Taarifa ya jeshi la polisi kuhusu sheikh ponda

Taarifa ya jeshi la polisi kuhusu sheikh ponda

A-town

JF-Expert Member
Joined
Oct 25, 2011
Posts
494
Reaction score
169
[h=3][/h]
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NDANI
[TABLE="class: wsite-multicol-table"]
[TR="class: wsite-multicol-tr"]
[TD="class: wsite-multicol-col"]



AGOSTI 10, 2013.​
[/TD]
[TD="class: wsite-multicol-col"]
JESHI LA POLISI TANZANIA
DAR ES SALAAM
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]



1. MNAMO TAREHE 10, AGOSTI ,2013 MAJIRA YA SAA 8 MCHANA, MAENEO YA SHULE YA MSINGI KIWANJA CHA NDEGE MANISPAA YA MOROGORO, KULIFANYIKA KONGAMANO LA BARAZA LA EID LILILOANDALIWA NA UMOJA WA WAHADHILI MKOANI MOROGORO. DAKIKA KUMI KABLA YA KONGAMANO HILO KUMALIZIKA ALIFIKA SHEKHE PONDA ISSA PONDA AMBAYE ALIZUNGUMZA KWA MUDA MFUPI.

2. KONGAMANO HILO LILIFUNGWA MAJIRA YA SAA 12:05 JIONI AMBAPO WATU WALIANZA KUTAWANYIKA, BAADHI YAO WAKIWA WAMEZINGIRA GARI DOGO ALILOKUWA AMEPANDA SHEKHE PONDA. BAADA YA KUTOKA KATIKA ENEO HILO, ASKARI WA JESHI LA POLISI WALIZUIA GARI HILO KWA MBELE KWA NIA YA KUTAKA

KUMKAMATA SHEKHE PONDA AMBAYE MPAKA SASA ANATUHUMIWA KWA KOSA LA KUTOA MANENO YA UCHOCHEZI SEHEMU MBALIMBALI HAPA NCHINI YENYE MLENGO WA KUSABABISHA UVUNJIVU WA AMANI.

3. BAAADA YA ASKARI KUTAKA KUMKAMATA, WAFUASI WAKE WALIZUIA UKAMATAJI HUO KWA KUWARUSHIA MAWE ASKARI. KUFUATIA PURUKUSHANI HIYO, ASKARI WALIPIGA RISASI HEWANI KAMA ONYO LA KUWATAWANYA.

4. KATIKA VURUGU HIZO, WAFUASI HAO WALIFANIKIWA KUMTOROSHA MTUHUMIWA. HIVI SASA IMETHIBITIKA KUWA SHEKHE PONDA YUKO KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI AKITIBIWA JERAHA KATIKA BEGA LA MKONO WA KULIA LINALODAIWA ALILIPATA KATIKA PURUKUSHANI HIZO.

5. KUFUATIA TUKIO HILO, TIMU INAYOSHIRIKISHA WAJUMBE KUTOKA JUKWAA LA HAKI JINAI IKIONGOZWA NA KAMISHINA WA JESHI LA POLISI CP ISSAYA MNGULU IMEANZA KUFANYA UCHUNGUZI WA TUKIO HILO.

6. AIDHA, JESHI LA POLISI LINATOA WITO KWA WANANCHI KUWA WATULIVU WAKATI SUALA HILI LINASHUGHULIKIWA KISHERIA.

Imetolewa na:-
Advera Senso- SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.​





kitongoni kabange kitongoni at 7:20 Pm
 
Ni taarifa ya kibabaishaji kabisa, haielezi nani kamdhuru sheikh ambacho ndicho kiini cha mgogoro badala yake inapiga balah blah kama kawaida yake.
 
kwanini wasimfuate hapo muhimbili wakamtia pingu,hapo ndiyo sehemu nzuri ya kumhoji alifikaje hapo!
 
Ni taarifa ya kibabaishaji kabisa, haielezi nani kamdhuru sheikh ambacho ndicho kiini cha mgogoro badala yake inapiga balah blah kama kawaida yake.

Nani kamdhuru , ndio kitu kinachotafutwa , sasa huyo shekhe ponda walimtoroshaje mbona hapa sijaewa
 
" 4. KATIKA VURUGU HIZO, WAFUASI
HAO WALIFANIKIWA KUMTOROSHA
MTUHUMIWA. HIVI SASA
IMETHIBITIKA KUWA SHEKHE
PONDA YUKO KATIKA HOSPITALI YA
TAIFA YA MUHIMBILI AKITIBIWA
JERAHA KATIKA BEGA LA MKONO
WA KULIA LINALODAIWA ALILIPATA
KATIKA PURUKUSHANI HIZO."

naomba kujuzwa elimu ya
Advera Senso- SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
 
Uchunguzi utakamilika baada ya miezi 6.
Kabla ya uchunguzi kukamilika, kamanda wa polisi wa mkoa atakuwa amepandishwa cheo.
Hii ndiyo CCM na serikali yake.
 
Mtoto mdogo sana Ponda hawez kuchezea kesho ya Taifa alaf asiwajibishwe Serikali na imfanye chchte kwa manuefaa ya Taifa
 
Tukio la mwangosi walianza na porojo kama kawaida yao,baada ya picha wakaja kugeuza maneno,
 
si afadhali hioo taarifa aijasema uongo kuliko ya ulimboka yaanai naiangalia taarifa ya kupatikana alietaka kumuua ulimboka ikisomwa na kova hakika sina hamu na jeshi nikianzia na baba yangu mzee kova aisee.....kirahisi hivi mtu anaambiwa aseme hivi
 
" 4. KATIKA VURUGU HIZO, WAFUASI
HAO WALIFANIKIWA KUMTOROSHA
MTUHUMIWA. HIVI SASA
IMETHIBITIKA KUWA SHEKHE
PONDA YUKO KATIKA HOSPITALI YA
TAIFA YA MUHIMBILI AKITIBIWA
JERAHA KATIKA BEGA LA MKONO
WA KULIA LINALODAIWA ALILIPATA
KATIKA PURUKUSHANI HIZO."

naomba kujuzwa elimu ya
Advera Senso- SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Hahahaa, Option umenifurahisha swali lako. Nadhani atakuwa darasa la pili la mkoloni huyo.
 
Huyu mtu ni hatari kwa amani ya taifa letu.mzahamzaha hutumbua usaha.arudishwe jela aondoe balaa zake uraiani
 
Wanachoamini watawala ni kwamba Watanzania wameumbwa kusahau! Kwa hiyo kila linalotokea hata likiwa zito kiasi gani litakaa kwa muda mfupi then litapita kama upepo!!
 
Ni taarifa ya
kibabaishaji kabisa, haielezi nani kamdhuru sheikh ambacho ndicho kiini
cha mgogoro badala yake inapiga balah blah kama kawaida yake.

vyanzo vingne vya habari si vilishasema kuwa Shekh Ponda alipigwa risasi na askari wa Ustaadh Said Mwema kwa amri ya Al haji Dr.Jah-kaya Khalfan Kikwet'?
 
Back
Top Bottom