Ni lazima kwa wakati huu, na haraka iwezekanavyo, Serikali ikazungumza na Masheikh, bila ya kuona muhali, na kwa uwazi kabisa, ili kutafuta suluhu ya kudumu, kwa faida ya Nchi na Taifa kwa Ujumla.
Asanteni wana CUF kwa taarifa.
mkuu kwani uamsho sio wazanzibari?Wazanzibar ni watu wakarimu sana, Tatizo nadhani ni hao uamsho wanao Taka damu imwagike Zanzibar kwa maslahi yao
Mkuu wangu hadi sasa hivi nashindwa kabisa kuelewa hili swala la kuujadili Muungano. kinachotakiwa kujadili ni nini hasa?.. kuwepo kwa Muungano au kero zilizozopo ndani ya Muungano.Asante CUF kwa kutoa tamko. ingawa wakati mwingine kutoa tamko kunaweza kuonyesha welevu ama ujinga wa mtu. Kiini cha tatizo la wazanzibari, ni Mkuu wa kaya, bunge pamoja na wabunge wote ambao kwa pamoja walipitisha sheria gandamizi ya kuzuia watu kutoa maoni yao wakati wa mchakato wa katiba. KIPEKEE, NAPENDA KUWAPONGEZA WABUNGE WOTE WALIOTOKA NJE YA BUNGE WAKATI SHERIA HII GANDAMIZI INAPITISHWA. Hakuna namna ya jinsi watakavyo kwepa kubeba dhamana wale wote waliokubali kwa pamoja kupitisha sheria ya kuzuia watu wasijadili muungano wakati muungano ni sehemu kubwa ya Katiba.
Matokeo ya kuziba watu midomo wasiseme kwa maneno ni kusema kwa vitendo. Hii ndiyo sababu kubwa ya yote yanayotokea zanzibari.
siwalaumu wazanzibari, siwalaumu waisilamu, wala sitalaumu UAMUSHO, bali lawama zangu ziende kwa mkuu wa kaya pamoja na wabunge wote walioshiriki kupitisha sheria gandamizi. Nawashukuru wabunge wote walio toka nje ya bunge kupinga sheria hii.
Kwa kuwa hakuna anayependa kuona machafuko, Lawama sasa hivi hazina msaada wala nafasi, napenda kumwomba Mkuu wa kaya, kwa busara zake, atoe nafasi kwa bunge lake tukufu, kikao cha kwanza, cha mwezi ujao, kiondoe sheria hii gandamizi, kiruhusu Muungano ujadiliwe, na mawazo ya wananchi yapewe nafasi.
"MUNGU IBARIKI TANGANYIKA, MUNGU IBARIKI ZANZIBARI, RIP TANZANIA"
Mkuu wangu hadi sasa hivi nashindwa kabisa kuelewa hili swala la kuujadili Muungano. kinachotakiwa kujadili ni nini hasa?.. kuwepo kwa Muungano au kero zilizozopo ndani ya Muungano.
Maana nijuavyo mimi hawa UAMSHO wasichokitaka ni MUUNGANO kwa sababu wanadai ni batil na kifupi haukuwa halali kwani wananchi hawakuhusishwa na kadhalika.
Nachpenda kuuliza miye ni kwamba ni muungano gani wa nchi mbili kuunda moja ambao umehusisha wananchi? hivi kweli wewe unaweza kuuliza hati ya ndoa ya wazazi wako ili kuhalalisha kuzaliwa kwako? na hata kama wakikupa itaondoa karaha za kero za mateso unayopewa n mzazi wako kwa fikra na imani kwamba mzazi wako hawezi kukutendea mabaya!
Ni muhimu sana kufikiria nje ya box la Uzanzibar kwa sababu kuna Wazanzibara wengi kuliko kundi dogo sana la walalahoi ambao wanafikiria zaidi mkono unaoingia kinywani. Msityaombee yaliyotokea Sudan na yanaendelea kuwakwaza hata pale walipofikiria wamemaliza matatizo yao kumbe ndio kwanza wamewasha moto mwingine. Muungano sii swala la ardhi hata kidogo bali unganisho wa WATU wake na umaskini wa Zanzibar unatengenezwa na viongozi wetu wenyewe kama ilivyo bara na maskini wengine nchi nyinginezo. Uhuru, haki na usawa haupiganiwi kwa kutazama matabaka ya uzawa ama dini bali kile unachoamini ni haki ya kuishi kwa kila binadamu iwe mkristu au muislaam.
Wazanzibar ni watu wakarimu sana, Tatizo nadhani ni hao uamsho wanao Taka damu imwagike Zanzibar kwa maslahi yao
Wazanzibar ni watu wakarimu sana, Tatizo nadhani ni hao uamsho wanao Taka damu imwagike Zanzibar kwa maslahi yao
Wazanzibar ni watu wakarimu sana, Tatizo nadhani ni hao uamsho wanao Taka damu imwagike Zanzibar kwa maslahi yao
Wazanzibar ni watu wakarimu sana, Tatizo nadhani ni hao uamsho wanao Taka damu imwagike Zanzibar kwa maslahi yao