Taarifa kwa abiria wa udart kituo cha Ubungo maji

UDA Rapid Transit

New Member
Joined
Jul 4, 2018
Posts
4
Reaction score
6
TAARIFA KWA UMMA

Dar es Salaam, Julai 26, 2018

Kampuni inayotoa huduma kwenye mfumo wa mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam, UDA Rapid Transit (UDART), inachukua nafasi hii kuujulisha umma kuwa kutokana na shughuli za ujenzi wa barabara za juu kwenye makutano ya barabara za Morogoro, Nelson Mandela na Sam Nujoma (Ubungo Interchange), tunalazimika kubadili utaratibu wa mabasi yaliyokuwa yakianzia na kumalizia safari zake katika Kituo cha Ubungo Maji.

Mabadiliko haya yataanza Jumatatu hii ya Julai 30, 2018; na yatakuwa kama ifuatavyo:

  1. Nyakati za asubuhi mabasi yanayotoa huhuma ya EXPRESS katika ruti namba 002 (yaani Ubungo kuelekea Kivukoni) pamoja na ruti namba 005 (Ubungo – Gerezani) yataanzia Ubungo Terminal badala ya Ubungo Maji.

  2. Nyakati za mchana na jioni mabasi ya ruti hizo yataendelea na huduma za kawaida zisizokuwa EXPRESS; lakini badala ya kuishia Ubungo Maji, sasa yataishia Ubungo Terminal.

Kutokana na mabadiliko haya, tunawashauri abiria wetu waliokuwa wakitumia Kituo cha Ubungo Maji sasa waanze kukitumia zaidi Kituo cha Ubungo Terminal ili kupunguza usumbufu.

Wakati wote wa shughuli hizo za ujenzi wa barabara za juu Ubungo, mabasi ya mwendo wa haraka yatakuwa yakitumia njia moja tu (single lane) kuanzia mataa ya ubungo kuelekea Kimara, ndio maana sasa mabasi yetu yataishia Ubungo Terminal ili kupunguza msongamano wa magari Kituo cha Ubungo Maji wakati wa kushusha na kupakia abiria.

Tunaomba radhi kwa usumbufu wa muda utakaojitokeza wakati huu serikali ikiboresha miundombinu ya usafirishaji jijini Dar es Salaam.

Asanteni sana.

Imetolewa na Deus Bugaywa

Mkuu wa Idara ya Mawasiliano UDART

NB:

Huduma ya Kimara kuelekea mjini, Morocco na kurejea Kimara haitaathiriwa na mabadiliko haya.
 
Taarifa ndio uhai wa huduma.Hongereni kwa kuwa na weledi wa namna hii.
 
Asante kwa taarifa
Swali kwenu? Hivi mbona Huduma zenu za kukata ticket pale kimara mwisho ni mbovu

Ova
 
God bless you dear!!
 
Karibu sana New Member
 
Back
Top Bottom