Taarifa kwa umma kuhusu madai ya TRA kupandisha ushuru wa magari toka nje ya nchi

Tatizo TRA mnaamini kuwa na gari ni anasa, alafu mnasahahu kuna Kodi za mafuta,vilainishi, vipuli na accessories, leseni, wiki ya usalama, Kodi kwenye gerage rasmi na zisizo rasmi, packing fees, za kubrashia viatu, bima nk.

Naamini magari yakiwa mengi mtachuma kutoka huku kote, kuliko haka ka 15 au 30% ka uchakavu mnakokomalia as once off.

Usafirishaji wa bidhaa kutoka bushi itakuwa rahisi na ghalama za maisha zitashuka
 
Kufuatia taarifa iliyoko katika mtandao wa Kijamii ikidai TRA imepandisha ushuru wa magari tunapenda kukanusha na kufafanua kama ifuatavyo;

1. Viwango vya kodi vinapitishwa na bunge na sio TRA.

2.Kodi hukokotolewa kwa kuzingatia thamani ya gari kwenye soko la dunia, gharama ya usafirishaji na bima. Ikiwa gari limenunuliwa kwa fedha za kigeni kiwango cha kubadilisha fedha cha siku husika kitatumika na sio ya wakati wa kuagiza gari hilo hivyo huenda ikatofuatiana na kiwango cha kikokotoo wakati wa kuagiza.

3. Umri wa gari unaweza kusababisha kodi ikaongezeka kutokana na uchakavu, kwa magari yaliyotengenezwa zaidi ya miaka 8 lakini haifiki miaka 10 kodi ya uchakavu ni 15% na gari lenye umri kuanzia miaka kumi na kuendelea tangu limetengenezwa kodi ya uchakavu ni 30%.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi bure kwa simu namba 0800110016 au 0800 750075 au 0800 780078 siku ya Jumatatu mpaka Ijumaa kuanzia saa 2 kamili asubuhi mpaka saa 1 kamili jioni au tuma barua pepe kwenda huduma@tra.go.tz.

Pamoja tunajenga taifa letu

Imetolewa na: Idara ya Elimu kwa Mlipakodi na Mawasiliano
Msimamo wetu ni upi ikiwa tunapinga gari chakavu kwa kuziwekea ushuru mkubwa wakati huo huo ukinununua gari mpya huo ushuru wake pia ni moto wa kuotea mbali?
Kwanini kusiwe na flat rate ya kodi ya kuagiza gari badala ya kuwa kodi ya kusema eti inategemea hali ya thamani ya fedha za kigeni kwa siku hiyo wakati kodi tunalipa kwa fedha ya ndani?
Kutokuwepona mifumo inayoeleweka ya kodi imepelekea wengine kushindwa kukomboa gari zao baada ya kuwasili hali inayosababishwa na mabadiliko ya ghafla ya viwango vya kodi tofauti na iliyokadiriwa hapo awali
 
Gharama za kuingiza magari Tanzania ziko fair kabisa sidhani itakuwa busara kupunguza zaidi ya hapa zilipo. Hata rate ya kuingiza magari ni nzuri sana na hii inamaanisha kuwa kodi zinalipika. Gharama zikupunguzwa zitafanya nchi igeuke jalala la magari chakafu na pia msongamano wa magari. Cha muhimu ni kuwa fedha zinatopatikana zitumike kwenye maendeleo ya nchi na siyo jinsi zinavyotapanywa sasa hivi kwa viongozi kuishi maisha ya anasa.
Mawazo ya kimasikini kabisa, as if ni kosa la mwananchi kutokuwepona miundombinu ya kutosha kuhimili gari zitakazoagizwa.
Ni sawa na kumwambia kijana wako jitahidi uwe mjinga na ujibu vibaya mitihani ili usichaguliwe kwenda sekondari maana kusoma ni gharama mimi sitamudu
 
Kwa hili la magari ya chini ya miaka 8 au yasizidi 10 kwa kweli mnaumiza watu at least mngefanya 12 years old ili wengi waweze kumudu kununua
Nadhani lengo sio kumudu, ila watakaoangukia kwenye kundi hilo wawe wengi mapato yaongezeka.
TRA kila mwaka hujiwekea malengo ya kuongeza makusanyo bila kuwa na mkakati wa kuhakikisha ustawi wa walipa kodi.
Ni kama mfugaji anayetaka maziwa mengi bila mkakati wa kumhudumia vizuri ng'ombe
 
Tatizo sio kulipa kodi tatizo hatuoni kodi zetu tunazolipa zinafanya kazi gani,,?
 
Unafiki mtupu viongozi wa hapo,Uongo ndiyo tabia yao,Wanasingizia wabunge wanafanya majambo kwa manufaa yao.
 
Inakuwaje gari ikiagizwa Zambia au Malawi ushuru wake ni mdogo kuliko Tanzania wakati zote zinapitia bandari ya Dar Tz?
Nafkr bandari huwa inakata Tu gate fee , alaf kule kwao mamlaka zao zina viwango tofaut na zetu , hvyo gar zao zinakuwa ni cheap, tofaut na sie gari zinazotumika bongo zinakatwa makoro koro yote pamoja
 
Mawazo ya kimasikini kabisa, as if ni kosa la mwananchi kutokuwepona miundombinu ya kutosha kuhimili gari zitakazoagizwa.
Ni sawa na kumwambia kijana wako jitahidi uwe mjinga na ujibu vibaya mitihani ili usichaguliwe kwenda sekondari maana kusoma ni gharama mimi sitamudu
Mawazo yangu ni ya kitajiri. Kama huna fedha ya kulipia kodi basi baki na umaskini wako.
 
Hii sheria ya kuwekea magari yenye umri mkubwa sio sahihi kabisa inamaana mtu akiwekewa kodi kubwa na akalipa je garii itapungua umri? Tusidanganyane watanzania kununua gari yenye umri mdogo uchumi kwa wengi hauturuhusu tutapambania magari ya 2005-2009 huko
Nchi zilizoendelea zinajua umuhimu wa usafiri kwa raia gari mpaka dola 500 na inatembea vizuri lakini hapa kukomoana na kufanya maendeleo yawe duni hasa mikoani
 
Kufuatia taarifa iliyoko katika mtandao wa Kijamii ikidai TRA imepandisha ushuru wa magari tunapenda kukanusha na kufafanua kama ifuatavyo;

1. Viwango vya kodi vinapitishwa na bunge na sio TRA.

2.Kodi hukokotolewa kwa kuzingatia thamani ya gari kwenye soko la dunia, gharama ya usafirishaji na bima. Ikiwa gari limenunuliwa kwa fedha za kigeni kiwango cha kubadilisha fedha cha siku husika kitatumika na sio ya wakati wa kuagiza gari hilo hivyo huenda ikatofuatiana na kiwango cha kikokotoo wakati wa kuagiza.

3. Umri wa gari unaweza kusababisha kodi ikaongezeka kutokana na uchakavu, kwa magari yaliyotengenezwa zaidi ya miaka 8 lakini haifiki miaka 10 kodi ya uchakavu ni 15% na gari lenye umri kuanzia miaka kumi na kuendelea tangu limetengenezwa kodi ya uchakavu ni 30%.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi bure kwa simu namba 0800110016 au 0800 750075 au 0800 780078 siku ya Jumatatu mpaka Ijumaa kuanzia saa 2 kamili asubuhi mpaka saa 1 kamili jioni au tuma barua pepe kwenda huduma@tra.go.tz.

Pamoja tunajenga taifa letu

Imetolewa na: Idara ya Elimu kwa Mlipakodi na Mawasiliano
Jibuni maswali mmeulizwa mnakaa kimya,mmekuja kufafanua nini hpa
 
Hii sheria ya kuwekea magari yenye umri mkubwa sio sahihi kabisa inamaana mtu akiwekewa kodi kubwa na akalipa je garii itapungua umri? Tusidanganyane watanzania kununua gari yenye umri mdogo uchumi kwa wengi hauturuhusu tutapambania magari ya 2005-2009 huko
Wanafata principal ya kipumbavu ya kuzuia dumping ilikuwepo kabla ya recycling industry kuja.
Haina maana siku hizi sababu magari chakavu yanasagwa chuma chakavu zamani yalitupwa dampo.
 
  • Thanks
Reactions: JMF
Nchi zilizoendelea zinajua umuhimu wa usafiri kwa raia gari mpaka dola 500 na inatembea vizuri lakini hapa kukomoana na kufanya maendeleo yawe duni hasa mikoani
Muendelezo wa Roho ya kiswahili wachache ndio wamiliki magari
 
Kuingiza IST bongo USA ulaya yote kwa Hela hio unasukuma bmw,vokswagon tuareg,GMC pick up,
 
Gharama za kuingiza magari Tanzania ziko fair kabisa sidhani itakuwa busara kupunguza zaidi ya hapa zilipo. Hata rate ya kuingiza magari ni nzuri sana na hii inamaanisha kuwa kodi zinalipika. Gharama zikupunguzwa zitafanya nchi igeuke jalala la magari chakafu na pia msongamano wa magari. Cha muhimu ni kuwa fedha zinatopatikana zitumike kwenye maendeleo ya nchi na siyo jinsi zinavyotapanywa sasa hivi kwa viongozi kuishi maisha ya anasa.
 
Gharama za kuingiza magari Tanzania ziko fair kabisa sidhani itakuwa busara kupunguza zaidi ya hapa zilipo. Hata rate ya kuingiza magari ni nzuri sana na hii inamaanisha kuwa kodi zinalipika. Gharama zikupunguzwa zitafanya nchi igeuke jalala la magari chakafu na pia msongamano wa magari. Cha muhimu ni kuwa fedha zinatopatikana zitumike kwenye maendeleo ya nchi na siyo jinsi zinavyotapanywa sasa hivi kwa viongozi kuishi maisha ya anasa.
Huku ni kuwakosesha raia vyombo vya usafiri huku wao wakitumia mwanya wa nafasi zao serikalini kukwepa kodi pindi wanapoagiza magari toka ng'ambo tena kwa pesa za walipa kodi wanazozikwapua.

Wazo la kupunguza msongamano wa magari halina mashiko kwani wajibu wa kujenga barabara ni wa serikali kupitia kodi za wananchi vinginevyo ni kudhirisha kuwa serikali imejaa ufujaji wa pesa za uma na kutokuwajibika.
 
Back
Top Bottom