Taarifa muhimu juu ya maendeleo ya CHAWADE

Taarifa muhimu juu ya maendeleo ya CHAWADE

Cha kustaajabisha hiki chama kina wanachama 8000 ambao ni wengi kuliko 6000 wa ACT! Halafu Kuna mijitu humu inasema Zitto ana mvuto! Ana mvuto halafu anapitwa na Chawade kwa wengi WA wanachama?
 
Tulishawazoea hawa...mwenzao Act...kashakufa kwa kukosa fedha....amenyimwa na mfadhali wao...wao ndo wataweza?...sasa ni lini hili tangazo litawafikia wananchi waishio vijijini?
 
Mleta mada nakkupendaaa
 

Attachments

  • 1432113576502.jpg
    1432113576502.jpg
    36.5 KB · Views: 93
Chama makini cha CHAWADE kinajiandaa kuchukua nchi October.
 
Cha kustaajabisha hiki chama kina wanachama 8000 ambao ni wengi kuliko 6000 wa ACT! Halafu Kuna mijitu humu inasema Zitto ana mvuto! Ana mvuto halafu anapitwa na Chawade kwa wengi WA wanachama?

Sasa wew libichwa lote hilo unashindwa walau kulinganisha mafanikio ya chama na muda wa kuanzishwa kwake ? Baada ya mwaka mmoja CHADEMA ilikuwa na wanachama wangapi?
 
Bora ukimwi....
 

Attachments

  • 1432127909382.jpg
    1432127909382.jpg
    8.5 KB · Views: 110
Sasa wew libichwa lote hilo unashindwa walau kulinganisha mafanikio ya chama na muda wa kuanzishwa kwake ? Baada ya mwaka mmoja CHADEMA ilikuwa na wanachama wangapi?
Mimi nimelinganisha ACT Wasaliti na CHAWADE ambacho hakijapata hata usajili WA kudumu.
 
CHAMA CHA WANANCHI NA DEMOKRASIA
CHAWADE



Phone: +255 789113534, +255 715 039991
Mw/Chai – Matombo na Gombero (house No 28)
chamachawade@yahoo.com


Taarifa kwa Umma

Ndugu wanachama wa CHAWADE, napenda kuchukuwa fursa hii adimu kwa heshima kubwa kuzungumza nanyi kupitia WARAKA huu, mambo muhimu juu ya maendeleo ya chama chetu kitukufu CHAWADE.

Jambo la kwanza ambalo napenda kuzungumza nanyi ni hili la maendeleo ya taratibu za usajiri wa chama chetu. Hadi sasa, taratibu zote zinaendelea vizuri juu ya USAJIRI WA KUDUMU hata hivyo kuna changamoto kadhaa ambazo natumaini tutaweza kuzikabili na hatimaye kupata usajiri wa KUDUMU.

Matarajio yetu ni kuwa kama hapatakuwa na mizengwe kwenye tarehe 20/06/2015 tunaweza kuwa tumepata usajiri wa KUDUMU.

Ndugu wanachama, jambo la pili ambalo napenda kuwafahamisha ni juu ya idadi ya wanachama hadi sasa. Kwa juhudi kubwa ambazo viongozi wa chama chetu wamekuwa wakizifanya juu ya kupata wanachama wapya, hadi sasa ninapowaandikia waraka huu, chama chetu kimefikisha wanachama elfu nane na thelathini na tatu (8,033).

Ndugu wanachama, jambo la tatu ambalo napenda kuwafahamisha ni juu ya ushiriki wetu kwenye UCHAGUZI wa mwaka 2015. Katika uchaguzi wa mwaka huu napenda kuwajulisha kuwa tutashiriki kikamilifu kwa kuweka wagombea kwa nafasi za ngazi mbali mbali (URAIS, UBUNGE NA UDIWANI) katika maeneo yote ndani ya nchi yetu.

Ndugu wanachama, endapo itatokea chama chetu kikawa bado hakijapata usajiri wa kudumu hadi kipindi cha uchaguzi, uongozi wa chama chetu utatoa TAMKO juu ya chama gani na wagembea wepi CHAWADE itawaunga mkono kwa mantiki hiyo tuwe na subira muda ukifika tutafahamishana.

Kwa kumalizia, ndugu wanachama, napenda kuwaomba kuendelea kuwa na SUBIRA pamoja na uvumilivu maana chama chetu bado kipo kwenye mchakato wa kupambana na kuhakikisha tunapata usajiri wa KUDUMU.

Nawashukuru sana kwa ushirkikano wenu katika kukijenga chama chetu.

Asanteni sana na Mungu awabariki.

CHAWADE!!! KWA PAMOJA TUTASHINDA!!!


Shabiri Mpaka
Mwenyekiti Chawade Taifa.


a bunch of twits!
 
Back
Top Bottom