Taarifa kwa Umma: Zahanati ya Mtama mkoani Mara kutoa huduma ya vipimo kwa wajawazito mezani na watoto chini ya mti

Wizara ya Afya Tanzania

Verified Member
Oct 1, 2020
31
125
TAARIFA KWA UMMA - ZAHANATI YA MTAMA MKOANI MARA KUTOA HUDUMA YA VIPIMO KWA WAJAWAZITO MEZANI NA WATOTO CHINI YA MTI

IMG-20210122-WA0006.jpg

MALALAMIKO YA WANANCHI:
Wananchi katika kijiji cha Nyagisya kata ya Kiore wilayani Tarime mkoani Mara wamelazimika watoto wao kupewa huduma ya Kliniki chini ya mti wa muembe huku wakining'inizwa juu ya mti kupimwa uzito na wajawazito nao wakilazwa juu ya meza,madawati,sakafuni ili kupata huduma za afya.

Akina mama wakiwa wamebeba watoto wao pamoja na wajawazito walisema kuwa wanalazimika kufanya hivyo kwa kuwa kijiji hakina zahanati na kwamba huduma hiyo ya kliniki hutolewa mara moja kwa kila mwezi.

Pia walisema kuwa wanaepuka umbali wa kilomita 4 kwenda kupata huduma ya Kliniki katika zahanati ya Mtana kata ya Manga,umbali wa km 12 kwenda zahanati ya Gamasara kata ya Nyandoto na hospitali ya wilaya ya Tarime iliyopo umbali wa km14.

Furaha Joseph mkazi wa kijiji hicho alisema,"mimi ni mmoja wa akina mama tunaoteseka kuitafuta huduma ya afya hatuna zahanati ukiugua,au kwenda kupata huduma ya clinic mpaka ujipange uwe na nauli elfu 3,000 ya pikipiki kwenda Mtana,na 5000 kwenda hospitali ya wilaya kama hauna inabidi utembee kwa miguu inachosha".

Happines Johanes alisema kuwa wanapokwenda kwenye zahanati hizo baadhi ya watoa huduma hukataa kuwapa huduma na kuwataka kwenda zahanati ya Gamasara au hospitali ya wilaya jambo ambalo liliwalazimu kuomba kupewa huduma ya kliniki katika kijiji chao ili kuepuka usumbufu.

"Tukienda Mtana nesi wanatuambia nyie nao mnatusumbua si mjenge zahanati yenu? mnakuja tu kurundikana hapa,ukiwa unaanza kliniki wanakusukuma kwenda hospitali ya wilaya. Tunashukuru serikali yetu ya kijiji ilikaa ikaona ni kwanini tuendelee kuteseka tukaona ni bora huduma ya kliniki tuifanye hapa kwetu hata kama ni chini ya mti inatusaidia kupunguza umbali na gharama za nauli na kauli mbalimbali za kukatisha tamaa", alisema Johanes.

Kutolewa huduma hiyo ya kliniki chini ya mti bado ni changamoto kwa akina mama wenye watoto na wajawazito kwa kuwa mvua ikinyesha hutangatanga kutafuta mahali pakufanyia huduma na kujikinga mvua hali ambayo wakati mwingine watoto kupimwa uzito huku nguo ikifungwa juu ya kenchi kwenye madarasa shule ya msingi Nyagisya na Wajawazito kulala juu ya madawati,meza na sakafuni kupata huduma ya cliniki.
 
VAPS

JF-Expert Member
Jul 10, 2012
4,629
2,000
Asante kwa taarifa. Ushauri wangu tupunguze kurusha live baadhi ya matukio hususani miradi ya maendeleo huko Chato.
 
tamsana

JF-Expert Member
Jan 13, 2012
903
1,000
Kulikuwa na haja gani taarifa kwa umma kusainiwa na Waziri. Anyway, naipongeza Wizara kwa kukubali tatizo, nilifikiri wangekanusha.
 
Simba zee 33

JF-Expert Member
Sep 15, 2020
1,374
2,000
TAARIFA KWA UMMA - ZAHANATI YA MTAMA MKOANI MARA KUTOA HUDUMA YA VIPIMO KWA WAJAWAZITO MEZANI NA WATOTO CHINI YA MTI

MALALAMIKO YA WANANCHI:
Wananchi katika kijiji cha Nyagisya kata ya Kiore wilayani Tarime mkoani Mara wamelazimika watoto wao kupewa huduma ya Kliniki chini ya mti wa muembe huku wakining'inizwa juu ya mti kupimwa uzito na wajawazito nao wakilazwa juu ya meza,madawati,sakafuni ili kupata huduma za afya.

Akina mama wakiwa wamebeba watoto wao pamoja na wajawazito walisema kuwa wanalazimika kufanya hivyo kwa kuwa kijiji hakina zahanati na kwamba huduma hiyo ya kliniki hutolewa mara moja kwa kila mwezi.

Pia walisema kuwa wanaepuka umbali wa kilomita 4 kwenda kupata huduma ya Kliniki katika zahanati ya Mtana kata ya Manga,umbali wa km 12 kwenda zahanati ya Gamasara kata ya Nyandoto na hospitali ya wilaya ya Tarime iliyopo umbali wa km14.

Furaha Joseph mkazi wa kijiji hicho alisema,"mimi ni mmoja wa akina mama tunaoteseka kuitafuta huduma ya afya hatuna zahanati ukiugua,au kwenda kupata huduma ya clinic mpaka ujipange uwe na nauli elfu 3,000 ya pikipiki kwenda Mtana,na 5000 kwenda hospitali ya wilaya kama hauna inabidi utembee kwa miguu inachosha".

Happines Johanes alisema kuwa wanapokwenda kwenye zahanati hizo baadhi ya watoa huduma hukataa kuwapa huduma na kuwataka kwenda zahanati ya Gamasara au hospitali ya wilaya jambo ambalo liliwalazimu kuomba kupewa huduma ya kliniki katika kijiji chao ili kuepuka usumbufu.

"Tukienda Mtana nesi wanatuambia nyie nao mnatusumbua si mjenge zahanati yenu? mnakuja tu kurundikana hapa,ukiwa unaanza kliniki wanakusukuma kwenda hospitali ya wilaya. Tunashukuru serikali yetu ya kijiji ilikaa ikaona ni kwanini tuendelee kuteseka tukaona ni bora huduma ya kliniki tuifanye hapa kwetu hata kama ni chini ya mti inatusaidia kupunguza umbali na gharama za nauli na kauli mbalimbali za kukatisha tamaa", alisema Johanes.

Kutolewa huduma hiyo ya kliniki chini ya mti bado ni changamoto kwa akina mama wenye watoto na wajawazito kwa kuwa mvua ikinyesha hutangatanga kutafuta mahali pakufanyia huduma na kujikinga mvua hali ambayo wakati mwingine watoto kupimwa uzito huku nguo ikifungwa juu ya kenchi kwenye madarasa shule ya msingi Nyagisya na Wajawazito kulala juu ya madawati,meza na sakafuni kupata huduma ya cliniki.
HUU ni uongo watanzania wenzangu
Serikali ya awamu hii ya Rais mwema mwenye Moyo wa huruma na upendo kwa RAIA wake amejenga zahanati na hospital kila kona
Wapiga dili wamadhalilisha nchi yetu bure
Sisi tupo Uchumi wa kati
Sio kama zamani
 
Kertel

JF-Expert Member
May 11, 2012
4,326
2,000
Sasa huko si ndio ipelekwe bombadier moja ikatumike kama majengo ya zahanati,nchi tajiri hii bwana.
 
OttoThyPrince

Member
Jun 24, 2020
60
95
HUU ni uongo watanzania wenzangu
Serikali ya awamu hii ya Rais mwema mwenye Moyo wa huruma na upendo kwa RAIA wake amejenga zahanati na hospital kila kona
Wapiga dili wamadhalilisha nchi yetu bure
Sisi tupo Uchumi wa kati
Sio kama zamani
Jinga kweli wewe
 
Statesman

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
23,277
2,000
Karibuni Sana Jamii Forums Wizara ya Afya, mmekua mfano kwa Wizara nyingine.

Tunajarajia watumiaji wa mtandao huu watatumia fursa hii adhimu kuwasilisha changamoto zao kwenu kwa utatuzi.

Niwatakie kazi njema katika Ujenzi wa Taifa letu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom