Taarifa rasmi ya PAC juu ya jinsi wanavyotuibia kupitia ATCL

Taarifa rasmi ya PAC juu ya jinsi wanavyotuibia kupitia ATCL

Hansen Nasli

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2012
Posts
883
Reaction score
338
TAARIFA MAALUM KUHUSU KAMPUNI YA NDEGE YA TANZANIA (ATCL)

Mheshimiwa Spika, Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL) ilianzishwa mwezi Novemba 2002 baada ya Serikali kubinafsisha lililokuwa Shirika la Ndege la Tanzania (Air Tanzania Corporation, ATC); katika Shirika hilo, Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA) lilinunua hisa asilimia 49 ndani ya ATC. Hata hivyo ubia kati ya ATCL na SAA ulikabiliwa na matatizo ya kiuendeshaji na kulazimika kusitishwa mwezi Agosti 2006 na ATCL kurejeshwa tena Serikalini kwa asilimia 100.

2.8.1 Hali halisi ya ATCL kwa sasa Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Taarifa ya Msajili wa Hazina kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2013 na kwa kuzingatia Taarifa ya Wizara ya Uchukuzi, imebainika kuwa ATCL kwa sasa ina Ndege moja tu aina ya Dash 8 – Q 300, Wafanyakazi 142 na Jengo la ATC House lililoko mtaa wa Ohio, Dar es Salaam huku ikiwa na madeni makubwa kama itakavyofafanuliwa hapo baadae.

2.8.2 ATCL imefikaje hapo ilipo kifedha na kuwa na Madeni makubwa?
Mheshimiwa Spika, baada ya kuvunjika kwa mkataba wa ubia baina ya SAA ana ATC, mnamo mwezi Machi 2008, Wizara ya Miundombinu kwa wakati huo iliingia katika makubaliano na Kampuni ya China Sonangol kuwa Kampuni hiyo ya China ingeleta ndege mpya 7 kwa ATCL ikiwamo Ndege 5 aina ya Airbus ambazo zingewasili mwaka 2012 na 2013.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Msajili wa Hazina na Uongozi wa Wizara ya Uchukuzi, Wakati ATCL ikisubiri ndege hizo mpya, Kampuni ya China Sonangol iliitambulisha Kampuni ya Wallis Trading Inc kwa ATCL na kisha Kampuni hizi mbili (Wallis Trading Inc na ATCL) zikaingia mkataba wa Ukodishaji ndege aina ya Airbus 320 kwa kipindi cha miaka 6 kwa Malipo ya USD 370,000 kila mwezi.

Mheshimiwa Spika, huu ndio ulikuwa mwanzo wa mwisho wa ATCL, kwani baada ya Ndege hiyo kuwasili ilifanya kazi kwa muda wa miezi sita tu na baadae ilifungiwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kwa kushindwa kutekeleza matakwa ya usafiri wa anga. Ndege hiyo ilipelekwa kwa matengenezo makubwa mwezi Julai, 2009 nchini Ufaransa na haijawahi kurudi hadi leo wakati ambapo Serikali kama mdhamini wa ATCL anadaiwa fedha nyingi na Kampuni ya Wallis.

Mheshimiwa Spika, kutokana na deni la ATCL kwa Wallis linalofikia USD 42,459,316.12 hadi tarehe 31 Oktoba, 2011 na kufuatia majadiliano mbalimbali baina ya Serikali na Kampuni hiyo, Serikali imekwishalipa jumla ya USD 26,115,428.75 hadi sasa wakati bakaa inayodaiwa ni USD 23,996,327.82.

Mheshimiwa Spika, Kamati inasikitishwa sana na upotevu huu wa fedha za Umma ambao umetokanana mkataba mbovu ulioingiwa na watumishi wa Umma wasiokuwa waaminifu na uchungu na Taifa lao.

Mabilioni ya fedha yanaoendelea kulipwa kwa Kampuni ya Wallis kwa huduma ya ndege iliyofanya kazi hapa nchini kwa miezi sita tu na kisha ndege hiyo kupelekwa Ufaransa kwa matengenezo ni fedheha kubwa kwa wazalendo wa Taifa letu. Aidha, Taarifa zinasema ndege hiyo ikiwa Ufaransa ilipakwa rangi na kukodishwa kwa Shirika la ndege la nchi ya Guinea wakati Serikali yetu ikiendelea kulipia tozo ya ukodishaji wa ndege husika.

Mheshimiwa Spika, ni wakati sasa kwa Serikali kuamua kwa dhati kushughulikia suala la ATCL kwa mapana yake ikiwa ni pamoja na kuangalia uhalali wa kulipa deni la Wallis (ambalo lipo chini ya dhamana ya Serikali, hivyo ni fedha za Umma) ambaye kimsingi naye alikiuka makubaliano ya Mkataba kwa kukodisha ndege iliyokuwa imekodishwa tayari kwa ATCL. Aidha, ni muhimu wahusika wa uingiaji wa mkataba husika wakafikishwa kwenye vyombo vya sheria ili haki itendeke.

Mapendekezo kuhusu deni la USD 23,996,327.82 ambalo ATCL inadaiwa na Wallis Trading Inc. KWA KUWA, Serikali haikunufaika na mkataba wa kukodisha ndege aina ya Airbus kutoka kwa Kampuni ya Wallis baada ya ndege hiyo kugundulika ni mbovu ndani ya miezi sita na kupelekwa kutengenezwa kwa muda mrefu,

NA KWA KUWA, Serikali inaendelea kulipa tozo yaukodishaji wa ndege hiyo ambayo haifanyika kazi,HIVYO BASI, Kamati inapendekeza yafuatayo;

a) Serikali kuangalia uhalali wa kulipa deni la Wallis ambaye kimsingi naye alikiuka makubaliano ya Mkataba kwa kukodisha ndege iliyokuwa imekodishwa tayari kwa ATCL.

b) Serikali ihakikishe inawafikisha kwenye vyombo vya Sheria ili haki itendeke kwa wahusika wa uingiaji wa mkataba huo unaoendelea kuipa hasara Serikali kwani hadi sasa hakuna kesi iliyopelekwa mahakamani mahususi kwa waliongia mkataba husika.
 
Nimemsikia Waziri akitoa majibu mepesi kabisa katika hili swala, only in Tanzania.
 
Inasikitisha sana kwakweli, laiti bibiyangu kule kijijini angeyajua haya katu asingepanga foleni kuipigia kura ccm kwa ahadi ya kanga na ugimbi.

Watanzania tunaumizwa huku tunaona..!!!!

BACK TANGANYIKA
 
  • Thanks
Reactions: jme
Watanzania msiwalaumu CCM. Acheni wafanye kazi yao kwa kuwa hawakuingia msituni na kutwaa madaraka. Mliwachagua ninyi wenyewe kwa kura zenu. Mjilaumu ninyi wenyewe kwani hayo ndiyo malipo ya rushwa ya chumvi, kanga na vikofia vya kijani!
 
Hali hii tunaendelea nayo mpaka lini? Mbona tunakuwa kama taifa la majuha kabisa? Inamaana hata huyo waziri Mwakyembe tunayemuita jembe kwa siku hizo zote alikuwa hayajui yote hayo? Bwana mkubwa mwenyewe naye kila siku mguu na njia bado alikuwa naha taarifa hizi mbaya sana kwa taifa?
Yaani sasa kila kitu kinaenda hovyo kwa miaka chungu tele kisha ndio kiibuliwe wakati maumivu yashakuwa hayavumiliki tena?
 
Mkuu wote wapiga madili unadhani nani atamzuia mwezie? Sana akigundua atadai na yeye apate mgao.
 
Piga Zitto hakika wewe ni jembe kichwa chako kimoja ni sawa na vichwa vyote vya UKAWA watajuta kukupoteza manake tumewaona wapinzani kipindi hiki wanakimbilia hoja za Zitto ili kujipatia umaarufu hakuna cha Mbowe,Lisu,lipumba,Mnyika,Lema,Msigwa,Wenje wala cha nani wote hao wanaangaika kutembelea nyota yako ili kujipatia umaarufu wao na vyama vyao vyenye sera za ukoka toka wakufukuze wanajuuuta manake kwisha habari yao hawana hoja
 
Inasikitisha sana kwakweli, laiti bibiyangu kule kijijini angeyajua haya katu asingepanga foleni kuipigia kura ccm kwa ahadi ya kanga na ugimbi.

Watanzania tunaumizwa huku tunaona..!!!!

BACK TANGANYIKA
 
inatia hasira sana asee.ningejua nisinge soma.nimekasilika sana
 
Piga Zitto hakika wewe ni jembe kichwa chako kimoja ni sawa na vichwa vyote vya UKAWA watajuta kukupoteza manake tumewaona wapinzani kipindi hiki wanakimbilia hoja za Zitto ili kujipatia umaarufu hakuna cha Mbowe,Lisu,lipumba,Mnyika,Lema,Msigwa,Wenje wala cha nani wote hao wanaangaika kutembelea nyota yako ili kujipatia umaarufu wao na vyama vyao vyenye sera za ukoka toka wakufukuze wanajuuuta manake kwisha habari yao hawana hoja
Nilidhani tungejadili yaliyodili katika ripoti ya Zitto. Lakini wewe hujitambui maana kazi anayoifanya Zitto ni kwa manufaa ya Watanania wote, na nina hakika Zitto mwenyewe wala hatakusikiliza kwa haya uliyoyaandika. Tulikuwa na sakata la escrow halikuletwa na Zitto. Mwache Zitto atufanyie kazi tuliyomtuma pasipo kumgombanisha na wanasiasa wenzake.
 
Piga Zitto hakika wewe ni jembe kichwa chako kimoja ni sawa na vichwa vyote vya UKAWA watajuta kukupoteza manake tumewaona wapinzani kipindi hiki wanakimbilia hoja za Zitto ili kujipatia umaarufu hakuna cha Mbowe,Lisu,lipumba,Mnyika,Lema,Msigwa,Wenje wala cha nani wote hao wanaangaika kutembelea nyota yako ili kujipatia umaarufu wao na vyama vyao vyenye sera za ukoka toka wakufukuze wanajuuuta manake kwisha habari yao hawana hoja

Hapo ndo unapoonesha akili zako ni za dv 5.Hoja iliyowasilishwa na Zitto ni ya PAC,kamati ambayo ina wajumbe 24/25 kama cjakosea.Zitto hayupo kwenye hiyo kamati peke yake,kwa Hoja yako unawatusi other members wa PAC, si UKAWA.
 
Inasikitisha sana kwakweli, laiti bibiyangu kule kijijini angeyajua haya katu asingepanga foleni kuipigia kura ccm kwa ahadi ya kanga na ugimbi.

Watanzania tunaumizwa huku tunaona..!!!!

BACK TANGANYIKA
mkuu kama nyie watu wa tunduma mumeweza hata wao wengine wataweza tu
 
Hali hii tunaendelea nayo mpaka lini? Mbona tunakuwa kama taifa la majuha kabisa? Inamaana hata huyo waziri Mwakyembe tunayemuita jembe kwa siku hizo zote alikuwa hayajui yote hayo? Bwana mkubwa mwenyewe naye kila siku mguu na njia bado alikuwa naha taarifa hizi mbaya sana kwa taifa?
Yaani sasa kila kitu kinaenda hovyo kwa miaka chungu tele kisha ndio kiibuliwe wakati maumivu yashakuwa hayavumiliki tena?

JK aliijua hii sakata ndio maana kamtoa mwakyembe chapchap toka wizara ya uchukuzi. Bado issue ya mabehewa na vichwa vya treni!
 
Inauma halafu inasikitisha kumbe ndio maana Rais akacheza kumuondoa Mwakyembe Zitto asimuondoe kwenye uwazir wake
 
hivi hakuna namna ya kuwafikisha hawa jamaa mahakamani? mbona wamelinajisi taifa kiasi hiki? ewe Mwenyezi Mungu hebu tusaidie viumbe wako.
habari kama hii ninapoisoma huwa inaniharibia siku yangu kabisa.
 
Back
Top Bottom