Taarifa kwa watanzania waishio nchini japan | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taarifa kwa watanzania waishio nchini japan

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by SHUPAZA, Mar 15, 2011.

 1. SHUPAZA

  SHUPAZA JF-Expert Member

  #1
  Mar 15, 2011
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 548
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Afisa mwandamizi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Japani , Bw. Francis Mussongo ametoa wito maalum kwa watanzania wanaoishi nchini Japani kuchukua tahadhari kufuatia habari za kuvuja kwa mnunurisho wa nyuklia. Ifuatayo ni taarifa yake kamili.
  Ndugu watanzania mliopo Japani,
  Kwa Mujibu wa taarifa zinaendelea kutolewa na NHK Japan, mitambo ya Nuclear Fukushima Plant (1) kuanzia saa 10 jioni kwa muda wa Japan inatoa radiations na kuna dalili za mlipuko katika kituo hicho, Hali hii imepelekea kutangazwa kwa hali ya dharura na watu wote wa maeneo hayo wanatangaziwa kuondoka maeneo ya karibu na eneo hilo ili kuepusha madhara endapo hali hii itaendelea.


  Endapo mlipuko utatokea kuna uwezekano wa kuleta madhara kwa watu na mali hadi umbali wa kilomita 10 kutoka eneo la Kinu hicho cha Nyuklia. Kwa kutambua kuwa kuna watanzania wenzetu katika eneo la Fukushima kupitia mtandao huu tunaomba wenye mawasiliano na wenzetu waliko Fukushima kuwajulisha kuondoka katika maeneo hayo. Tahadhari pia inatolewa pia maeneo ya Fukushima kuna uwezekano wa kutokea Tsunami tunashauri wenzetu waliko huko wajulishwe kuondoka maeneo ya ufukweni ili kujihami.

  Francis Mossongo,
  Afisa mwandamizi Ubalozi wa Tanzania,Tokyo.

  12, March, 2011
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Mar 15, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,266
  Likes Received: 19,397
  Trophy Points: 280
  nadhani hii taarifa ni ya tr 12/3
  but i hope maofisa watakuwa wanashirikiana na watz walioko huko.
   
Loading...