Mafyangula
JF-Expert Member
- Jan 16, 2025
- 513
- 911
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma inapenda kuwakumbusha viongozi wote wa umma walioainishwa kwa mujibu wa kifungu cha 4 (1) cha Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma (Sura ya 398), kuwa upokeaji wa Tamko la Rasilimali Maslahi na Madeni mwaka 2025, ulioanza tarehe 01 Oktoba, 2025 utamalizika tarehe 31 Desemba, 2025.
Uwasilishaji wa Tamko hilo kwa Kamishna wa Maadili ni kwa mujibu wa kifungu cha 9 (1) (b) cha Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma na kwamba kutoa Tamko la uongo, kuchelewa ama kushindwa kuwasilisha Tamko kwa kipindi kilichoainishwa kisheria ni ukiukwaji wa maadili kwa mujibu wa kifungu cha 16 cha Sheria tajwa.
Aidha utoaji wa tamko hilo unafanyika kwa njia ya Mtandao (Online Declaration system - ODS).
Viongozi ambao walishawahi kutoa Tamko kwa njia ya mtandao watatumia taarifa "credentials" walizotumia awali na kuendelea na utoaji wa Tamko. Kiongozi ambaye hajawahi kutoa Tamko atatakiwa kuingia kwenye Mfumo kupitia anuani ods.maadili.go.tz na kubofya kitufe kilichoandikwa jisajili kisha atafuata maelekezo yatakayomsaidia kujisajili na kuendelea na zoezi la utoaji wa Tamko husika.
Ikumbukwe kuwa hakutakuwa na muda wa nyongeza wa kuwasilisha Tamko.
Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa kupitia barua pepe helpdesk@maadili.go.tz. au simu +255262160199/+255262160192/+255734101040.
Imetolewa na:
Jaji (Stahiki) Sivangilwa S. Mwangesi
KAMISHNA WA MAADILI
Jengo la Maadili, 1 Mtaa wa Maadili, S.L.P 225, Dodoma, Simu: 026-2160190, Barua pepe: ec@maadili.go.tz Tovuti: MAADILI | JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - Mwanzo