Taarifa kwa vyombo vya habari

Speaker

JF-Expert Member
Aug 12, 2010
6,324
2,238
Nimependa sana utetezi wa zitto kuhusu waandishi wa habari na jinsi
wanavo jidai kujua mawazo ya watu kwa kutafsiri kile wanacho ongea.

Zitto ana point,hakuna sababu za kibailojia zinazo mfanya mtu mwenye miaka 30 au 35
asiwe raisi,.............ukizingatia sasa vijana wana barehe mapema sana kuliko enzi hizo
za mababu.

zitto amesema:

Kampeni ya kupunguza umri wa urais haina uhusiano na mimi kutaka kugombea urais 2015

1. Baadhi ya vyombo vya habari vimehusisha kauli yangu ya kutaka kupunguza umri wa kugombea urais
na mimi ‘kuutaka urais’.
Mimi nikiwa mwanachama na kiongozi wa chama chama changu cha CHADEMA naelewa na kuziheshimu
taratibu na kanuni tulizojiwekea za kuomba nafasi mbalimbali za uongozi, ikiwemo nafasi ya urais.
Nafasi ya uongozi ndani ya CHADEMA haiombwi kwenye warsha.
Iwapo chama change, wakati muafaka ukifika na kutokana na matakwa ya jamii,
kikiona nipewe jukumu lolote sitasita kutekeleza wajibu huo niwe au nisiwe mgombea.

2. Kwa hivyo, nilichozungumza jana ni kutoa maoni yangu kwamba muda umefika kwa Taifa letu
kupunguza umri wa kugombea urais.

Maoni yangu haya yanatokana na ukweli kwamba hakuna sababu zozote za kisayansi zinazomfanya
mtu aliye chini ya umri wa miaka 40 akose sifa za kuwa Rais.
Msimamo huu nimekuwa nao tangu zamani nikisoma shule na haujawahi kubadilika.
Hakuna mahala popote katika maoni yangu niliyotoa jana niliposema kwamba nataka umri wa urais
upunguzwe ili nipate fursa ya kugombea nafasi ya urais. Pia siwezi kutaka katiba iandikwe kwa ajili yangu.
Vilevile kamwe isionekane kwamba matakwa ya muda mrefu ya vijana ya kutaka umri wa kugombea Urais
kupunguzwa yanalenga kunipa fursa mimi kwani mimi ni binaadamu naweza nisiwe na sifa za kuwa Rais lakini kukawa
na vijana wengine wengi wenye umri chini ya miaka 40 wenye Uwezo na Uzalendo wa kutosha kushika usukani wa nchi yetu.
Ni maoni yangu kwamba tupate mabadiliko ya vizazi katika uongozi wa nchi yetu ili kukabili changamoto za sasa zinazokabili Taifa letu.


3. Tunapojiandaa kutoa maoni kuhusu Katiba Mpya ni vizuri vyombo vya habari vikajikita kutoa taarifa bila
kuweka tafsiri au kuwatafasiria maoni ambayo wananchi na viongozi watakuwa wanayatoa kuhusu
maudhui ya Katiba Mpya.
 
Hata kama Zitto anautaka uraisi, hilo halina ubaya. Yeyote yule anaweza akautaka uraisi ila mwisho wa siku katika demokrasia wananchi ndiyo final arbiters.

So I don't see where the issue is with him wanting to be president. After-all it's every citizen's right (provided they meet the minimum qualifications).
 
Urais siyo mali ya wazee,mchakato wa kuamua Rais awe na sifa zipi ni wa Watanzania,kila mmoja ana wajibu wa kupendekeza sifa za mgombea urais aweje,ili mradi awe Mtanzania.
Mbona Zitto akitoa maoni yake juu ya kipengele cha kikatiba kuhusu urais watu mnaanza kujiharishia!!!!!! nin nini hii? ni uwoga au nini?Mimi mwenyewe napendekeza miaka 30 mtu aruhusiwe kugombea Urais,ikipitishwa ntachukua fomu na kuomba ridhaa ndani ya chama changu.Pengine vijana watapiga kura kwa sababu kijana mwenzao ntakuwa nimegombea.Maana Wazee waliotuongoza toka Mwinyi hadi Jakaya hawajatuletea Matumaini,Ngoja tuingie sisi wenyewe kama mwl Nyerere.Kosa letu liko wapi.
 
Back
Top Bottom