Taarifa: TRA kugawa mashine za EFD jijini Dar

Sasa kule kulazimisha kuwauzia wafanyabiashara kwa bei ghafla sababu zake ni nini....bila shaka mtaji umerudi!!
 
Wanaingizwa kwenye mtego utawasikia watavyo lalamika watakapojikuta wanajipelekea VAT wenyewe
 
Point I entirely agree with you mkuu
 
Kukwepa kodi kuna husika kwa njia moja ama nyingine
Mi nimeifunga wiki sasa haijatuma taarifa
Nawasubiria waje siwaoni
 
Wafanyabiashara hawakosi sababu
Kama wewe si mfanyabiashara huwezi jua nini kinatokea sasa...lakini chukua muda utafute takwimu za kibiashara na mapato kwa miezi mitatu tu iliyopita utapata picha halisi jinsi hii sekta ilivyoyumba
 
Nimesafiri nchi mbalimbali nimeona baadhi ya nchi za africa zinazosimamia ukusanyaji wa kwa mashine mpaka kwa mama lishe,machinga nk,na wananchi wamezoea na ni jambo la lazima Hivyo basi watanzania lazima tubadilike kila unaponunua bidhaa yoyote dai risiti na mfanyabiashara toa risiti kwani kuna ugumu gani?
Mashine za EFD kutolewa bure mimi binafsi ninamuunga Rais
 
Hivi ndivyo inavyotakiwa sio tu kuwalazimisha kununua. sasa sijui wale waliokwisha kunuzinunua watafikiriwaje?

Tokea mwanzo mashine ni bure, tatizo elimu haikutolewa ya kutosha, na pia kutokua na tabia ya kuuliza wahusika sahihi, information nyingi tunapata mtaani ambazo zinakua si sahihi na siasa pia zikaingia tena juu yake.

Sheria ya EFD inavyosema, mfanyabiashara anaponunua mashine ya efd (moja au zaidi) kwa mara ya kwanza atarudishiwa pesa yake yote kwa njia ya kodi pindi atakapoanza kuitumia. Mfano alitakiwa alipe kodi milioni moja, na kanunua mashine laki nane basi atatakiwa kulipa kodi laki mbili tu. Kwa wale ambao huwa wanakwepa kodi, ndio watakua hawana namna ya kurejesha hela yao.
 
Wanaingizwa kwenye mtego utawasikia watavyo lalamika watakapojikuta wanajipelekea VAT wenyewe
VAT haina tatizo kama watu wanavyofikiri, kikubwa ni kupata elimu yake. Na kwa sasa TRA haitoi VAT kirahisi, wamegundua watu wengi wanatumia VAT kukwepa kodi. Anyway, umeshasikia mtu mwenye VAT analalamikia VAT na kutaka kuondolewa?
Sasa hivi kuingizwa VAT ni mpaka uwe na mauzo ya analau 100m kwa mwaka.

Ni hivi, kwa faida ya wasiojua mambo ya return.
Unaponunua bidhaa ya Tsh. 1180 (1000 + 180 ya VAT)
Ukaiuza hiyo bidhaa kwa TShs 1416 (1200 + 216 ya VAT)

Kiasi cha VAT unachotakiwa kupeleka TRA kwa hiyo bidhaa ni sh 36 tu na sio 216 yaani ( 216 - 180 = 36 ).

Sasa kwa mfano jumla ya manunuzi yako kwa mwezi ni 1m ambayo VAT yake tuseme ni 180,000
Na mauzo yako kwa mwezi huo ni laki nane ambayo VAT yake tuseme ni 144,000

Ina mana kwa mwezi huo, hutolipa kodi na bado unawadai TRA sh 36,000 (180,000 - 144,00).

Ndio mana kuna wafanyabiashara wasio waaminifu wanachofanya wananunua risiti za manunuzi za watu, wanajumlisha kwenye mahesabu yao kukwepa kodi.

Kwa maelezo zaidi ya VAT nenda ofisi yeyote ya TRA, kuna ofisi ya elimu kwa mteja.
 
Point I entirely agree with you mkuu

Mashine zote za phaze II (kuanzia 2013) zinaingiza manunuzi pia, sema watu wenyewe hawatumii au hawajui. Ila manunuzi lazima yawe na risiti za EFD, so ukinunua mzio dai risiti. Kama hufahamu jinsi ya kuiniza, nenda kwa aliye kuuzia akuelekeze. kuiniza manunuzi ni rahisi kuliko hata kutoa risiti.

Na kitu kingine, mpaka sasa hivi, mfumo wa kodi ni ule ule, hamna kilichobadilika. unaweza uliza walioanza tumia mashine tokea 2013, hamna aliyeongezewa kodi kwasababu ametumia mashine, labda kama mtaji wake umekua.
 

mkuu upo sahihi kabisa ila kuna baadhi ya vilaza wameshindwa kukuelewa.
ngoja nitoe mfano kidogo hapa,
-kodi ni 18% ya ulicho uza
-nimenunu bidhaa ya jumla dar kwa sh.8000/- nikasafirisha mpaka mkoani
-nikauza rejareja kwa sh.10000/-
-calculate kodi 18% ya 10000/-
-kodi ya TRA kwa bidhaa hiyo ni sh.1800/-
-kilichobaki kwa mfanya biashara ni sh.200/- katika bidhaa hiyo
-hapo hujalipa fixed cost za kuendesha biashara yako na familia yako
watu tuache ushabiki wa kipumbavu tuwe realistic.
 
Kweli mtu aliyekuuzia kukufundisha na kwanini TRA wasifundishe walipa kodi ili aya malalamiko yasijirudie tena?
 
Kuwakamata wakamatwe tu, hakuna namna.

Mimi ugomvi wangu ni kwa kanuni ya kuipata hiyo kodi. TRA wameshindwa kuainisha ni 18% ya kitu gani. Wao wanakata 28% ya mauzo ambayo ukiitafakari inakula hadi mtaji.

Mfano mauzo ya pukipi 1,800,000/-, hata kabla ya EFD, hiyo ndo bei. Na mfanyabiashara anafukuzia 50,000/- hadi 100,000 kwa mfano. Lakini 18% ya 1,800,000= ni 324,000/- ambayo imeingilia hadi mtaji. Hivyo wafanya biashara watafunga maduka yao.

Kwa nini hawafungi maduka?

1. Hujitahidi kutotumia mashine za efd. Baadhi ya maduka ukidai risit hiyo, uteja unaisha. Anachukua mali yake, anakurudishia pesa yake.
2. Huziharibu machine za efd ili zifanye yale watakayo.
3. Ni kuandika thamani ndogo kulinganisha na thamani halisi ya bidhaa iliyonunuliwa. Hii ndo inayotumika kwa wafanya biashara wengi.

Mfano, hiyo pkpk ya 1,800,000/- ambapo yeye anatafuta faida ya 50,000- hadi 100,000/-, ukinunua kwenye receipt ataandika let say 80,000/- ambayo kodi yake ni 14,400/-. Ukitoa kwenye 50,000/- atabaki na 35,600/- au ukitoa kwa 100,000/- atabaki na 85,600/- ili alipie chumba, leseni, wasaidizi, kodi ya anakoishi n.k

Hapo tra walifikiria kwa kutumia Masaburi.
 
AAcha siasa kwenye kila jambo,mwanzo mlilalamika mashine bei juu,mmepewa sasa unakuja na visababu kibao huku ukipiga ramli za mgomo.Akili za Mbowe hizi.


Tatizo mnaleta siasa kwenye maisha ya watu mtakuja kulia humu maana hamjui kwa nini wafanyabiashara wanalalamika
 


Umezungumza kitu makini kwa tunaoelewa biashara na ukataji kodi wa mashine hizi
 


Hauko sahihi boss.. nadhani kama kuna mfanya biashara mwenye VAT experience atujuze.

Pili mfanyabiashara mwenye VAT, yeye halipi VAT, anayelipa ni mnunuzi wa mwisho kabisa, ndio mana yeye anadai (claim) VAT TRA mwiho wa siku. kwa mfano wako uliotoa. bidhaa ya 8000 VAT yake ni 1440, na ameuza kwa 10,000 ambayo VAT yake ni 1800. Kiasi anachotakiwa kupeleka TRA ni 1800 - 1440 = 360 tu,

Pia kwa wafanya biashara wanachofanya, anaweka faida yake then juu yake anaweka kodi. kwa mfano wako, kama anataka kupata faida ya 2000. basi atauza 10,000 plus VAT. yaani 11800. Vininevyo watu wangefunga maduka, isingekua biashara.
Hapa kikubwa ni kupata elimu ya kodi, kutoka kwa watu wanaohusika na kodi. kama kuna wataalam watusaidie
 

Mkuu hizo hesabu za wapi?, TRA wanakata 18% ya mauzo yako na siyo 18% ya faida yako na ndiyo ugomvi na wafanyabiashara unapoaanzia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…