Taarifa Rasmi ya CHADEMA Kuhusu Msiba wa Mzee Philemon Ndesamburo

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
TANZIA

Mwenyekiti wa Chama Taifa, Freeman Mbowe ametangaza msiba wa mmoja wa Waasisi wa CHADEMA, Mzee Philemon Ndesamburo na kusema kuwa nchi imempoteza mmoja wa watu mahiri waliopigania demokrasia na maendeleo, kwa maneno na vitendo, kwa ajili ya maendeleo ya nchi kwa vizazi vya sasa na baadae.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma kuhusu msiba huo uliotokea leo ghafla asubuhi, Mhe. Mbowe amesema chama kimempoteza mmoja wa 'makamanda' waliokiasisi na kusimamia agenda za mabadiliko kwa miaka zaidi ya 25 bila kuchoka pamoja na kuwepo vikwazo mbalimbali katika mapambano hayo.

"Nimepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa za kifo cha Mhe. Philemon Ndesamburo aliyefariki mapema leo Jumatano Mei 31, 2017, majira ya asubuhi. Ni hudhuni kubwa na maumivu makali yasiyoelezeka kwa kumpoteza Kiongozi na Mzee watu.

"Mzee Ndesamburo ni mmoja wa waasisi wa Chama Chetu cha CHADEMA na siasa za mabadiliko kwa ujumla nchini. Amekuwa Mbunge wa Moshi Mjini kwa miaka 15, ni Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Kilimanjaro na Mjumbe Baraza Kuu la CHADEMA na juzi tu siku ya Jumamosi 27 Mei 2017 alishiriki kikao cha Baraza Kuu mjini Dodoma.

"Leo alikuwa na miadi ya kukutana na Meya wa Jiji la Arusha Mhe. Lazaro Kalist kwa ajili ya kumpatia rambirambi yake kwa watoto wa Shule ya msingi ya Lucky Vincent ya Arusha waliofariki katika ajali mbaya gari hivi karibuni.

"Mstahiki Meya alifika ofisini kwa Mhe. Ndesamburo, ili aandikiwe hundi hiyo, wakati amechukua kalamu aandike hundi hiyo aghafla Mzee wetu akajisikia vibaya akaangua hivyo akalazimika kukimbizwa hospitalini ambapo mauti yalimkuta," amesema Mhe. Mbowe na kuongeza;

"Chama kimempoteza mpambanaji na mpigania ukombozi na mabadiliko ya kweli ndani ya Taifa, alifahamu kupigania na kutafuta haki, uongozi bora na demokrasia katika Taifa letu.

"Kwa niaba ya chama na viongozi wenzangu, natoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wote bila kusahau wanachama, wapenzi wote wa CHADEMA nchi nzima na Watanzania wote walioguswa na msiba huu mkubwa kwa kumpoteza Kiongozi wetu."

Mhe. Mbowe amesema kuwa katika maisha ya mwanadamu huu ndio wakati mgumu kuliko wote, ambapo ameomba Mwenyezi Mungu awatie nguvu familia ya Mhe. Ndesamburo katika wakati huu mzito wa majonzi ya msiba huo.

Mhe. Mbowe amemuelezea Mzee Ndesamburo kama kiongozi shupavu, jasiri, aliyejiamini.

Ameongeza kuwa ingawa kimwili hatuko nae lakini, hekima, busara na matendo yake yataishi milele yakifanya akumbukwe daima.

Bwana alitoa, Bwana ametwaa. Jina lake lihimidiwe.

Imetolewa na:

Tumaini Makene

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA
 
Tumaini Makene kazi ya kuhabarisha UMMA hapo Ufipa imemshinda?

Inakuaje taarifa nzito namna hii mnazitoa muda muutakao nyie?


CDM inahitaji reformation ya hali ya Juu..
 
Tumaini Makene kazi ya kuhabarisha UMMA hapo Ufipa imemshinda?

Inakuaje taarifa nzito namna hii mnazitoa muda muutakao nyie?


CDM inahitaji reformation ya hali ya Juu..
Huu si muda wa lawama mkuu ...tumpumzishe mzee wetu kwa amani then turudi kwenye haya ....
 
Pamoja na kuwa wote tutaelekea huko lakini inauma.
Mungu awape moyo wa uvumilivu wafiwa wote na wengine wote na hasa wanasiasa wajifunze kwake siasa hasa kutogeuka geuka - yaani ukigeugeu.
Alisimamia anachokiamini bila kujali vitisho au upepo kitu wanachokosa wanasiasa wengi wa sasa hivi.
 
Poleni sana wana CHADEMA wote Tanzania nzima na wale mlio nje ya Tanzania kwa kuondokewa na alama ya Kipekee ya Kishujaa na Maendeleo Mzee Philemon Ndesamburo. Ama hakika ni moja ya pigo kubwa ndani ya Chama chenu Kikuu cha Upinzani nchini Tanzania kwani hakuwa tu ni Mwanasiasa mwenzenu bali alikuwa pia ni Kiongozi na Dira ya Kiutendaji wa wengineo wote.

Kikubwa tumieni hiki Kifo chake kama chachu yenu ya kuelekea katika Mapambano ya Kiuokombozi ya nchi hii ambayo mnayaamini ili muweze pia kumuenzi vizuri sana huyu Mzee wenu ambaye hata Mimi Mshabiki wa CCM nilikuwa namkubali, namheshimu na nilipenda mno Siasa zake ambazo zilijikita zaidi katika Kutenda kuliko Kuzungumza na alichokifanya kinaonekana mno katika Jimbo aliloliongoza.

Sidhani kama huu utabaki tu kuwa ni Msiba wa wana CHADEMA bali nadhani huu utakuwa ni Msiba wa Watanzania wanaoamini zaidi katika Siasa za Kistaarabu, Kiungwana na Kimaendeleo zaidi ambazo nadhani ndizo zina afya zaidi kuliko zile za maji taka. Mzee Ndesamburo ametuachia somo kubwa, zuri na litakaloishi mioyoni mwetu sisi Vijana na Wanasiasa wachanga.

Poleni sana wana CHADEMA wote, Familia yake nzima, Watanzania na Wanasiasa wote na Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi Amen.
 
R.I.P. Philemon Ndesa Pesa.
Hakika ulikuwa jembe ndani na nje ya CHADEMA.
Remember you always!
 
Tangulia kamanda ni kati ya wale makamanda walioitangaza chama ndani na nje ya mipaka ya nchi yetu na alikuwa ni mfano bora wa kuigwa kwa kuipigania moshi mjini kusonga mbele alikuwa mmoja lakini ni zaidi ya wabunge wa ccm 100!
 
Tumaini Makene kazi ya kuhabarisha UMMA hapo Ufipa imemshinda?

Inakuaje taarifa nzito namna hii mnazitoa muda muutakao nyie?


CDM inahitaji reformation ya hali ya Juu..
Angekuwa Mbowe kaitwa polisi,Makene angekurupuka fasta,maana Mbowe ndio ulaji wake
 
Back
Top Bottom