TAARIFA KWA WANAOSUBIRIA MATOKEO YA UDAHILI SUA

TAARIFA KWA WANAOSUBIRIA MATOKEO YA UDAHILI SUA

hashimrashidy

Senior Member
Joined
Sep 11, 2015
Posts
197
Reaction score
145
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania ilitangaza kukamilisha kuchakata majina ya waombaji wa awamu ya pili tarehe 23/09/2018 na kuwa majina hayo yamekwisha rudishwa vyuoni kwa ajili ya kutangazwa. Kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo SUA hatujaweza kutangaza majina yote ya waombaji waliochaguliwa katika awamu ya pili. SUA inaendelea kufanyia kazi suala hilo ikishirikiana na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania na likikamilika muda wowote majina yatatangazwa.

Tunaomba uvumilivu katika wakati huu mara tutakapo tatua changamoto iliyojitokeza majina yatatangazwa. Mwisho tunaomba radhi tena kwa usumbufu uliojitokeza

IMETOLEWA NA MKURUGENZI,
KURUGENZI YA MASOMO YA SHAHADA ZA AWALI
 
duh kwa kweli inaumiza. watu wameshindwa kuomba awamu ya tatu kwa kuwa hawajui kama wamepata awamu ya pili ama lah. na mbaya zaid deadline ni leo..
 
Back
Top Bottom