Zogoo da khama
JF-Expert Member
- May 20, 2013
- 643
- 619
Wapendwa Salaam,
Muda si mrefu nimepokea simu toka kwa mtu nisiyemfahamu, namba yake ni 0692 242 138 baada ya salam, akajitambulisha kwamba yeye anaongea toka Airtel huduma kwa wateja.
Swali lake la kwanza nazionaje huduma zao, nikamjibu wastani, pili akasema nimezawadiwa Tsh. 150,000 kwa siku ya leo, nikasema asante, akasema kuna masharti natakiwa nitayatii ili kupata hiyo pesa, hapo sasa ndo pagumu, ile kuuliza maswala ya miamala yangu na lini mara ya mwisho kutoa pesa.
Nikajibu hayakuhusu we weka mzigo basi jamaa kakata simu. Nimepiga Airtel huduma kwa wateja wameikana hiyo namba pia hawana kitu kama hicho. Mpaka hapo mshapata picha ya utapeli ulivyo, ukijichanganya tu kutoa taarifa ya miamala yako umepigwa/ibiwa.
Jioni njema