawasilisha Taarifa za kazi za Kamati kwa kipindi cha Mwaka wa Fedha 2010/2011 na Taarifa hizo zitajadiliwa na Bunge kwa kadri itakavyoonekana inafaa. Hivyo Taarifa hizo zitawasilishwa mezani tarehe 10 Aprili, 2012 ili kutoa fursa kwa Wabunge kuzipitia kabla ya kuanza kuchangia Bungeni.


  UCHAGUZI WA WABUNGE WA BUNGE LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI:
  Kufuatia kufika ukomo wa kipindi cha Ujumbe wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki na kwa kuzingatia masharti ya Mkataba wa kuanzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki na Kanuni za Bunge, katika Mkutano wa Saba wa Bunge kutakuwa na Uchaguzi wa Wabunge Tisa watakao iwakilisha Tanzania katika Bunge hilo. Hivyo kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa, siku ya uteuzi itakuwa ni Jumanne tarehe 10/4/2012 saa kumi jioni na Uchaguzi utafanyika siku ya Jumanne tarehe 17/4/2012.


  HOJA BINAFSI ZA WABUNGE:
  Kwa mujibu wa Kanuni ya 54, Katibu wa Bunge amepokea makusudio mawili ya Wabunge kutaka kuwasilishwa Hoja binafsi. Aidha, kwa mujibu wa fasili ya (1) na (2) ya Kanuni ya 55 Wabunge hao wameshaandikiwa barua ya kuwataka wawasilishe Taarifa za Hoja zao kwa Katibu wa Bunge. Endapo hoja hizo zitakidhi matakwa ya Kanuni za Bunge zitatengewa muda wa kuwasilishwa Bungeni katika Kikao kijacho cha Saba.
  MAMBO MENGINE:


  SEMINA ZA WABUNGE WOTE:
  Ofisi ya Bunge imepokea maombi mawili kutoka Taasisi mbili za Umma ya kufanya Semina kwa Wabunge katika Mkutano wa Saba wa Bunge. Semina hizo ni kama ifuatavyo:-
  Semina kwa Wabunge wote kuhusu Anuani Mpya za Makazi na Simbo za Posta pamoja na Mabadiliko ya Teknolojia ya Utangazaji kutoka Analojia kwenda Dijitali;
  Semina kwa Wabunge wote kuhusu Sensa ya Watu na Makazi.


  Imetolewa na
  Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa
  Ofisi ya Bunge
  Dar es Salaam
  7 Aprili, 2012
   
 2. T

  Tenths Senior Member

  #2
  Apr 9, 2012
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 108
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Asante kwa taarifa
   
 3. S

  Saitoti Member

  #3
  Apr 9, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante Mkuu.
   
 4. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #4
  Apr 9, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,407
  Trophy Points: 280
  Thanks for da info.
   
 5. S

  Saitoti Member

  #5
  Apr 9, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Katika Hoja binafsi nashauri Mh . Visenti Nyerere atoe hoja ya kuondoa pensheni kwa Mkapa na viongozi , Raisi mtaafu atakaye jishuhulisha na Siasa ( kampeni ) kwani anatumia kodi zetu.

  Pia kuhoji Waziri mkuu Pinda , Kutumia ufunguzi wa wa chuo cha VETA (Pwani) kunadi CCM Waziri alisema CCM oyee, Hiyo sio sahii kwani nimatumizi mabaya ya ofisi ya wazari mkuu.
   
 6. w

  warea JF-Expert Member

  #6
  Apr 9, 2012
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 244
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii taarifa mbona haipo kwenye tovuti ya bunge?
  Na lini tovuti ya bunge itaandikwa kwa kiswahili, maana taarifa za utendaji zimeandikwa kwa kiswahili, wakati tovuti yenyewe ni imeandikwa kiingereza? Au ndo falsafa ya kiswakinge?

  Tunajadili kwa kiswahili na kuandika ripoti kwa kiingereza! Au
  Tunaandaa tovuti kwa kiingereza, tunaweka humo vya kiswahili. Mzungu akifungua anakutana na kiswahili. Mswahili naye anaogopa kufungua ingawa ndani kuna kiswahili.
   
 7. B

  Benno JF-Expert Member

  #7
  Apr 9, 2012
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 332
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Utahoji kila kitu,
   
 8. F

  FJM JF-Expert Member

  #8
  Apr 9, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Hiyo statement inaonekana imeandikwa tarehe 7 Apri, Kikao cha bunge kinaanza tarehe 10 April. Lakini cha ajabu uongozi wa bunge bado hauna uhakika kama hoja binafsi zimekidhi matwaka au la! Siku 3 kabla ya kikao hauna uhakika wa hoja zitakazowakilishwa!!! Bunge la zima moto.
   
 9. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #9
  Apr 9, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  kwa hiyo ile taarifa ya kamati ya mama sitta kuhusu mgomo imepotezewa?
  Warudishe zile perdiems waache utani!
   
 10. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #10
  Apr 9, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Pia napendekeza kuwe kuna hoja binafsi kwa ajili serikali iwe inatenga fedha kwa ajili ya kununua magunia ya bangi am bayo yatatumiwa na Lema kwa ajili ya M4C maana huyu kijana ni mpambanaji sana.
  Peoples..............
   
 11. Mkondakaiye

  Mkondakaiye JF-Expert Member

  #11
  Apr 9, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 839
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Acha kejeli, kama unavuta wewe bangi usiwahusishe na makamanda wa CDM
   
 12. l

  liverpool2012 Senior Member

  #12
  Apr 9, 2012
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pia napendekeza wabunge vichaa(kibajaji) wapate muda wa kupeleka hoja binafsi

   
 13. chumvichumvi

  chumvichumvi JF-Expert Member

  #13
  Apr 9, 2012
  Joined: May 6, 2010
  Messages: 1,050
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  thanks for the info
   
 14. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #14
  Apr 9, 2012
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Ni jambo la kusikitisha kuona waTanzania wanakubali hii taasisi nayo imparanganyike; utaona jamaa wazuri kutoa taarifa kwenye blog binafsi badala ya kuweka kwenye tovuti yao.... yaani Du! Inasikitisha nimefuatilia kwa muda mrefu.... hii ndio trend, wabunge vijana please lisemeeni hili... otherwise itafika wakati hakuna taasisi itakayoamini tena Tanzania... I real miss Mr. Six.
   
 15. Mlingwa

  Mlingwa JF-Expert Member

  #15
  Apr 9, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 382
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tumekusoma mkuu
   
 16. marksalewi

  marksalewi Member

  #16
  Apr 9, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 95
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  dogo janja anasema tukazie macho tv kesho madam spika akimwapisha
   
 17. m

  matawi JF-Expert Member

  #17
  Apr 9, 2012
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Asante Inauma kwa taarifa muhimu kama hii keep up
   
 18. F

  FRANK MICHAEL Senior Member

  #18
  Apr 9, 2012
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 150
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Achana huyo mjinga nadhani jana kalala bar
   
 19. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #19
  Apr 9, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,544
  Likes Received: 10,481
  Trophy Points: 280
  hivi spika ni yuleyule au wanachagua mwingine si alisema ubunge haulipi.
   
Loading...