Taarifa kwa umma kuhusu vijana kujiunga na JKT

SniperBoi

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2016
Posts
1,104
Reaction score
1,135
TAARIFA KWA UMMA
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) linapenda kuutaarifu umma juu ya utapeli unaoendelea kufanywa na baadhi ya watu wanaojifanya wanauwezo wa kuwaingiza vijana wa kitanzania kwenye mafunzo ya JKT kwa lengo la kupatiwa malipo.

Utapeli huo unafanyika kwa njia ya simu za mkononi kwa kutuma ujumbe mfupi wa maneno tofauti tofauti.

Jeshi la Kujenga Taifa linasisitiza kuwa ujumbe huo siyo sahihi na wananchi wanatakiwa kujiepusha na utapeli huo wenye lengo la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Taarifa za mchakato wa uchukuaji wa vijana wa kujiunga na mafunzo ya JKT utolewa na Makao Makuu ya JKT kwa mfumo ulio rasmi wa mawasiliano ikiwemo luninga, radio, magazeti na tovuti ya JKT.

Aidha, JKT kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, inafuatilia kujua ni mtu gani au kikundi kipi kinahusika na utapeli huo ili hatua kali za kisheria ziweze kuchukuliwa.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa
Tarehe 17 Oktoba 2016
CHANZO: www.jkt.go.tz
 
Wafute tuu vijana wameshakata tamaa ya kwenda huko na wengi wao walishabadilisha mitazamo ya maisha so kwenda jkt sio kipaumbele chao.
 
TAARIFA KWA UMMA
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) linapenda kuutaarifu umma juu ya utapeli unaoendelea kufanywa na baadhi ya watu wanaojifanya wanauwezo wa kuwaingiza vijana wa kitanzania kwenye mafunzo ya JKT kwa lengo la kupatiwa malipo.

Utapeli huo unafanyika kwa njia ya simu za mkononi kwa kutuma ujumbe mfupi wa maneno tofauti tofauti.

Jeshi la Kujenga Taifa linasisitiza kuwa ujumbe huo siyo sahihi na wananchi wanatakiwa kujiepusha na utapeli huo wenye lengo la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Taarifa za mchakato wa uchukuaji wa vijana wa kujiunga na mafunzo ya JKT utolewa na Makao Makuu ya JKT kwa mfumo ulio rasmi wa mawasiliano ikiwemo luninga, radio, magazeti na tovuti ya JKT.

Aidha, JKT kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, inafuatilia kujua ni mtu gani au kikundi kipi kinahusika na utapeli huo ili hatua kali za kisheria ziweze kuchukuliwa.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa
Tarehe 17 Oktoba 2016
CHANZO: www.jkt.go.tz

Jk alikuwa mtu wa kuunda kuunda tume maharage yeye naona kaja na hii mpya ya kutumia future tense si katika matamko yake au yale yanayotolewa na wasaidizi wake. Utasikia taarifa ita..tuta..wata...mchakato uta...[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom